Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Kweli magonjwa yako mengi na tunajua kila mtu anayekwenda kule kwa Babu Loliondo anataka kupata ile dawa ili apone maradhi sugu kama babu alivyosema kua dawa ile ambayo ameoteshwa na Mungu kama alivyonukuliwa na vyiombo vya habari. Babu kasema dawa ile inatibu magonjwa sugu kama vile Pumu/Kisukari/Kansa/Presha/Ukimwi na vidonda vya tumbo. Sasa hii niliyoisikia kwa jamaa waliofunga safari tena kwakutumia nauli kubwa tu na kwenda kushinda kwenye mazingira magumu kule Loliondo wamekwenda kupata dawa kwa Babu ili waongeze nguvu za kiume! Jamani hembu kwa wale waliotoka kwa babu hizi siku mbili je Babu ameshaanza kutoa tiba hii ya kuongeza nguvu za kiume? mimi nilitoka huko wiki kadhaa lakini sikusikia kama kuna matibabu haya! Nawasilisha.