Samson Mwigamba aelezea makucha ya Mbowe na CHADEMA

Samson Mwigamba aelezea makucha ya Mbowe na CHADEMA

Mwigamba njaa ni mbaya sana ndugu yangu. Ulikuwa m1 wa watu walionishawishi kuipenda Chadema kwa makala zako za Kalamu ya mwigamba. Ila pale ulipotaka kuanzisha uasi wewe na wenzako kina Heavy kabwe na Kitila Mkumbo ndio ukawa mwisho wako.

Hutamsahau ben wa saa8.
Nini maana ya uasi? Mtu kutoa hoja ya kumpinga Mbowe ndio anakuwa muasi.
Usihukumu binadamu mwenzako wewe sio Mungu hujapewa uwezo wa kujua watakao uona na ambao hawatao uona ufalme wa Mungu
 
Na ushahidi ni huu hapa wa kuthibitisha huyu mnafiki asivyojitambua kabisa

Makala hii iliandikwa na Samson Mwigamba tar 9//12/2009
NAKUHURUMIA ZITTO KABWE
MHESHIMIWA Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, salaam.

Awali ya yote naomba kama nianze kwa kutangaza mgongano wa kimaslahi kama ilivyo kawaida kwa wabunge kufuatana na Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la Mwaka 2007.
Mgongano wa kimaslahi ni kwamba ninakuandikia waraka huu nikitaka kujadili machache juu ya mwenendo wa mambo ndani ya CHADEMA, mambo ambayo yanakugusa kila wakati nikitaka kujaribu, kwa faida ya wasomaji, kuangalia kulikoni na wakati huohuo nikijua kwamba wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na ambaye tumekuwa pamoja tukikubaliana kwa mambo karibu yote, wakati wote.

Mheshimiwa unajua urafiki wetu ni wa muda mrefu na kwa kweli nilikupenda kabla wewe hujanifahamu; nikakuhesabu kama rafiki kabla hujanifahamu na kwa bahati nzuri sana uliponifahamu ukakubali kuwa rafiki yangu. Nimekuunga mkono katika matukio, maamuzi na hata mitazamo yako mingi kwa muda mrefu.
Nilikuwa upande wako katika kupiga vita ufisadi na hata uliposimamishwa ubunge wakati wa hoja ya Buzwagi nilikuwa upande wako.

Nilikuwa upande wako ulipotoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga utaratibu wa kuwachagua wabunge wa Afrika Mashariki na hata katika kile ulichokiita ‘bifu’ kati yako na Spika wa Bunge, lililotokana na hatua yako ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge na maneno uliyoyatoa nje ya ukumbi huo kuhusu uwezo wa spika kusimamia kanuni za Bunge.
Nilikuwa pia upande wako uliposimama kumtetea Spika kuhusu hoja iliyotolewa na mwandishi mmoja akipinga uwepo wa Kamati ya Bunge ya Kutunga Sheria katika kanuni mpya za Bunge.

Nilikuwa upande wako pale ulipounga mkono maelezo ya kitaalam ya TANESCO kununua mitambo ya Dowans na hili unalifahamu zaidi maana tulikuwa tukiwasiliana sana na huenda mimi na Absalom Kibanda ni miongoni mwa waandishi wachache sana tuliodiriki kusema waziwazi kupitia kalamu zetu kwamba tunaunga mkono msimamo wako wa kununua mitambo ya Dowans.

Utakumbuka pia siku moja tulipishana mtazamo tulipokuwa tukichangia kwenye mtandao mmoja wa intaneti hoja ya utafiti wa taasisi moja iliyoonyesha kwamba bado Kikwete na CCM ni maarufu kuliko vyama vya upinzani kwa mbali sana.
Unakumbuka kwamba mimi nilitofautiana na wewe kwa hoja za kitaalam zinazohusu utafiti. Lakini baada ya kutoa hoja zako na mimi nikatoa hoja zangu na wewe ukazijibu nilikubaliana na wewe na hatimaye nikawa upande wako.
Lakini katika siku za karibuni nimejikuta nikiwa katika mfululizo wa matukio, mitazamo na maamuzi ya mimi kutokubaliana na wewe. Utakumbuka nilianza kutokubaliana na wewe kuhusu uamuzi wako wa kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa taifa wa CHADEMA.

