Moto sio Mangi!
Nikikumbuka around 2003, Mkapa ndo amefanikiwa kuleta ARV batch ya kwanza, enzi hizo ARV kwa madoni tuu, wa wenye connection. Wakati Mkapa anazindua hiyo programu hapo Mwananyamala, alilia sana Ben. Waya ukimtesa sana Hayati Mkapa akiwa kama raisi wa hii nchi. Watu walipukutika sio poa. Mtu anazikwa kama kiroba, bora wakristo majeneza yalikuwa yanasitiri maiti. Waislamu wakiwa wanazika mtu kwenye sanda anakuwa kama fimbo, mnaona kichwa tuu.
Hatari Mangi, tumetoka mbali na huu ugonjwa.
Enzi hizo watu wanatoka mikoani kufuata ARV hapa mjini. Maskini unakufa kilo mbili, dawa hamna.