Samsungs wanashida gani?

Ipo hivi, kwanza kabisa Hii fact ni maalum tuu kwa flagship(high end) Maana ukiliweka hili katika ujumla wake, hamna anayemkuta Samsung kwa technology ya ku compress battery kubwa mpaka sasa kwa hizi kampuni kubwa zote unazozisikia, hapa nazungumzia Iphone, Oppo, infinix, nokia, tecno, Xiaomi, n.k

Samsung M51 na F62, wote hawa wana 7000mAh(# doesn't lie endurance rating za gsmarena zinaongea, hivyo hawadanganyi), ni mara mbili ya hio uliyotaja, kwenye hizi kampuni kubwa hakuna aliyefikia hapo, wengi wamegota kwenye 6000mAh.

Kwahio unakuja kugundua sio kwamba hawawezi, ila kuna sababu.

1. Sifa ya flagship ili ipendwe inaanzia kwenye muonekano, na huwezi zungumzia muonekano huu bila ku consider unene wa simu, battery kubwa inahitaji space kubwa, na kwa sababu ukubwa wa simu kwa juu(urefu×upana) ni limited kwa size ya kioo unachotaka kutumia, basi sehemu itakayo kua affected ni Unene, matokeo yake ni simu kubwa ambayo ni ngumu ku i manage mkononi.
NOTE : Moja ya sifa ya flagship ni display kubwa, sasa imagine simu kama Note 20 ultra yenye kioo cha inch 7 kasoro nukta halafu iwe nene, utaishikaje?

2. Uzito, ieleweke battery ni hardware, hivyo size inavyokua kubwa uzito unaongezeka, Sasahivi kampuni nyingi za simu zinashindana katika kuhakikisha wanatengeneza simu nyepesi isimkere mtumiaji hata akiweka mfukoni, na tukumbeke ushindani huo ni wa kwenye hizi high end sababu ndio zinaipa kampuni sifa na kutambulisha technologia yao mpya.
Flagship zinatengenezwa na material/hardware bora/imara mfano tempered glass, Aluminium flame n.k, hivi vyote vinaongeza uzito kwenye simu, while low end wanatumia ma plasti kote,
Hivyo basi kuachana tuu na battery simu inakua nzito tayari, sasa ukibugi kwenye battery unashangaa unatengeneza simu ya nusu kilo na ushee, sitanii (ulefone power Armor 13, ina nusu kilo), sasa hii uite flagship? Angalia Samsung S21 ultra mwenye 5000mAh pamoja na battery ndogo kulinganisha na M51 lakini material yake mazito yameifanya imzidi Uzito M51 yenye 7000mAh iliyotengenezwa kwa plastic, haya angeongezewa na hizo 2000mAh ingekuaje? Na ukija upande wa pili huyu M51 amemzidi S21 ultra unene tena kwa mbali tuu(ana 9.5mm, bado 0.5mm tuu agonge 1cm), sababu ni nini? Utagundua ni battery, kitu ambacho Samsung hawezi kubali kwenye flagship zake.

3.Space, Ieleweke ukisikia simu ina kitu hiki na hiki cha ziada, jamani hivi vitu vinaanzia kwenye hardware, hivyo vinahitaji space kuvi accommodate, flagship hua inaongezewa features mfano heart rate sensor, wireless charging, camera bora, speaker bora, au hio note 10 uliyoitaja, inahitaji space zaidi kwa ajili ya ku accommodate ile S-pen, ambayo kimahesabu hio pen tuu imechukua sehemu ya 900mAh, umeona sasa? n.k n.k, hivi vitu vyote vinahitaji space, hivyo kufanya eneo la battery kua finyu..

4. Businesses strategies, battery ni hitaji kubwa sana kwenye simuu, kuna watu hilo tuu ndilo kipaumbele chake kikubwa kwenye simu, hivyo atatafuta lets Say M31s sababu ya battery then ametosheka, Mwingne anahitaji vyote, atanunua flagship kupata features bora, halafu atachukua yenye battery kubwa itakayomsaidia kwenye bussy days, hiki ni kitu cha kawaida, sema tuu wengine pengine kutokana na hali za kiuchumi hio option inaangukia kwenye viswaswadu.
Mfano binafsi nina Samsung kubwa, halafu nina kijisamsung Duos cha Batani kwa ajili ya backup, tayari mpaka hapo ni deal kwa kampuni.