Nilikutumia barua pepe ndefu sana nikipinga uamuzi huo na kukuomba kwamba ujitoe kwa hoja nyingi ambazo najua unazikumbuka vema.
Kwa bahati mbaya hukujibu ile barua pepe, lakini sikukata tamaa, nikaambiwa nipitie kwa msaidizi wako David Kafulila. Nikafanya hivyo na Kafulila akanihakikishia kwamba kila tunachoongea anakufikishia na kwamba unampa majibu ya kunipatia.

Lakini mheshimiwa unakumbuka kwamba mwishoni kabisa majibu yako yalikuwa ni kwamba hoja zangu zote ulikuwa unazikubali lakini ulishazizingatia kabla hujaamua kujitosa kwenye kugombea uenyekiti na hivyo usingejitoa. Nashukuru kwamba baadaye uliamua kujitoa japo ulikuwa umechelewa.
Mheshimiwa Zitto, nilitofautiana na wewe pia kwa kauli zako ulizokuwa unazitumia kutaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kujiondoa.

Katika moja ya taarifa za habari ulinukuliwa ukisema unatofautiana na Mbowe kwa sababu wewe ni mjamaa wakati yeye ni bepari. Nikawaza na kukumbuka kwamba Agosti 13, 2006 wakati chama chenu kinazinduliwa upya ulikuwepo na ninaamini ulishiriki kikamilifu katika kufanya utafiti, kuchambua na hatimaye kuja na katiba mpya iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu siku hiyo na kupitishwa kuwa katiba mpya ya chama hicho.

Na kwamba maneno haya yanayosomeka kwenye utangulizi wa katiba hiyo mpya ya CHADEMA yakiwa
yametamkwa kwa kunyanyua mikono na wajumbe wa mkutano huo mkuu, basi yalikuwa ni yako pia: “Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika Agosti 13, 2006, mjini Dar es Salaam, tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha siasa kitanachoitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya Nguvu na Mamlaka ya Umma na Dira na Dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea.

“Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitavyotungwa kwa mujibu wa Katiba ili kuimarisha kutetea, kudumisha, na kuendeleza Demokrasia ya kweli na hatimaye kuweza kuleta maendeleo ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa jamii nzima ya taifa la Tanzania.”

Kama na wewe ni miongoni mwa wana CHADEMA waliotamka maneno hayo siku hiyo kwamba: “Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitakavyotungwa kwa mujibu wa Katiba hii” nilitegemea uwe umeisoma katiba yenyewe na kuona kwamba ibara ya 3 ya katiba hiyo, ibara ndogo ya 3.B. kifungu cha 3.1.1 kinasema “CHADEMA ni chama cha itikadi ya Mrengo wa kati (center party)”.

Hata kwa elimu ndogo tu maelezo haya yanatosha kuonyesha kwamba chama hiki kinaongozwa kwa itikadi iliyoandikwa ndani ya katiba ambayo ni Mrengo wa Kati na wala si itikadi binafsi ya Mbowe ya ubepari ama ya Zitto.
Kwa imani niliyokuwa nayo kwako na nikizingatia elimu kubwa uliyokuwa nayo, nafsi yangu ikanituma kufikiria kwamba labda ‘wamekunukuu vibaya’. Nilihudhuria mkutano wenu na waandishi wa habari uliokusudia kuzika tofauti zenu na Mbowe na kusonga mbele kama chama.

Pale ulipoulizwa swali na mwandishi mmoja kwamba utawezaje kufanya kazi na Mbowe wakati wewe ni mjamaa na yeye ni bepari; ukajibu kwa namna ambayo haikukata kiu yangu ndipo nikaamini kwamba kumbe hukunukuliwa vibaya bali ni kweli ulisema maneno hayo.
Nilipingana na wewe pia pale ulipoamua kupinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA).

