Samwel Sitta: Tanzania iko tayari kupambana na aina yoyote ya uchokozi kutoka Malawi!

Malawi wanataka Lake Nyasa ambalo wao wanaliita Lake Malawi liwe lao lote,, wanasema Watanzania wana maziwa mengi sana pamoja na bahari ya Hindi so its better tuwaachie Lake Nyasa/Malawi liwe lao 100%.. So they started exploration ya mafuta na gas mpaka wanakaribia kuingia Mbinga sasa..

bora tu tuwaachie, kwanza hatulitumii sana, hata ziwa tanganyika wakitaka wachukue tu, hatupendi vita sisi na rais wetu ni mpole
 
Malawi wanataka Lake Nyasa ambalo wao wanaliita Lake Malawi liwe lao lote,, wanasema Watanzania wana maziwa mengi sana pamoja na bahari ya Hindi so its better tuwaachie Lake Nyasa/Malawi liwe lao 100%.. So they started exploration ya mafuta na gas mpaka wanakaribia kuingia Mbinga sasa..

Serikali ya dhaifu ipo tu....hawajamaa chokochoko wameanza kitambo sana kuhusu ziwa nyasa si tuwatandike tu...
 
Wanajeshi wetu wana vitambi vikubwa sana kweli wataweza milima ya malawi? Enzi za mwalimu tulikuwa tunaogopwa na kila taifa na hata akina nduli iddi amini dada walikuwa wanajaribu tu nguvu zetu na hawakufurukuta
 
Tusimlaumu mtoa thread, ni mtazamo wake. Wapo wanaokubaliana kuwa katoa taarifa kwa umma kuwa serikali inajua kinachoendelea kwenye mpaka wetu na Malawi. Serikali ingekaa kimya wakati habari za mzozo zimeenea nchini
 
mm nataka wachukuwe mpaka juu sio ziwa tu watanganyika mmezoeya kuwadhulumu zanzibar sasa unganeni na malawi basi kama mnapenda muunganona mara hii mtapigana peke yenu sisi hatuji chezea mungu nyinyi
 
Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .

Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.

Pole sana. unaonyesha usivyo komaa kisiasa na kurukia kuleta mada ya kushtua watu. Hajatangaza vita
 
mm nataka wachukuwe mpaka juu sio ziwa tu watanganyika mmezoeya kuwadhulumu zanzibar sasa unganeni na malawi basi kama mnapenda muunganona mara hii mtapigana peke yenu sisi hatuji chezea mungu nyinyi

hata kupigana kwenyewe mnajua zaidi ya kujitoa mhanga.!
 
Inasemekana ziwa lile huwa lina hama kutoka sehemu moja na kuamia sehemu nyingine hivyo kuna kipindi sehemu kubwa huwa iko tanzania na kuna wakati sehemu kubwa huwa Malawi sasa naona wanataka kutumia nafasi hivyo kujitwalia...tutawabutua
 
huyu mzee anaropoka sana ..sijui anakuwa amelewa ndo anaingia bungeni? hana maamlaka at all ya kuongea na kutoa kauli hizo...anyway ni kwa kuwa nchi yenyewe iko valuvalu watu wanawaza futari tu therefore hakuna mtu wa kudhibiti haya
 
Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .

Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.
Sidhani kama tamko lina-amount kutangaza vita na ninashukuru kuwa hatimaye kuna mtu ametoa kauli yenye uzito wa kiserikali. Kuendelea kukaa kimya kwa jambo hili, au kumtumia mwanadiplomasia Membe kunaendelea kuwavimbisha kichwa Malawi. lazima wajue kuwa wanakabiliana na Tanzania
 
Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .

Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.

Kwani Tanzania ina Amri Jeshi MKuu? Huyo Amri Jeshi Mkuu kashindwa hata kumuua Dk Ulimboka ataweza kuipiga Malawi? Angalia hata migomo ya walimu na maandamano ya watoto wa darasa la kwanza kashindwa kuitatua ataweza vita?

Nchi ipo Autopilot (Johnson Mbwambo, 2008)

TUMBIRI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .

Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.

miafrika ndivyo tulivyo sosi NN
 
Atleast kavunja ukimya! kwani hizi habari tumekua tukizijadiri sisi wabunge wa jamii na serikali ilikua bado ipo kimya..Tulitegemea AMIRI JESHI MKUU jana agusie japo kwa nukta tu kua mipaka ya nchi yetu sio SALAMA lakini kimya mie nadhani tumpe hongera mh SITA kwa ujasiri wake kwani BETTER LATE THAN NEVER kama hawa MALAWI wakishapata hayo mafuta na ukizingatia makampuni ya uchimbaji ni ya UINGEREZA kwao maslahi kwanza na itakua ngumu eti hiyo km hiyo iamuliwe na UN, obvious UK ita side upande wa MALAWI kwani wana interest..Nini serikali inapaswa kufanya ni kuieleza MALAWI kua uchokozi km huo haukubaliki wa kusema ziwa lote ni lao, pia ni kuwaonya very strongly hao raia wa UK wenye makampuni kua NEVER CROSS TO OUR TERRITORIAL WATER na wakikiuka wakamatwe na washitakiwe kwa sheria za TZ that will sound better to them all kwani ata hao UK wanajua kua dispute area btn MALAWI -TANZANIA ni ktk ziwa sasa kwanini wafanye uchimbaji wa mafuta?

Mkuu kumbe wewe ni mbunge!? Kwanini usiwe verified user hapa jf?
 
ukisema kuwa "Tanzania ipo vitani na Malawi" hilo ndilo tangazo la vita ila ukisema tupo tayari hiyo ni kauli ya kuwapa moyo wananchi wasiogope,anayetangaza vita ni amiri jeshi mkuu, katiba inasema hivi

44.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali
ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.
(2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya
tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya
kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani
ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha
mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria
kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita
lililotolewa na Rais.
 
Nimejikuta sina la kuchangia zaidi ya kucheka tu, thread nyingine ni burudani tosha kabisa.
 
Heri Sitta ametoa tamko,sielewi jana kwanini mkuu wa nchi hakugusia hizi chokochoko. Wamalawi wamejaa Dar es Salaam,wengi ni wafanyakazi wa ndani wa watawala wetu! Wanatufahamu sana kwamba siku hizi ni kama joka la Kibisa!
 
kwani huko mipakani kuna nini kimetokea mpaka jamaa aseme hivyo?

Mpaka wa Tanzania na Malawi, una historia ndefu. Tangu miaka ya mwanzo ya uhuru, aliyekuwa raisi wa Malawi, alidai mpaka wa Tanzania na Malawi ni pale ziwa Nyasa linapoishia. Hivyo, Tanganyika, haimiliki hata tone moja la maji ndani ya ziwa Nyasa. Haya ndiyo mafundisho kwa wanafunzi wote ndani ya nchi ya malawi. Upande wa pili, Tanganyika wanadai Mpaka wake upo katikati ya ziwa nyasa. Hivyo, ugomvi huu upo tangu miaka ya mwanzo ya uhuru.
 
Mkuu kumbe wewe ni mbunge!? Kwanini usiwe verified user hapa jf?

Mibunge ya CCM haipendi kuwa Verified kwa sababu watahojiwa na NEC na Kamati Kuu yao. Ni Mwigulu LM Nchemba na Hamis Kigwangala waliothubutu kuwa verified humu. Hata hivyo huwezi kuwaona wanachangia kwa ID zao halisi kwenye mijadala mizito inayoangamiza chama chao. Utawaona kwenye thread za Propaganda dhidi ya CDM hususan thread za Rejao, zomba na the like.

TUMBURI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Back
Top Bottom