Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,068
12,498
Mjadala unaendelea muda huu kwenye Twitter Spaces ya JamiiForums Septemba 29,2022.

3095832E-C4A8-4633-9270-79444204D92B.jpeg


Unaweza kusikiliza kupitia kiunganishi hiki hapa >>> JF SPACES

Dr. Shakilu Jumanne
Tunachoongelea hapa ni uvimbe unaotokea tumboni. Ni magroup ya magonjwa kadhaa yanayo sababisha saratani tumboni.

Dr. Fat-Hiya
Satarani inaongoza kwa vifo hapa kwetu na duniani kote, kwa Muhimbili ni kama wagonjwa 800 kwa mwaka wanaogundulika.

Tatizo kubwa ni kuwa wagonjwa wengi wanakuja kwenye wakati ambao ugonjwa unakuwa mkubwa, ni ngumu kutibu kwa wakati huo.

Saratani ya mafigo ndiyo inaongoza kwa umri wa miaka 3-4, na saratani ya matezi inafuata kwa watoto chini ya miaka 10.

Pia kuna saratani za ini, misuli n.k

Dalili zinazoonekana sana ni uvimbe ambao mara nyingi huchelewa kugundulika kwa kuwa huwa hauna maumivu. Huendelea kwa kufanya watoto wachoke sana, kudhoofika na kudumaa na baadae inaweza kubana mishipa ya mwii na utumbo. Anaweza kuanza kukosa choo vizuri.

Anaweza pia kuwa anakojoa damu, au kuishiwa damu mara kwa mara. Dalili zote hizi zinategemea na aina ya saratani.

Homa pia huonekana, homa hizi huwa hazisikii matibabu ya kawaida tunayoyafahamu.

Tumbo linaweza kujaa, maji kujaa kwenye mapafu, mtoto hakui vizuri na anaweza kupata changamoto za upumuaji.

Dr. Mohamed
Kawaida uvimbe ktk tumbo unaweza kuwa wa aina nyingi, unaweza kuwa katika tezi (neuroblastoma) ambao ndiyo unaonekana zaidi hapa Tanzania, kisha uvimbe wa figo, ini na ktk damu.

Kabla ya upasuaji ni muhimu kufahamu aina ya uvimbe, siyo kila uvimbe unahitaji upasuaji.

Mfano ni lymphoma, mara nyingi tunatumia tu chemotherapy kwa kuwa wakati mwingine huwa upo sehemu mbaya, mfano kwenye mayai ya watoto wa kike. Ukitoa maana yake umemuondolea mayai.

Mfano mwingine ni uvimbe kwenye figo ambao husambaa kwenye kifua na ini, mara nyingi hupata chemotherapy kwanza kabla ya upasuaji kwa kuwa uvimbe husinyaa.

Kwa mazingira yetu, wagonjwa wengi huja ukiwa ni mkubwa, unaweza kuonekana. Hii ni changamoto kubwa.

Uelewa wa wenzetu (Ulaya na Marekani) ni mkubwa kuliko sisi, mara nyingi wazazi hugundua uvimbe ukiwa bado mdogo. Wanaweza kuutoa kwanza kisha wanafanya chemotherapy.

Dr. Shakilu Jumanne
Siyo kila uvimbe ni saratani na kwa bahati mbaya hatuna kinga (hasa kwa watoto), wao hazina uhusiano na maisha wanayoishi. Hatuna ushauri wa namna gani waishi, kikubwa ni muhimu kuwaleta mapema ili wachunguzwe.

Mfano, kitovu na bandama vinaweza kuvimba na isiwe saratani. Mtu wa kawaida ni ngumu kujua mambo haya, ni kuwapeleka hospitalini kwa uchunguzi.

Mzazi unapomuosha mtoto ni muhimu uwe na tabia ya kubonyeza tumbo ili ukigundua kuna uvimbe umlete haraka hospitalini.

Wazazi wengi huona uvimbe mapema lakini hupuuzia, ukiwauliza watakwambia tuliona miezi kadhaa lakini hatukujua kuwa ni tatizo.

Kwa zamani saratani ya tezi iliongoza, kwa sasa saratani ya mafigo ndiyo ipo juu. Pengine ni sababu ya kuongezeka kwa mbinu za uchunguzi.

Kila sehemu iliyopo tumboni inaweza kupata saratani.

Dr. Fat-Hiya
Uelewa wa watu bado ni mdogo, utakuta mtoto analetwa akiwa hawezi kuhema vizuri, hawezi kutembea. Elimu ya ziada inahitajika ili jamii iwahishe watoto wakiwa na ugonjwa kwenye hatua ndogo.