Unakumbuka kwamba nilialikwa katika uchaguzi huo miongoni mwa wageni wachache wanafunzi, wanahabari, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali walioalikwa kushuhudia uchaguzi ule.
Wakati wa uchaguzi wenyewe utakumbuka mimi na wewe tulikaa meza moja na tulitenganishwa na mtu mmoja tu (Mkurugenzi wa Uenezi Taifa wa CHADEMA, Erasto Tumbo).

Nilitegemea mambo yasiyoendana na sera na kauli mbiu za chama chenu ambazo zinatangazwa hata katika jina la chama (DEMOKRASIA na MAENDELEO) ambayo yalifanyika pale ukumbini uliyaona.
Najua jioni wakati wa kutangaza matokeo hukuwepo lakini nategemea ulipata taarifa za kauli za vijana mbalimbali walizotoa pale wakitaja waziwazi majina ya watu walioharibu uchaguzi ule.

Sikutarajia kama Naibu Katibu Mkuu wa chama upinge hatua ile iliyochukuliwa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na kikao kingine chochote cha juu ya msimamizi wa uchaguzi eti kwa sababu tu rafiki yako Kafulila alikuwa anaongoza.
Hilo lilinipa taabu kubwa na naomba uniwie radhi rafiki yangu lakini nasema ukweli wa nafsi yangu kwamba nilifikia kujiuliza mara mbilimbili kama ungechaguliwa wewe kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, hali ingekuwaje?

Na mwisho nilipingana na wewe pale ulipopinga kwenye vyombo vya habari kuvuliwa wadhifa kwa David Kafulila. Kwanza ulionekana umeweka ubaguzi kwa sababu katika maneno yote uliyonukuliwa ulisisitiza juu ya Kafulila peke yake na hukumgusia kabisa Danda Juju wakati wote walivuliwa kwa sababu
zinazofanana.

Lakini kwa sababu Kafulila ni rafiki yako sana, umemwandaa kuwa mbunge na unamuunga mkono katika harakati zake, na ni mbunge mtarajiwa kwa kuwa anakubalika sana jimboni basi ukamtetea na kumsahau ‘mhanga’ mwenzake. Hilo tu linafanya tutofautiane na zaidi sana tunatofautiana kwa kupinga maamuzi ya Katibu Mkuu wako nje ya vikao, maamuzi aliyoyachukua kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

Najua yote haya umeamua kuwa kimya hujayatolea kauli yako ikiwa ni pamoja na yale ya kumfadhili Kafulila kwenda Kigoma kuichafua vizuri CHADEMA. Lakini kama ni kweli, napingana na wewe na kama unaendelea kukaa kimya nitaamini kwamba ni kweli.
Sasa limeibuka la kusema kwamba unatembea na barua ya kujiuzulu nyadhifa zako zote ndani ya CHADEMA ikiwa ni pamoja na ubunge. Bado pia sijapata kauli yako, narudia kusema kwa kuendelea kunyamaza unanifanya niamini kuwa ni kweli.

Na kama ni kweli, nakuhurumia sana Zitto Kabwe. Sasa naona kile nilichokuambia wakati nikikushauri ujitoe kugombea uenyekiti kinatimia. Nilikuambia ujitoe haraka tena kimyakimya kwa kumweleza tu Katibu Mkuu aweke fomu yako pembeni lakini hukutaka kunisikia.

Lakini utakumbuka moja ya sentesi zangu ilikuonya kwamba ukingang’ania kugombea iwe umeshinda
uenyekiti ama umeshindwa utapata shida kubwa. Nilikueleza kwamba hutaaminika tena na Watanzania na kila kitu utakachofanya utaonekana kama ulikuwa ni mamluki ndani ya chama.
Ni kwa bahati kwamba umetokea kuwa na viongozi wenye busara sana kina Freeman Mbowe na kina Dk. Wilbrod Slaa wakisaidiwa na hekima na kamati ya wazee.

