Sasa Nimeamini JF ni kila kitu, hatimae am in a relationship!!!

grand-mal

JF-Expert Member
Feb 22, 2013
337
176
Habari wana MMU,

Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa mlionipa ikiwa, ni pamoja na ushauri na uungwaji mkono mkubwa uliofanywa na wote walioniandikia private messages katika huu uzi https://www.jamiiforums.com/love-connect/405796-a-serious-woman-to-join-in-marriage.html. Ulikuwa ni mtihani mzito kwangu, kwani ni kazi sana kuanzisha mahusiano na mtu ambaye hamjawahi kuonana wala hamjuani lakini imewezekana.

Nimekuwa kwenye mchakato kwa muda mrefu, nimeongea na wengi, nimeonana na baadhi. Wengi wanafaa kuwa wake lakini nilikuwa nahitaji mmoja tu. Nashukuru kwamba mmoja huyo nimempata, japo tuko bado katika kipindi cha matazamio. Tumeongea tumeelewana na tunadhani 'we are compatible' , naendelea kuomba ili malengo yetu yatimie. Tumekubaliana kwamba tunaweza kuishi pamoja lakini tuwe kwenye uhusiano wa kawaida wa sasa, nasisitiza uhusiano wa kawaida. Yeye ni member humu, na tunategemea wakati muafaka ukifika tutaweka mambo hadharani, na najua itakuwa surprise kwa wengi, lakini jamani inawezekana.

Tumepanga tukijaaliwa ndoa ifungwe jamiiforums kuonyesha shukrani zetu. Siku hiyo tunataka mkuu Invisible awe visible, mkuu Paw hatutapenda kuona pingu zako siku hiyo, kwani itakuwa full shangwe na watu wataruhusiwa 'ku-misbehave' bila kupewa ban.

Nitaomba dada yangu lara 1 awe mbali na mchumba wangu mtarajiwa asije akaanza kumpa ushauri wa kuingia nusunusu, yale mambo yake ya mguu ndani mguu nje hapana, hatuyataki. Sisi tuko serious na tunategemea kupendana kwa dhati kama tulivyoanza.

Mkuu Mtambuzi na Nicas Mtei ninawashukuru sana kwani nyuzi zenu zilinifariji sana na kunifanya nisikate tamaa.

Kaunga michango yako imetuunganisha. Nawshukuru wote humu hata ambao sijawataja.

Siku hiyo natamani iwe kesho kwani itakuwa furaha sana, Smile na wote wengine itakuwa ni smile tu.

Nasema tena nashukuru sana na tuombeane heri ili mambo yetu yaende kama tulivyopanga. Inawezekana kupata mwenza popote. Mungu anaweza kutumia njia yoyote kukupa mwenza kama ukimuomba.

Kwa uzi huu pia naomba niseme imetosha, no more private messages.

Nina furaha sasa jamani.

Its me grand-mal.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom