Vigogo wa Kampuni tatu za Madini ya Tanzanite Mererani matatani kwa kuvamia mgodi wa serikali

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Sakata la uvamizi haramu wa Mgodi wa Kitalu C wa Madini ya Tanzanite uliopo Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, unaomilikiwa na serikali namwekezaji mzawa kampuni ya madini ya Franone sasa imekuwa shamba la bibi baada ya wafanyabiashara wengine watatu wakubwa kuingia katika mgodi huo na kuchimba madini chini kwa chini kinyume cha sheria.

Kampuni tatu zinazodaiwa kuingia Kitalu C na kuchimba kwa njia haramu maarufu kwa njia ya Bomu ni pamoja na kampuni ya Tanzanite Explore inayomilikiwa na Victor Philipo Mkenga na Kampuni ya Saniniu Mining inayomilikiwa na Bilionea Saniniu Laizer na Kampuni Manga Gems(T) ltd inayomilikiwa na familia ya marehemu Mathias Manga.

Akithibitisha tukio hilo Afisa Mfawidhi wa Madini Mirerani RMO ,Mernad Msengi alisema ni kweli ofisi yake ina taarifa za tukio hilo na hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kusimamishwa uchimbaji kwa wafanyabiashara hao waliovamia Kitalu C na pili kuwapa nafasi ya mazungumzo kati yao na Kampuni ya Franone kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

,,Ni kweli tukio hilo lipo na ofisi yangu imeshachukua hatua ikiwemo kusimamisha uchimbaji kwa kampuni zinazomilikiwa na wafanyabiashara hao kusimama na tumewapa nafasi ya mazungumzo kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa.

Alipoulizwa kwa njia ya simu mwekezaji wa kapuni ya Franone Onesmo Mbise alikiri kuwepo kwa kampuni zinazozunguka mgodi wa kitalu c kuvamia na kufanya uchimbaji haramu wa bomu, kinyume cha sheria.

Awali tukio lingine kama hilo liliwahi kutokea march 10 hadi 13 mwaka huu kwa kampuni ya Gem Rock Venture inayomilikiwa na mfanyabiashara Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti kuchimba kwa njia haramu katika kitalu C na kufanya serikali kukosa mapato hivyo hatua zaidi zinahitajika juu ya kuthibiti uchimbaji huo haramu kwa wafanyabiashara wakubwa.

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mapema mwaka jana katika hotuba zake aliwahi kuwaonya wafanyabiashara wa Tanzanite kuacha mara moja kuvamia mgodi wa Kitalu C na kuchimba kwa njia ya Bomu na kusisitiza kuwa atayekaidi amri hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Habari kutoka katika Mji wa Mirerani zinadai kuwa wafanyabiashara hao walivamia mgodi wa Kitalu C mwanzoni mwa mwezi huu na waliingia zaidi ya mita 600 katika kitalu hicho na kuchimba kwa njia haramu.

Vyanzo vilidai kuwa Saitoti alipochimba kwa njia haramu katika mgodi wa Kitalu C serikali ilimchukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kumfungia mgodi wake na pia alifikishwa Mahakamani kujibu mshitaka lakini kwa wafanyabiashara hao imekuwa tofauti hivyo kuonyesha wazi kuwa wafanyabiashara hao wanalindwa na baadhi ya vigogo wa serikali kama wanavyotamba wao.

Mkurugenzi wa Manga Gems,Brayan Manga alipoulizwa juu ya tukio hilo alijibu kwa dharau na kusema kuwa hana taarifa za kuvamia kitalu C na kusema kuwa hakuna Mtaalamu aliyethibitisha kuwa yeye amevamia mgodi huo.

Mfanyabiashara Victor Mkenga na Bilionea Saniniu Laizer hawakuweza kupatikana kuelezea tuhuma hizo kwa kuwa simu zao za kiganjani zilikuwa zikiita bila ya kupokelewa pamoja na kutumiwa ujumbe wa sms mara zote bila ya mafanikio lakini juhudi zaidi zinaendelea kuwasaka.

Ends...
 
KAtika hotuba zake za awali kabisa, Samia alitoa maelekezo kuwa KITALU C kisiguswe. Nilidhani ni code language kumbe ni uwekezaji wa serikali upo pale.

Sasa RMO anazungumza nini na wavamizi badala ya kusimamia sheria?

Tukisema serikalini kumejaa watendajj wa hovyo sana, mifano yake ndo hawa wanaopetti petti wahalifu
 
Kwa sas kama una kisu kikali, unauhakika wa kula nyama yeyote uipendayo hata kama ipo chini ya Ikulu.
 
Kwa mini wawazuie wazawa kufaidi maliasili zao? Wanawazuia ili wawape waarabu wawe wanajichotea tu maliasili zetu.
 
Back
Top Bottom