Hawa wakaamua kukurejesha kwenye unaibu katibu mkuu. Nilishuhudia siku ile wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA walivyoshangilia uteuzi wako na wa Dk. Slaa na Hamad Yusuph kama wakuu wa Sekretarieti ya chama.
Nilidhani sasa ungetulia na kufanya kazi ya kujenga chama chenu na kusonga mbele lakini haikuwa hivyo.
Baada ya kushauriana sana wakati ule ulipotaka kugombea uenyekiti niliamua kutafuta habari za kiuchunguzi ndani ya CHADEMA. Nimeongea na viongozi mbalimbali na maofisa wa CHADEMA makao makuu, nimeongea sana na David Kafulila na hata niliwahi kumsikiliza mama yako mzazi akiongea na watu ambao sikuwafahamu.

Nimegundua kitu kimoja tu: kwamba kama mambo haya huyafanyi kwa makusudi na kwa malengo maalumu, basi watu uliowaamini sana ndani ya CHADEMA hata kama walikuwa na nyadhifa ndogo, walikubali kutumiwa ili wakutumie wewe kuimaliza CHADEMA na wewe ukaingia mkenge.
Ukakubali kugombanishwa na viongozi wenzako wa ngazi za juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe ili malengo ya watu hao yatimie. Sasa nakuonea huruma.

Nakuonea huruma kwa sababu kama ni malengo ya hao watu kukutumia kukimaliza chama hawatafanikiwa na badala yake watakumaliza wewe bure na utakuja
kushtuka ukiwa umekwisha kisiasa.

Kama ni malengo yako kwa utashi wako umeamua kutumika kukimaliza chama, nakuhurumia kwa sababu utajimaliza wewe na CHADEMA itaendelea kuimarika bila wewe wala Kafulila.
Ukitaka kujua ninachokisema, tuulize sisi waandishi tunaopata mawazo ya Watanzania moja kwa moja.
Kwa kuanzia muulize tu Edward Kinabo kwamba Jumatano iliyopita alipoandika makala ya “Simwelewi Zitto Kabwe” aliungwa mkono na wasomaji wangapi na walikuwa na mawazo gani juu yako. Hapo ndipo utakapoelewa kile ninachokisema.

Namalizia kwa ujumbe wa msomaji wangu mmoja tu kati ya wengi. Huyu aliniambia anaitwa Meshack na yuko Korogwe. Aliniambia, “Sisi tulishajua kwamba Zitto anaondoka CHADEMA na kwamba anachosubiri tu ni pensheni yake ya ubunge ambayo huwa inatolewa baada ya Bunge kuvunjwa.

Naomba Mwigamba kwa sababu unaweza kuongea na viongozi wakuu wa CHADEMA, waambie kwamba
wasije wakafanya kosa la kumvua Zitto uongozi wala kumvua uanachama.
Sisi hatutaki apate kisingizio cha kuondoka CHADEMA. Waambie wamuache tu mpaka atakapoondoka mwenyewe ili Watanzania wazidi kumfahamu,” mwisho wa kunukuu.


Tafakari mwenyewe ulikofika, uamue cha kufanya. Kumbuka uamuzi wa mwisho ni wako wengine tunakueleza tu maana tumejiapiza kuzungumza ukweli hata katikati ya ugomvi.

Kama utaamua kuondoka CHADEMA ama kujivua tu nyadhifa zako. katika yote nakutakia kila heri!


Hata kwenye ndoa ukishaona mtu anaoa au luolewa mara ya kwanza ya pili ya tatu ujue huyo ni mushkeli. Ni kukosa msimamo kimaisha.
 