Kuna madhara makubwa ya kuwatibu bila kujua chanzo sahihi, ugonjwa unakuwa unaongezeka, baadhi pia hutumia dawa asili ambao hudhani hazina kemikali. Dawa hizi hazina dozi na zina kemikali nyingi zinaweza kusababisha kufeli kwa mafigo na maini.

Anna Henrh (Mtaalamu wa lishe)
Watoto wengi wanapata utapiamlo kwa kuwa huwa wanapunguza kula, huwa wanadhoofika.

Watoto wakishaugua tunawabadilishia aina ya Lishe kwa kuwa ulaji wao hubadilika

Kwa mfano, Watoto wenye Saratani ya Figo tunawapa Protini nyingi na Wanga kidogo ili waweze kuhimili Matibabu

Baadhi ya watoto wanakula vizuri lakini hawaongezeki, tunakuwa hatuoni matokeo. Huwa tunatafuta njia mbadala ya kuwasaidia, hasa kwa kutumia mpira wa chakula ambapo chakula kinakuwa kinaingia polepole.

Obadia Ngoka - Muuguzi bingwa kitengo cha Saratani kwa watoto.
Tiba ya chemotherapy husababisha maudhi (madhira) mengi. Kama wahudumu, huwa tunasaidia kuyapunguza.

Ni jukumu letu kupunguza madhila haya ili Mtoto aweze kumaliza Matibabu.

Tunatoa Elimu zaidi kwa Wazazi ili wakikutana na Watoto wenye dalili tulizozitaja amshauri kuweza kutafuata ushauri zaidi wa kitabibu na sio vinginevyo

Pia, kuna saratani ambazo Mtoto anaweza kuendelea kuishi maisha marefu

Dr. Fat-Hiya
Baadhi ya wazazi hawakubaliani na tiba za hospitalini kwa kuwa kuna imani mtaani kuwa mgonjwa hawezi kupona kwa tiba zetu, hivyo wao huanza na tiba mdabala kwanza.

Wengine hufikiria urefu wa matibabu. Baadhi ya wazazi hukataa, huamua kuwachukua watoto. Baadhi wanasikiliza, baadhi wanagoma kisha wanarudi baadae ugonjwa ukiwa mkubwa zaidi.

Dr. Shakilu Jumanne
Baadhi ya magonjwa mfano HIV huongeza nafasi ya kuugua saratani kwa watoto ndiyo maana wanawake wanapimwa wakati wa ujauzito.

Lakini kwa kiasi kikubwa saratani nyingi ni sporadic, hutokea haraka saba bila sababu.

Watoto wapewe chakula bora kuboresha lishe yao, husaidia kujenga afya.

Dr. Lulu
Tanzania inafanya tafiti za saratani kwenye ngazi mbalimbali, kwa leo tumeamua kutoa elimu ili watu wagundue mapema, waende hospitalini watibiwe.

Tafiti za kwenye jamii, pamoja na kwenye maabara zote zinafanyika Tanzania.

Kuhusu Kanda ya ziwa, sitaki kusema kuwa wingi wa watu wanaogunduliwa ndiyo uthibitisho wa kuwa sehemu hiyo ndiyo imeathirika zaidi, pengine ni kwa sababu watu wake wanachunguza zaidi.

Hatujawa na taarifa sahihi (ushahidi sahihi) kuwa watu wa kanda ya ziwa ndiyo wanapata saratani kwa kiasi kukubwa kuliko sehemu zingine.

Saratani kwa watoto zinatibika, japo kwenye jamii tumeamini kuwa ukipata saratani lazima utakufa.

Kutokupona hutokana na kuchelewa matibabu, lakini walau siku hizi watu wanajitahidi kuliko miaka ya zamani.

Dr. Shakilu Jumanne
Pamoja na uwepo wa gap kubwa la taarifa za kitafiti, kwa miaka hii mitano Tanzania kama nchi tumepiga hatua kubwa sana, hata Madaktari wameongezeka.

Kwa kanda ya ziwa, tafiti zinaendelea kubaini chanzo halisi cha uwepo wa kiwango kikubwa cha saratani.

Ocean Road, Muhimbili na maeneo mengine wanafanya tafiti, wataalamu wengine pia wanashiriki. Changamoto ni uwekezaji, lakini tunaboresha. Tutafika.

Kuhusu sumu kuvu (Aflatoxin) mara nyingi husababishwa na uhifadhi wa mazao kama karanga, mahindi, maharage n.k hufanya fangasi na unyevu viungane na kuzalisha hiyo sumu.

Kwa watoto, hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kupata saratani na sumu kuvu. Ila kwa watu wazima, mara nyingi husababisha saratani ya ini.

Christian Kidaya - Mratibu wa Elimu ya Saratani, Bugando
Elimu ni muhimu, huwa tunatoa zaidi wakati wa events mfano siku ya saratani duniani. Vipeperushi pia vipo.

Changamoto kubwa ya kufanikisha mambo haya ni bugdet.

