Kuna kitu wengi hawajaelewa kwa neno mchimbaji mdogo wa Madini (Laizer)

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,170
3,775
Kila mtu hutamani angekuwa na bahati kama aloipata Laizer tena ya kuwa Billionea kwa TSH au Milionea wa USD.

Wengine wamefikiria labda Bwana Laizer aliamka asubuhi maskini halafu akalalia U bilionea usiku,(hii sivyo).

Navyomfaham Laizer ni mchimbaji wa madini wa muda mrefu sana ila kwa zaidi ya miaka 10 hausiki katika ufanyakazi(Yaani sio MWANA APOLO AU MZAMAJI) isipokuwa ni msimamizi au uhudumiaji .

Akiwa ni mkazi wa kijiji cha wamasai kiitwacho NAISINYAI(Karibu pia na MERERANI) umbali kama 10km kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA .

Ni mjasiriamali wa muda mrefu kwa madini (Broker na mchimbaji(muhudumiaji mgodi wengine wanasema anaye mdhamini ndo mana mgodi wake unajina maarufu kwa mchina)) pia ana milika Mall moja Arusha na Hoteli Mererani(Manyara inn) .

Hivyo huyu siyo mtu wakudhania alichokipata hataweza kukitumia kwa usahihi au hata totozi(bata) kwa wingi.

Neno Mchimbaji mdogo lisikufikiriashe kuwa anatumia dhana duni kwenye kuchimba au kwa kuone ile picha yake alovaa lubega ukadhani alikuwa kapuku(Mavazi ya kimasai yapo ya gharama kuliko suti )

Bwana Laizer alipofanikiwa alisaidia ndugu zake wote pia ni mtu wa watu sana tena sana. Kasaidia watu wengi wa kijiji chao na Mirerani. Hii sio kwake tuu ila kwa matajiri wa Mirerani hilo ni suala la kawaida Yaani Mirerani Wapo watu wanaishi kwa maisha ya mwingine(Marehemu Bilionea Msuya alikuwa na mapungufu yake ila wengi walikuwa wakiishi kupitia mkono wake) .

Bwana Laizer yawezekana alikuwa bilionea wa TSH kabla ya kupata umarufu karibuni kwani kuhudumia mgodi sio kazi nyepesi, kuanzia vifaa,maji,chakula cha wafanyakazi,umeme,mafuta ya Generata,oil,Mitambo,wasomi(Waongoza miamba,mitambo n.k) ambayo kwa siku sio chini ya milioni 2 inaeza potea.

Tangu mgodi huu ulompa madini hayo aanze kuuhudumia si chini ya miaka mi 4 naufahamu na kuusikia. Pia uongo watu wanaozusha kuwa hakuwahi pata dini lolote si sawa, sema hakuwahi pata labda lenye ukubwa kama huo.

Usije ukaacha kazi yako ukawaza kwenda kuhudumia mgodi ili uwe bilionea kama Laizer (NISEME TUU ni mwezi mmoja utajikuta umekauka huna hata mia) . Inawezekana ila kama una uwezo wa kutosha wa kifedha tena fadha yenye kuzunguka ila kama ni akiba kama ya Bilioni mbili utajikuta umeimaliza na hata hujapata kitu.

Kwa Madini ya Tanzanite one wapo walowahi shika hela zaidi ya hizo sema hayakuwa na promo kama hii..

HELA HUTENGENEZWA NA HELA.
 
Sheria ngowi anashona suti nadhani bei zake zinaweza kufika hadi million 2. Be serious tafadhali. Ebu tupatie hizi taarifa vizuri sisi akina Tomaso
mleta mada hajazungumzia suti zote yani hajasema kuwa hayo mavazi yanapita bei suti zote, yeye anazungumzia suti hizi za laki 2 au laki 3 , kuhusu designer suits mfano hizo za sheria ngowi upo sahihi
 
Sheria ngowi anashona suti nadhani bei zake zinaweza kufika hadi million 2. Be serious tafadhali. Ebu tupatie hizi taarifa vizuri sisi akina Tomaso
Nimesema yapo(Sio lazima) pia bei ya suti kufika hadi milioni mbili sio kwamba ni suti zote(zipo suti laki na nusu ) Kuna Lubega inafika kuanzia laki na nusu had laki 3 na hapo kavaa tatu au nne mana kuna namna ya kuvaa sio kufunika kama shuka
 
Nimesema yapo(Sio lazima) pia bei ya suti kufika hadi milioni mbili sio kwamba ni suti zote(zipo suti laki na nusu ) Kuna Lubega inafika kuanzia laki na nusu had laki 3 na hapo kavaa tatu au nne mana kuna namna ya kuvaa sio kufunika kama shuka

Huyu mtani wangu wa kuibiana ng'ombe namshauri aitume hela yake kama ifuatavyo, kama hana mpango wa kuongeza Mall nyingine

Aongeze billion zingine 2.6 halafu anikopeshe mimi nitazirudisha baada ya miaka mitano.

Vinginevyo anunue Treasury Bonds (Hati Fungani) kutoka BOT, Serikali waendelee kumtunzia hela yake huku ikiwa inazaa faida kubwa.

Angalia hapa:

Tuseme labda akiamua kuziwekeza kwa namna hiyo, kwa asiliamia 10 (10%). Faida atakayopata kwa mwaka ni kama ifuatavyo;

7.4bnx0.1=0.74bn=740,000,000/=
Less: 10% tax 74,000,000/=

NET PAY/ PROFIT =666,000,000/=

Akifanya hivyo, atapata faida ya million 666 kwa mwaka, sawa na wastani wa million 55.5 kwa mwezi, au million 1.85 kwa siku! What an investment!
 
Back
Top Bottom