Na. Mwandishi wetu.
Kada wa chama cha Mapinduzi CCM ambaye kwa nyakati tofauti amepata kuwa mwenyekiti wa mkoa wa wa Arusha chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na baadae kutimkia ACT WAZALENDO kuwa muasisi na katibu mkuu wa kwanza wa chama hicho Samson Maingu Mwigamba amewasikitikia watanzania wa vyama vyote wanaohama vyama vyao na kujiunga na CHADEMA na kusema hawana tofauti na mtu anayeruka vumbi na kukanyaga moto na kusisitiza kuwa sifa kuu ya kukuwezesha kuishi kwenye chama hicho ni UNDUMILAKUWILI.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mkoani Arusha hivi karibuni, mwigamba amesema kwamba chama hicho chake cha awali kimepoteza uwezo wake wa asili wa kujisimamia na hivyo kujikuta kinaenda enda tu sambamba na kusema kuwa chama hicho sio mfano mzuri wa kimbilio la demokrasia na utawala wa sharia unaofuata katiba na usimamizi bora wa fedha akitoa mifano kadhaa.
View attachment 736419
‘’huwezi hama CCM halafu useme unafuata Demokrasia CHADEMA, utakuwa unachekesha rafiki yangu, pale CHADEMA demokrasia ni Mwenyekiti na mwenyekiti ndio Demokrasia, analotaka ndio huwa na ukijaribu kumkosoa lazima uende na maji’’. Anaanza kueleza Mwigamba

‘’mimi ni kama nimekulia ndani ya Chadema nikishiriki katika nafasi mbalimbali za ndani ya chama, nakuhakikishia kama kuna chama kinasigina katiba basi CHADEMA ni namba moja…kumbuka namna mbowe na wenzake walivyokinyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ili kimpe yeye nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kudumu, na kumbuka siku tu niliyoanza kuhoji kuhusu hilo nilivyofurumushwa kama kuku pori’’. Anaongeza Mwigamba huku akicheka

Mwigamba anaendele kusema kuwa mara baada ya mbowe kuchukua kijiti cha uenyekiti wa chama hicho alijidhatiti kuhakikisha chama hicho kinakuwa na agenda ya kuisimamia ili kipate kuaminiwa na wananchi na hatimaye kupewa dola jambo ambalo chadema ilifanikiwa kwa kujitanabaisha wazi kuwa wao ni watetezi wa rasilimali za nchi na wapinga ubadhilifu na ain azote za ufisadi.
anasema aliwahi kusimuliwa kisa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kuhusu chanzo chama hicho kushikilia ajenda ya kupiga vita ufisadi ambapon alimwambia kuwa mwaka 2004 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti taifa alialikwa kwenye mikutano mikuu ya vyama vya Republican na Democrats vya Marekani alipokutana na Mwanasheria Kivuli aliyetokana na chama cha Democrats wakati huo Republican ikiwa inaongoza nchi chini ya Rais George Bush na mwanasheria huyo kumweleza Mbowe kwamba haijalishi chama kina sera nzuri kiasi gani, lazima kiaminiwe na wananchi.

samson-mwigamba.jpg

Samson Mwigamba siku alipojiunga CCM.
Aidha mwigamba anasimulia zaidi kuwa mwanasheria huyo alimweleza mbowe kwamba ameishi Tanzania kwa vipindi tofauti na katika kufanya kazi zake na utafiti aligundua kwamba nchi ilikuwa inapoteza pesa nyingi kupitia ufisadi na kumwambia Mbowe kwamba kama nchi ikifanikiwa kuzuia pesa zinazopotea kwa ufisadi, haitahitaji tena kuwa na bajeti tegemezi kwa mataifa ya nje na kumshauri kuangalia vitabu vya taarifa za Mdhibiti na MKaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anazozitoa kila mwaka ataona pesa nyingi zinavyopotea na huo ndio ukawa mwanzo wa Mbowe wakati huo akiwa mbunge wa Hai, kuanza kuzunguka mikoani akiambatana na wabunge wengine wa CHADEMA ya wakati huo ambao ni Marehemu Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Dr. Willibrod Slaa (Karatu), Dr. Amani Walid Kabourou (Kigoma mjini) na Grace Kiwelu (Viti maalum) kuelezea mapungufu waliyoyaona wakiwa na ripoti za CAG wakiwaeleza wananchi jinsi ufisadi ulivyokuwa unatafuta mabilioni ya pesa za watanzania maskini.
‘’Huo ndio ukawa mwanzo wa CHADEMA kushikilia ajenda hiyo ya ufisadi mpaka wakaingia nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo Mbowe aligombea urais na kushindwa na Jakaya Kikwete lakini wakapata wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa viti maalum. Ni uchaguzi huo ndio uliowaleta bungeni akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na wenzao na hoja ya ufisadi ikawa ni hoja hasa’’. Anaendelea Mwigamba

