mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,411
- 7,016
Jumatano nzuri!
Nina tafakuri hapa. Kama dini ni utapeli, nikimaanisha Ukristo na Uislamu zote, sasa Mungu aabudiwe kwa njia gani? Ni kwamba watu wasiende makanisani? Misikitini?
Na je, dini zililetwa hasa kwa lengo lipi? Na hao waliozileta dini wanafaidikaje?
Au walifaidikaje? Je, wanaendelea kufaidika?
Unaamini Mungu wa kweli anakutaka uende kanisani au msikitini kumuabudu?
Unamuabudu Mungu kipofu au aonaye?
Babu zetu waliabudu Mungu aliyejibu... kwamba watu waliomba na mvua zilinyesha kwa WAKATI.
Watu waliomba na dawa za matatizo mbali mbali zilipatikana. Watu walipewa vipawa mbali mbali ikiwemo kuwa hodari kwenye miti ya dawa nk!
Mungu alijibu maombi ya wazee wetu. Siku hizi ukuomba unajibiwa na Mungu? Usijilishe mawazo na imaginations zako ukadanganya watu umejibiwa. Acha utaahira!
Nina kila sababu ya kusema dunia ya leo 99% ya Mungu anayeabudiwa na wengi hajibu maombi ya watu wake. Hali inapelekea watu wengi kuwa kama vichaa wa imani.
Jiulize! Kwa nini wazee wetu walijibiwa na sasa hivi WEWE na wenzako hamjibiwi???
Watu wengi wanasingizia wakati wa Mungu haujafika, pale ambapo wanaomba na hawajibiwi.
Mawasiliano ni two way basis. Unaomba, unapewa, au unaelezwa kusubiri kidogo, au unakataliwa kwa sababu a, b, c! Sasa wengi leo wanadanganya wamejibiwa kumbe si kweli.
Dalili za uongo kwenye dini ni Mungu kutojibu maombi ya watu wake. Hakuna impact chanya kwa watu, ambayo inaweza kudhihirika.
Yote haya yalianza baada ya ujio wa Ukristo kutoka kwa Wakoloni, pamoja na Uislamu.
Nafikiri ni njama za kuwatenga weusi na Miungu yao yenye nguvu SANA. Leo hii kijana kuchinja ng'ombe au mbuzi na akagawa nyama kwa wahitaji, anaona ni ushirikina.
Kuwanunulia wazee pombe wanywe wafurahi, kijana anaona ni DHAMBI, ni ushirikina.
Huwaheshimu wazee wa kwenu ila unawaheshimu wazee wa Rome na Oman.
Kijana kufanya tambiko kwa wazee wako waona ni ushirikina. Huko ndiko kwenye kuwakumbuka wazee na kwenye majibu mengi.
Usiogope kusimamia haki!
Dini zililetwa kutupumbaza, tena kwa makusudi. Uongo???
Mungu alikuwa Afrika hata kabla ya ujio wa Ukristo na Uislamu. Kutembea na mke wa mtu haikukubalika enzi za babu zetu. Kudhulumu(udhulmati) haukukubalika, uonevu, wivu, husuda, vijicho nk!
Kipi kipya dini zimeleta?
Mungu Muumba wa Afrika ni wakati sasa aanze kupewa heshima yake. Hizi dini koloni tuzitupe kule. Hazina faida.
Dini ya kweli ni kumpenda mwenzio kama nafsi yako na kuwajali yatima na wajane. Mambo haya yote yalikuwa kwetu hata kabla ya kuja kwa dini za Wakoloni.