Saninu Laizer wa madini lipa pesa za watu. Ulituonyesha una madini ya mabilioni leo hii mchina anataka bilioni 8 zake

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,151
Lazier lipa bana atujazoea kuringishana huku tunadhulumu watu

ARUSHA: Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite katika Mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Saninu Laizer maarufu kwa jina la Bilionea wa Tanzanite amemwangukia Mwekezaji raia wa China, Jun Fang akiomba wakae mezani kutafuta suluhisho ya mgongano wa kimaslahi kati yao.

Bilionea Laizer ameyasema hayo Jijini Arusha baada Fang kutaka kutaka kuomba msaada wa Balozi wa China nchini ili apate haki yake ya fedha na mali vyenye thamani ya Sh bilioni 8.5 ambazo (Laizer) anadaiwa kuonesha dalili za kutaka kumdhurumu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha Laizer alikiri kuingia ubia na mwekezaji Fang toka mwaka 2011 hadi mwaka 2021 kwa mwekezaji huyo kumiliki hisa asilimia 70 na yeye kama mzawa kumiliki hisa asilimia 30 kwa makubaliano kuwa Fang kuleta vifaa vyote vya kisasa vya uchimbaji,mtaji na kulipa gharama zote za uendeshaji ikiwemo mishahara ya wafanyakazi na alifanya hivyo.

Alisema baada ya mkataba kumalizika mwaka 2021 alimtaka mwekezaji Fang kuingia makubaliano (MOU) ya awali ambayo hakuyataja lakini raia huyo wa China aligoma kusaini makubaliano hayo.

‘’Mimi niko tayari kufanya kazi na Mchina wakati wowote na aje mezani tutatue changamoto zilizopo na tufanye kazi ya uchimbaji madini ya Tanzanite katika kitalu D kama zamani’’alisema Laizer.

Picha na John Mhala
Una maoni usisite kutuandikia
-
#MwangwiwaUkarimu
#echoesofkindness
#HabarileoUPDATES

1706102120915.jpg
 
ile ilikuwa ni mambo ya kisiasa tu, jamaa mgodi ulikuwa unaendeshwa na huyo mchina na washirika wengine, yale mawe waligawana na huyu mchina na washirika wengine
Aiseee hii dunia kuna watu ukiwaona mbingun unaudited huyu na mtanguliziwakembelezahaki siokwa kutuhadaa vile ka
 
Kwa hio machina kagoma kuingia mkataba na vifaa vyake kapepea navyo kwa hio nini kinafuata tukafukie mashimo?
Mchina kataka helayake kwanza...
Jamaahataki anataka wasaini kwanza mkataba then amlipe

Mchina ngaashtukaaaa kagomaaa no mny no saini fukiashimoooo jamaa kadata issue imefika ubalozin ndio hana hamu
 
Back
Top Bottom