Mwigamba anasema kuwa Mbowe alimwambia kwamba waliamua kwenye kamati kuu kwamba kabla ya wabunge wao hawajaenda bungeni, chama kiwe kimefanya utafiti na kuvumbua madudu ya ufisadi ili wanapoenda bungeni wayasimamie hayo na ndio zama zilizoibuka kashfa ambazo majina yake yamebaki kwenye kumbukumbu za watanzania kashfa kama za Meremeta, Deep Green, EPA, Richmond, Buzwagi, na nyinginezo

“Ajenda hiyo ikaipelekea CHADEMA kuwa maarufu sana nchini kiasi cha uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa akagombea urais na kuchuana vikali na Kikwete. Ingawa hakushinda, chama kilichupa kutoka wabunge watano wa majimbo mpaka 23 na baadaye 24, na kutoka wabunge 6 wa viti maalum mpaka 25. Chama kikawa maarufu kiasi cha kufikiriwa kuingia madarakani mwaka 2015. Mbowe alirudia kunihadithia kisa cha huyo mwanasheria kivuli wa kimarekani mara pili tukiwa Karatu mwaka 2012 akitamba juu ya kuutumia vizuri ushauri wa mwanasheria huyo”, anasema Mwigamba.
Mwigamba anasema kwa kipindi kirefu chama hicho kilifanikiwa kujijengea sura ya kuwa watetezi wa Rasilimali za nchi na waoinga ufisadi wakiwa nje lakini wanapokuwa ndani ya chama wanakuwa na madudu makubwa hasa yanayohusu matumizi ya fedha hasa zinazotokana na ruzuku na hivyo kusababisha mitafaruku mikubwa miongoni mwa wananchama na viongozi wao kama ile iliyowahusisha Mbowe na Marehem Chacha Wangwe, na huu wa karibuni baina ya Mbowe na Zitto kabwe ulioishia kwa Zitto kufukuzwa uanachama na hatimaye kutimkia ACT WAZALENDO
“Lakini ndugu mwandishi hebu rejea mwaka 2013 uone Mbowe alivyofanya juhudi kubwa kuvuruga chama kwa matayarisho ya kuja kumpokea yule waliyempachika nembo ya ufisadi. Walianza na Zitto, Kitila na mimi wakamalizia kwa Slaa 2015 na gia ikawa imebadilishiwa angani. Muulize leo Mbowe kuhusu ushauri wa yule mmarekani na wapi wameipotezea ajenda yao ya ufisadi mpaka wananchi wanakosa Imani na chama chao, atakuambia alibadilisha gia angani’’. anasema
‘’alibadilisha gia angani akamchukua Lowassa ambaye Lema alisema kumzomea fisadi kama Lowassa ni heshima kwa Mungu, Msigwa akasema anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili, Lissu akasema CCM wamempa fomu ya kugombea urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani. Leo Nyalandu anaenda kujiunga na chama cha kubadilishia gia angani!!!? ameshajua Mbowe 2020 akibadilisha gia angani ataelekeza wapi chama?” anahoji Mwigamba huku akicheka kwa utani.
‘’huwezi kuwaelewa chadema kama ni popo au ndege, mchana wanasimamia hili, jioni lile basi ilimradi tu…hebu ona mbowe alivyokuwa anasema Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA…leo amebanwa nayeye kwenye madili yake amegeuka anasema Magufuli dikteta/…hakuna Dikteta katika siasa za Tanzania kumzidi Mbowe nakuambia mimi, chadema wanalijua hilo na UKAWA halikadharika’’.
‘’akigeuka huku anaona waliojihusisha na ufisadi wanapukutishwa kutoka serikalini, akigeuka anaona utumishi wa umma unavyorejea kwenye uadilifu na uchapakazi, miradi ya maji inatekelezwa hata iliyolala kwa miaka, miradi ya barabara za juu iliyohubiriwa kwa miaka inaanza, reli ya standard gauge iliyoishia kusemwa midomoni kwa karne inanyanyuka, miradi ya umeme, nk, akaona hapo hana jinsi, akasema rais anatekeleza ilani ya CHADEMA’’. Anaendelea Mwigamba
‘’ Mbowe na CHADEMA yake walipoona rais anawashughulikia mpaka wale waliowachangia wao pesa za kampeni na hatimaye kumgusa Mbowe mwenyewe kwa ufisadi mkubwa aliolifanyia shirika la nyumba la taifa kwa makumi ya miaka, hali yao ikawa ngumu vijana wa mtaani wanasema siku hizi vyuma vikakaza, wakaanza kusema rais anavunja sheria na hatimaye wakaibuka na udikteta’’. Mwigamba anaongeza
Tukio jingine alilolibainisha Mwigamba ni la Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye.
’’ Ni Sumaye huyu huyu aliyeshambuliwa sana na Mbowe na CHADEMA yake miaka ya 2000 pale wafanyabiashara wasio wana CCM walipolalamika kunyanyaswa na mamlaka ya serikali hususani TRA. Sumaye akaibuka na kusema,…. Kama mfanyabiashara unataka mambo yako yakunyookee, tundika bendera ya CCM kwenye biashara yako…. Walimtukana Sumaye kila matusi na kuonyesha anavyotumia vibaya madaraka ya uwaziri mkuu lakini leo Sumaye ni nguzo kuu kwenye CHADEMA’’.
‘’Hauwezi kuwa na akili timamu halafu uwaamini chadema si unakumbuka Kwenye uchaguzi wa 2015 kimsingi Sumaye ndiye alikuwa mpiga zumari mkuu na sasa ni mmoja wa watu wanaopigiwa upatu ndani ya CHADEMA kugombea urais 2020 mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote lakini anayeongoza kwa kukosa alama hata moja aliyoiacha eti leo agombee urais!!!? Hiyo ndiyo CHADEMA’’. Anazidi kueleza