Dr. Lulu
Kuna utaratibu wa makundi ya WhatsApp ili kufikia vituo vya chini, tunazungumza nao na kuwaelekeza, wanaleta wagonjwa.

Dr. Shakilu Jumanne
Tujenge utaratibu wa kugundua magonjwa mapema. Hutengeneza urahisi wa kutibu na kupona mapema.

Dr. Fat-Hiya
Wazazi wazipuuze wakiona uvimbe wowote, wawahishe watoto hospitalini.

Kwa wahudumu wa afya pia, wakiona uvimbe wawe wanatoa rufaa haraka ili afanyiwe vipimo mapema.

Watoto wa saratani wanahitaji sana damu, watu wajitolee kusaidia upatikanaji wa damu.

Dkt. Lulu
Hatuna ushahidi kuwa Saratani nyingi zinatoka Kanda ya Ziwa lakini unaweza kukuta kuna sehemu moja ya chanzo cha Saratani ni utaratibu mbovu wa kutunza mazao kama ya nafaka mfano karanga mbichi
 
Ni majadiliano muhimu, nime join lakini ni kaleft sababu ya mazingira niliyopo. Kama unaweza join usikilize! Ni elimu muhimu sana sana.
 
Nini chanzo cha Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa ikoje Tanzania? Kufahamu haya na mengine zaidi, ungana nasi ktk Mjadala na Wataalamu wa Watoto unaoendelea sasa kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

Fdy7NwXWIAARyOc.jpg


Dkt. Shakilu Jumanne: Saratani ya Uvimbe Tumbo kwa Watoto ni aina ya Saratani ya Watoto ambayo ina utofauti na Saratani nyingine inayotokea Tumboni (Stomach #Cancer).

Dkt. Fat-Hiya Abdallah Said: Dalili kubwa ni Tumbo kuvimba. Hapa inategemea na aina ya Saratani, linaweza kuvimba ndani ya wiki mbili na kuna wakati inaweza kuwa zaidi ya hapo Pia, mara nyingi Uvimbe huo hauna maumivu ndio maana unachelewa kubainika.

Dkt. Fat-Hiya Abdallah Said: Uvimbe wa #Saratani ukiwa mkubwa zaidi ndipo unaanza kumuumiza Mtoto na inaweza kukandamiza sehemu nyingine za mwili Mfano; Kibofu cha Mkojo, hivyo Mtoto anaaanza kukojoa Damu, kupata Homa ambazo hazisikii Dawa.

Dkt. Mohammed Sultan Salim: Uvimbe katika Tumbo ni neno pana sana, kuna vimbe nyingi Kuna Saratani katika Tezi, huo ndio Uvimbe mkubwa kabisa, unafuatia Uvimbe katika Figo pamoja na Uvimbe katika Ini.

Dkt. Fat-Hiya Abdallah Said: Saratani ni moja ya Magonjwa ambayo yanaongoza kwa vifo vingi, inakadiriwa Watoto 300,000 hadi 400,000 Duniani hufariki. Muhimbili tunakawaida ya kuwa na Watoto 800 wanaougua Saratani kwa Mwaka, inawezekana takwimu zikawa zaidi ya hapo.

Dkt. Mohammed Sultan Salim: Kabla ya kumfanyia upasuaji Mtoto lazima upime kwanza Mfano kuna Uvimbe unatokea katika Mayai kwa Watoto wa kike, ukiutoa maana yake umetoa Mayai, kuna Uvimbe ambao auhitaji upasuaji.

Dkt. Mohammed Sultan Salim: Uvimbe katika Figo huwa unasambaa katika Kifua Mgonjwa kama huyo hautakiwi kumfanyia upasuaji kwanza, ni muhimu apate Mionzi kisha ndio upasuaji, Mionzi inayoweza kufanya Uvimbe usinyae.

Dkt. Mohammed Sultan Salim: Uvimbe mwingi katika Tumbo ni wa Saratani lakini siyo kila Uvimbe ni Saratani Hivyo ni vizuri Madaktari wakatambua kuwa siyo lazima ufanye Upasuaji kwa kila Uvimbe wa Mgonjwa.

Dkt. Mohammed Sultan Salim: Kwa kuwa Uvimbe mwingi hauna maumivu hatua za mwanzoni, na kwa kuwa Mtoto anakuwa hana uelewa, ni ngumu kujua mapema tatizo hilo Wengi wanakuja Hospitali wakati tayari hali imeshakuwa mbaya.

Dkt. Shakilu Jumanne: Saratani haitokani na Mazingira ya Mtoto, ni muhimu Mzazi kuwa makini na kujitahidi kumwezesha Mtoto kupata matibabu mapema anapoona dalili Mfano Bandama inaweza kuvimba lakini isiwe Saratani japokuwa zipo Bandama ambazo zinavimba kutokana na Saratani.

