Samwel Sitta: Magufuli anashauriwa vibaya!

Samwel Sitta: Magufuli anashauriwa vibaya!

Aende akaandike vitabu vya riwaya ya mapenzi
 
Na anyamaze kamwe huyo Mzee. Tulikuwa tunamheshimu lakini heshima yake aliitosa kwenye BMK. Amwache JPM atumbue majipu. Tuko nyuma yako Rais wetu.
 
Six anahofia nyeti zake kuonekana kutokana na huu upepo unaoivumia hiyo wizara ya uchukuzi.Avumilie tu kama anavyovumilia JK.
 
Kwani kuna mahali pasafi nchi hii ambapo ambapo pakiguswa na rais Magufuli utasema anashauriwa vibaya. Kila mahali panahitaji kusafishwa kwa haraka.
 
Ile dhambi ya kuchakachua katiba ya wananchi imtafune Sitta milele.
 
Sita roho inamuuma kimya kimya, katiba mpya ndio iliyommaliza

Sitta amwache Magufuli afanye kazi yake.Asifikiri huu ni utawala wa Mkwere alyekuwa Rais wa matanuzi na wizi wa mali ya summa.

Rais mstaafu Mwinyi aliwahi kusema kila kitabu na zama zake.Zama za kina Kikwete na kina Sitta zimekwisha.
 
Hivi huyu mzee kwa nini asinyamaze tu, anazidi kujiaibisha tu, watanzania hawataki kumsikia
 
Ule uchunguzi alioagiza magufuli juu ya mikataba ya wizara ya uchukuzi na wajenzi wa reli ndio tatizo maana utafuta nafasi ya mzee Sitta, hence hapati hata senti tano. Ndio kelele zote hizi
 
Pasco umeongea vema..maana hapa janvini kuna watu wameanza kupiga debe magu akae miaka 20 anyooshe nchi..

Hiii nchi ya ovyoo sana na wananchi wake hawajielewi hawajui madhara ya udikteta kaka lkn watajuta na watamchukia jamaa soon
 
Last edited by a moderator:
Magufuli yuko makini kwa anayofanya, sita atueleze ile hela iliyobaki kwenye bunge maalum la katiba wakati ukawa walivyotoka nje aligawana na nani?
 
Mbona Wanyarwanda wameendelea kumuamini Kagame tena kwa Wingi.
Magu akitutoa tulipo akae milele.

Kuna kitu kinaitwa manipulation ndugu, viongozi wa kiafrika wanauwezo wa kumanipulate chaguzi mbalimbali, in short mwenye haki ktk chaguzi za kiafrika sio mpiga kura bali mhesabu na mtangaza mshindi! Kwahiyo suala la sijui Kagame anapendwa na wanyarwanda hiyo ni subjectivity!
 
Huu utawala utawaacha kando wenye akili wengi na kuchukua mashabiki....

CC: Nicholas
 
Last edited by a moderator:
Akwende zake pumbafu huyu amwache raisi afanye yake hili zee nafiki kweli kweli

..siyo vizuri kumtukana na kumbeza mzee sita , yeye katoa maoni yake, yasipuuzwe hata kama hukubaliani nayo. Wewe kuwita pumbafu ni maoni yako tu, siyo lazima tukubaliane na wewe. Nachukia sana wana JF kutukana humu, tutoe hoja na si matusi. Anayetukana hana hoja na uelewa wake ni mdogo ?wewe tuambie nini kosa au ubaya wa mzee sita..
 
Kuna kitu watu hawakijui kumhusu Magufuli, hoja ya kuwa anashauriwa vibaya sii hoja, kwasababu Magufuli ninayemfahamu mimi, hashauriki, na hana hata chembe ya busara!, Magufuli ni mtu wa maamuzi magumu kwa haraka, pupa na papara!.

Wengine hili tuliliona na tukalisema mapema tuu!, tena huu ni mwanzo!, nawaambieni subirieni tuu, na ikitokea akanogewa na urais, kile kipengele cha two 5 yeas terms kitaondoka and no one can stop himi!, mtaniambia!.
[h=3]If you can't beat them, join them! He is the worst dictator.[/h][h=3]Kwa Kasi Hii ya Magufuli na "Hapa Kazi Tuu", Hivi Kweli Kuna [/h] Merry X-mass & Prosperous NY!.

Pasco

Huyu huyu ndo tunamtaka! Tumeona utendaji wake akiwa waziri, tumeina utendaji wake muda huu mfupi baada ya kuwa rais, nchi inanyooka, kodi zinalipwa, wahujumu uchumi roho juu, nidhamu ya kazi imerudi! HUYU HUYUUUUUU!
 
Issue ya tija kuzungumzia hapa ni utaratibu mzima wa mchakato wa tenda ya miradi ya trilions bgmoyo na SGR. Sita anasema ilisimamiwa na Ikulu! Serukamba anasema walipinga kwa niaba ya bunge. Ni nchi gani duniani ikulu inaingia mikataba ya aina hii pasipo kuhusisha bunge? Wapi uwazi? Kenya mradi SGR serikali imehenyeshwa na wabunge kila kipengere. Bila katiba mpya kusimamia mambo haya nchi itaendelea kuendeshwa kwa vificho na watu wachache kwa maslahi yao.
 
Mbona Wanyarwanda wameendelea kumuamini Kagame tena kwa Wingi.
Magu akitutoa tulipo akae milele.

Sisi Waafrika tuna matatizo, sijui nani atatuokoa. Kagame ni kiongozi mzuri lakini kuamini kuwa Rwanda yote hakuna mwingine kama au bora zaidi yake ni shida kubwa.
 
Kuna kitu kinaitwa manipulation ndugu, viongozi wa kiafrika wanauwezo wa kumanipulate chaguzi mbalimbali, in short mwenye haki ktk chaguzi za kiafrika sio mpiga kura bali mhesabu na mtangaza mshindi! Kwahiyo suala la sijui Kagame anapendwa na wanyarwanda hiyo ni subjectivity!

Matatizo yetu yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja. Hakuna anayekubali matokeo ya uchaguzi yanayotofautiana na kile anachotaka yeye. Ni shidah. Wapo waliompigia kura EL wanaoamini kuwa kwa kuwa wao walimpigia kura ni lazima angeshinda tu; kutoshinda kwake ni sababu kaibiwa kura!!!
 
Back
Top Bottom