IMG-20150727-WA0027.jpg

“Mtazame hata huyuNyalandu mwenyewe. Angalia clip ya video ya Joshua Nassari bungeni, angalia tweets za Mch. Msigwa na Halima Mdee. Hivi hawaoni hata aibu mtu ambaye haijapita hata miaka mitatu tangu mmwite majina ya kila aina (mshika makalio ya mabinti askari wa wanyamapori, mtalii wa kutumbua kodi za watanzania na wasanii Marekani, fisadi wa hati za rais za uwindaji, nk) leo mnamwita kamanda, jembe, mara dume, mmh!”
Mwigamba anawapa pole sana wale wote wanaokimbilia CHADEMA na wale wanaojiandaa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.
''Kama ni mafisadi waende maana kwenye seerikali ya Magufuli hamna namna ya fisadi kusurvive. Ni sawa na kumwambia mwenye dhambi asurvive mbele ya nuru ya Mwenyezi Mungu. Haiwezekani. Wa namna hiyo watangulie tu CHADEMA ndiko kwenye ngome mpya ya mafisadi. Lakini wale walio waadilifu wanaodhani kule ni kimbilio, wamuulize Dr. Slaa atawasimulia vizuri zaidi. CHADEMA mchana unaweza kuwaona malaika safi toka mbinguni na usiku ukakuta ni mashetani wenye mapembe kabisa!''. alimalizia
Ipo siku Mwigamba unaweza kimbia CCM ukaanza kuisema vibaya pia. Maana ulipokua CDM ulikua unaiona CCM ya hovyo. Najua ukikosa cheo CCM utakuja kutukimbia tu kama ulivyotoka CDM ukaenda ACT Wazalendo na leo upo Chama kikubwa CCM ambacho misingi yake ni imara na kinaongozwa na kujitofautisha kwa misingi ya kiitikadi na falsafa na sio uwanaharakati
 
Well said Mheshimiwa Mwigamba. Chadema is dead as a party.
Sasa chadema iliyokufa tunaweka viongozi wao vizuizini na kutumia muda mwingi kuishambulia badala ya kutekeleza ila tuko kulumbana na chadama.
Mwigamba ametumia kipimo cha chadema kuzuiwa kufanya shushuli za siasa.
Mku nikuambie hivi hiki chama kinazidi kuimariaka zaidi ya mara nne leo hii turuhusu waendelee na shuhhuli zao tuone.
Tusijifanye hatuoni yanayoendelea kisa ni ukada ukada usikufanye mtumwa wakati mambo yako wazi kabisa.
 