Dkt. Shakilu Jumanne: Mzazi anapokuwa anamuogesha Mtoto awe na kawaida ya kumkagua, Mfano kumminya sehemu ya Tumboni au pembeni ya Tumbo, ukibaini kuna uvimbe mfikishe Hospitali mapema Kuna kesi nyingi zinatokea Wazazi wanakuja, ukiwauliza wanasema waliona ni uvimbe wa kawaida.

Dkt. Shakilu Jumanne: Kila kiungo ndani ya Tumbo kinaweza kupata Saratani, kama jamii ni muhimu kujenga tabia ya kutafuta Huduma ya #Afya mapema Ni vizuri Mtu ambaye siyo Mtaalamu wa Afya kugundua tatizo hilo kwa Mtoto mapema lakini tunashauri ukiona dalili uwahi Matibabu

Anna Henry: Tunapata visa vingi vya Saratani kwa Watoto na ni changamoto maana wengi wanakuja Hospitali wakiwa tayari wamepata Utapiamlo Hii ni kwasababu Mtoto anakuwa hana hamu ya kula kutokana na maumivu anayoyapata Tumboni.

Anna Henry: Watoto wakishaugua tunawabadilishia aina ya Lishe kwa kuwa ulaji wao hubadilika Kwa mfano, Watoto wenye Saratani ya Figo tunawapa Protini nyingi na Wanga kidogo ili waweze kuhimili Matibabu.

Dkt. FAT-HIYA: Wazazi wa Watoto wenye Saratani wawapeleke Hospitali kwa ajili ya Matibabu zaidi Watu wamezoea kupokea ushauri kutoka kwa Watu wasio Wataalamu na huishia kutumia Mitishamba au kununua tuu Dawa Hii husababisha Watoto kuzidiwa matibabu yanakuwa changamoto.

Muuguzi Obadia Ngoka: Matibabu ya Saratani yanahusisha #Chemotherapy, na madhila huweza kujitokeza wakati wa Matibabu Kama kupungukiwa Kinga ya Mwili na Damu Ni jukumu letu kupunguza madhila haya ili Mtoto aweze kumaliza Matibabu.

Muuguzi Obadia Ngoka: Tunatoa Elimu zaidi kwa Wazazi ili wakikutana na Watoto wenye dalili tulizozitaja amshauri kuweza kutafuata ushauri zaidi wa kitabibu na sio vinginevyo Pia, kuna #Saratani ambazo Mtoto anaweza kuendelea kuishi maisha marefu.

DKT: FAT-HIYA: Kuna baadhi ya Wazazi hawana imani na matibabu ya Hospitali, kutokana na Imani kuwa Saratani haitibiki Tunajitahidi kuongea na Wazazi ili wasiachane na Matibabu kwa kuwa mengi huchukua muda mrefu Baadhi huelewa na kuwaleta Watoto inavyotakiwa.

DKT: SHAKILU: Ni kweli kwamba Watoto wengi hupata Saratani kwa sababu ambazo nyingi hazijulikani Lakini sababu kuu ni mgawanyiko ya mabadiliko ya Vinasaba, kutokana na kipindi ambacho Mwili hujijenga kuanzia Tumboni.

DKT: SHAKILU: Asilimia ndogo sana ya Saratani hutokana na sababu za kurithi Pia, Watoto wenye VVU wanahatari kubwa ya Kupata aina fulani za Saratani, Wazazi wenye Maambukizi hupatiwa Matibabu maalum ili kuwakinga Watoto.

DKT. LULU: Tafiti za Saratani Nchini zinafanyika katika ngazi ya Kijamii na Pia kimaabara Kuna sehemu zenye aina nyingi za Saratani. Mfano katika Jamii zinazooana Ndugu kwa Ndugu, lakini hatuna ushahidi kuwa Saratani nyingi zinatoka Kanda ya Ziwa.

DKT. LULU: Saratani inatibika. Jamii inaaamini Saratani haitibiki kwa sababu asilimia kubwa ya Wagonjwa hufariki. Hii ni kwa sababu wagonjwa huanza matibabu kwa kuchelewa hivyo nafasi ya kupona inakuwa ndogo.

DKT. LULU: Saratani ya Watoto pia inatibika Wazazi wawafikishe Watoto hospitali mapema Matibabu yakianza mapema uwezekano wa kupona ni wa juu na Watoto wataendelea kukua vizuri.

Dkt. Lulu: Hatuna ushahidi kuwa Saratani nyingi zinatoka Kanda ya Ziwa lakini unaweza kukuta kuna sehemu moja ya chanzo cha Saratani ni utaratibu mbovu wa kutunza mazao kama ya nafaka mfano karanga mbichi
 
Back
Top Bottom