Samuel Eto’o afungiwa mechi nne, atozwa faini ya Tsh. 49.6 Milioni na CAF kwa utovu wa nidhamu AFCON 2025

Samuel Eto’o afungiwa mechi nne, atozwa faini ya Tsh. 49.6 Milioni na CAF kwa utovu wa nidhamu AFCON 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto’o, amefungiwa kuhudhuria uwanjani kwa mechi nne na kutozwa faini ya dola 20,000 za Marekani (Sh49.6 milioni), akidaiwa kufanya utovu wa nidhamu wakati wa mechi ya robo fainali ambayo Cameroon ilipoteza dhidi ya Morocco kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

1768459829548.png
FECAFOOT imethibitisha kupokea uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF). Hata hivyo, shirikisho hilo limehoji uamuzi huo, likieleza kuwa adhabu hiyo imetolewa bila maelezo ya wazi au sababu za kuridhisha.

Hatua hiyo imeibua mjadala mkubwa ndani na nje ya Cameroon, huku wengi wakisubiri kuona iwapo FECAFOOT au Samuel Eto’o watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa CAF.

==

Cameroonian Football Federation president Samuel Eto’o has been suspended for four games for alleged misbehaviour during his team’s loss to Morocco at the Africa Cup of Nations.

The federation, known as FECAFOOT, said Wednesday that it had taken note of the decision from the disciplinary committee of the Confederation of African Football to suspend its president along with a $20,000 fine, but that it “lacks any explicit justification”.

“FECAFOOT further notes that the expedited procedure leading to this decision raises serious concerns regarding the fundamental requirements of a fair trial,” the federation said.

CAF said Monday it was investigating match incidents during the quarterfinals between Cameroon and Morocco, and Algeria and Nigeria.

CAF did not refer to any specific incidents at the Morocco-Cameroon match, but the only widely known outlier was the behaviour of Eto’o, who was seen gesturing angrily during the game towards Moroccan counterpart Fouzi Lekjaa, with CAF president Patrice Motsepe also sitting nearby.

“FECAFOOT reaffirms its unwavering support for its president and its commitment to upholding the principles governing credible disciplinary justice,” the federation said.

Source: www.aljazeera.com
 
Etoo anaona bila yeye hakuna Cameroon 😁timu anakuwa mkorofi muda wote
 
Huyu nae angetulia tu kama wakina aboutrika na drogba, ila sawa tu wakafungie tu.

Morocco tunaenda kubeba ndoo yetu, hatuna mpinzani afrika hapa 😄 na brazil atatukoma tu.
 
Ndio muamini sasa moroko wametoa rushwa kwa marefa
Hata sisi tuliminywa
 
Morocco wamfunge Senegal mzee daah mpira unadunda ila sio kihivyo wale jamaa mpira wanajua sana..

Wanajua sawa, ila kila timu ina mbabe wake, senegal anawaonea zaidi wanaopaki basi, wasiokaba ngoja akutane na best team in afrika
 
Huyu nae alipoanza kuzinguana na kocha, kila mtu kutaka timu yake icheze nikamuona n fala, Safi sana CAF
 
AANAKOMAAKAMA.WAKINA MU7 MWACHE AFIE MADARAKAN

MU7 AKITOBOOA HII MIAKA ILI8BAKIA NIKOPALE
 
Msiojua na kufatilia mpira bado mnamlaumu Eto Fills kwa yaliyotokea Morocco.
 
Back
Top Bottom