5. Upgrade, Kila Mwaka Kampuni zinatoa flagship mpya yenye features mpya za kuvutia, binadamu hata kama alichonacho kinamtosha, ila ana shauku ya kupata kikubwa zaidi kadiri ya mda. Hivyo hata kama wana uwezo wa kuweka 7000mAh leo hii, hataweka ila ataanzia kwenye 3500mAh ili mwakani akiweka 4000mAh bado uone kuna improvements, mfano note 10 plus ana 4100mAh na note 20 ultra ana 4500mAh, tayari kuna watu wanashawishika kununua note 20 ultra kwa sababu hio,
Sasa mtu alinunua S21 ultra kwa sababu ya battery ya 5000mAh, leo hii ukamletea s22 ultra ina 5000mAh tena atanunua ya nini?..

Mtazamo wangu,
Nunua Simu ambayo utaitumia bila kua na mawazo ya kuangalua battery percentage, Simu ambayo Bila kuzima Data basi inakufikisha mda wako wa kulala huku ikiwa imebaki na charge incase ya dharura ya umeme, binafsi sikumbuki ni lini nilizima data kwenye simu yangu, naperuzi kokote na kwa kujiyosheleza ila jioni nachezea 50%-40%, Sikumbuki ni lini niliwasha simu yangu, mana sijawa na sababu ya kuizima na haijawahi zima sababu ya charge.

Moja ya stress ambazo ni kero kwenye simu basi ni charge, simu ni yako lakini unaitumia kwa kuichungulia,

Sitaki kuzungumizia wale rafiki zangu wa,
please wait.....
Unfortunately Jamiiforums has stoped...
Camera is not responding.......
Twitter has crashed......
Naweza nisababishe watu wagombane na keyboard huko.
Vipi mkuu kuhusu nokia,bei na chaji......namanisha simu nzuri latest
 
Siyo uongo mkuu, nimemiliki oppo a3s, a31, a1k, realme 6 na a92 zote ukaaji wa chaji ni zaidi ya masaa 24 na data ikiwa on. Nilikuwa na samsung j6+ chaji masaa 7 tu. Kuna ndugu yangu ana Samsung a51 chaji masaa 12 imeishiwa chaji. Kwa sasa nina Redmi 9 chaji kuanzia masaa 20 ukiwa online.

Simu za oppo kama ni kupiga na kupokea tu chaji inadumu muda mrefu zaidi.
Yani wana maanisha screen on time non stop sio ukiwasha data siku nzima
 
Kaka sasa unafeli yani A10s ubora wake ni upi mpaka iishinde A12 au A12 body design yake ilivyo kaa vibaya ndio unaiona ni simu ya hovyo mpaka ukaishusha kwa A10s angalia specification mwenyewe kisha ujisahihishe

Galaxy A10s

Display 6.2 PLS IPS
720×1520 pixels

13 mp
1080p

2/3 RAM
helio p22

4000 mAh

Storage 32gb



Galaxy A12

Display 6.5 PLS IPS
720×1600

48MP
1080p

4/6 RAM
helio p35

5000 mAh

Storage 32/64/128

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
Sikatai A12 ni bora zaid ya A10s ila katika hizo nyanja mbili A12 hamkuti a10s, nakushauri shika simu zote mbili zikiwa na conditions sawa halafu njoo uniambie.
 
mAh ni nini? Unaposema 2000 au 7000 mAh .huwa nini kinamaanishwa? Tofauti ya 2000 mAh na 7000mAh ni nini?
 
mAh ni nini? Unaposema 2000 au 7000 mAh .huwa nini kinamaanishwa? Tofauti ya 2000 mAh na 7000mAh ni nini?
Ni uwezo wa battery kukaa na chaji, mfano kama battery ya simu yako ina 4000mah na inakaa masaa 10 na chaji, inamaanisha simu inatumia 400 milliapere kwa lisaa. Simu hiyo hiyo ikiwekwa battery yenye 2000mah itakaa na chaji masaa ma 5.
 
Ni uwezo wa battery kukaa na chaji, mfano kama battery ya simu yako ina 4000mah na inakaa masaa 10 na chaji, inamaanisha simu inatumia 400 milliapere kwa lisaa. Simu hiyo hiyo ikiwekwa battery yenye 2000mah itakaa na chaji masaa ma 5.
Thanxx
 
Nokia alishaacha kutengeneza Simu toka 2013, Kampuni ya sasa inayotengeneza simu za Nokia (HMD) wamenunua tu Haki za kutumia Hilo Jina, sio Nokia wenyewe.

Na lowend ni simu zenye specs ndogo na za bei rahisi most of time Laki 3 kushuka Chini.
Duuuh kama ndo hivyo kazi tunayo,hii nadhani ndo ya Bill Gates?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom