Sasa hivi watu wanavaa uniform za kazini mitaani

Sasa hivi watu wanavaa uniform za kazini mitaani kuturingishia kuwa wana kazi, zamani walikuwa wanavalia kazini

Maisha yamebadilika zamani mtu alikuwa anaona aibu kuondoka nyumbani akiwa kavaa uniform ya kazini na kurudi nayo kavaa .Walikuwa wakienda kubadlishia kazini na akitoka anaingia chooni anabadilisha ndio anarudi nyumbani.

Sasa hivi mtu anaondoka nyumbani anapanda daladala na uniform na kurudi akiwa na uniform yenye nembo ya kazini kwake kuringisha kote apitako Kuwa Yeye ana ajira.

Waajiri wa sasa hawana kazi kubwa kuhamasisha wafanyakazi kuvaa uniform tofauti na zamani.

Kweli kila enzi na zama zake loo.

Mnaofanya kazi wenye uniform karibuni mtaani kwetu mtukoge
Ila sio ya rangi ya Ugoro kama suti ya NSSF
 
Ipo siku utasema wanayanga tunaringa na jezi zetu, na tutazitinga ile mbaya
FB_IMG_1629891302832.jpg
 
Jirani yangu anafanyia Lugalo anatoka na gwanda zake anaenda kuvalia kazini!

Yaani mimi ningekuwa yeye ningevalia hukuhuku mtaani ili nisilipe nauli😂
 
Tuulize wahenga.

Au labda ukisema zamani unamaanisha nini?

Kwanza mabasi ya viwanda na makampuni yote. karibu kila kiwanda kilikuwa na mabasi yake yanawateremsha wafanyakazi kwenye vituo vikubwa Dar.

Halafu walikuwa wanavaa uniforms.

Wafanyakazi wa customs na bandari kuna mpaka uniforms za Jumatano.
Tulipokuwa Jeshi la Kujenga Taifa kipindi hicho Operesheni Nyerere vijana tuliokuwa mafunzoni na tunafanyakazi kwenye mashirika ya umma tulipaswa kuvaa kombati zetu maofisini wakati wote..
 
Hata mi siku hizi natembea na boya la kuogelea(life jarket) kuwalingishia watu mtaani kuwa nimeajiriwa kwa njiwa poli. Au nasema uongo ndugu zangu
Mkuuu Hamia kwa Kitana njiwa pori miyeyusho. Karibu mitaa yetu hapa Kayenze na huko Igombe wape Hi washkaji akina White!
 
Poor mindset,inferiority complex and poor level of thinking which may result from both malnutrition and pschological issues!
Ndo nyie wavaa unifomu kwa wingi mnajifanya mnajua Kizungu. Kila post.... Poor mindset "come on"
 
Back
Top Bottom