Ipo siku Mwigamba unaweza kimbia CCM ukaanza kuisema vibaya pia. Maana ulipokua CDM ulikua unaiona CCM ya hovyo. Najua ukikosa cheo CCM utakuja kutukimbia tu kama ulivyotoka CDM ukaenda ACT Wazalendo na leo upo Chama kikubwa CCM ambacho misingi yake ni imara na kinaongozwa na kujitofautisha kwa misingi ya kiitikadi na falsafa na sio uwanaharakati
Mku Mawakala hawaaminiki.
Mfano angalia mgogoro wa Urusi na England hayo yote ni tamaa za watu aina ya Mwigamba mm chama changu ccm niliwapa tahadhari juu ya huu usajili wa chama kipya ndani ya chama hakitatuacha salama kwani hawa wote sio wa kuaminika ukishakuwa ni mwepesi kutumika na adui tayari ni ugonjwa hauponi huo ila jibu ni muda
 
Ningemwelewa tu kama angesema na udhaifu wa ACT aliyoihama na kwenda ccm. Hii ni kwa sababu ya mbowe tumemwelewa lakini kitendo chavyeye kuhama act kinamwondolea credibility ya aliyoyazungumza.
 
Nilikuwa nafurahia makala za Mwigamba akiwa CHADEMA. Sikuona shida sana alipoenda ACT ingawa nimekuwa na mashaka sana na utimilifu (credibility) wa Zitto. LAKINI alipoenda CCM nikahisi huyu keshakwisha kisiasa.

Kwa kifupi, alipofikia na kwa maelezo aliyoyatoa hapa, UAMUZI SAHIHI kwake ni kuachana na siasa za vyama kabisa na kuwa mtazamaji kama sisi wengine. Nafikiri bado anao uwezo wa kuona aliyoyasema hapa yanavyowiana na hapo alipo leo hii. Sidhani kama ndio kakubali kutumiwa kujenga hoja ya kupinga umuhimu wa demokrasia Tanzania kirahisi hivyo! Labda kama na yeye ameamua kujiunga na watu wa ovyo sana waliojitokeza kwa nguvu awamu hii.
 
ngoja, kuna siku watakosa maneno hawa wahama vyama
 
hivi ccm kuna demokrasia? teh teh nafasi ya mwenyekiti kugombea lazima uwe rais na unapigiwa kura za ndio huyo na hapana mwingine ni huyohyo. mwigamba kachanganyikiwa.
 
Kwa hiyo malamiko huyaoni mpaka mpaka Maskofu wanatoa waraka bado huoni sio.
Mku mwenye nia nzuri huonekana na upingaji uzidi mpaka kwa Makundi ambayo ulikuwa hutegemei basi jaribu kujicheki mwenyewe ktk akili yako kama mahali hauko vizuri
Hata yesu aliposalitiwa baraza la maaskofu na wakuu wa dini walitoa waraka na wakakata shauri yesu asurubiwe acha upuuzi nani kakuambia askofu hawezi kutumiwa na wanasiasa??wewe ni mkristo?waraka wa pasaka uliona wapi ukawa unasemea wanasiasa hio ni kazi ya kanisa na lengo la pasaka kukumbuka mateso ya wanasiasa??
 
hivi ccm kuna demokrasia? teh teh nafasi ya mwenyekiti kugombea lazima uwe rais na unapigiwa kura za ndio huyo na hapana mwingine ni huyohyo. mwigamba kachanganyikiwa.
Usiropoke tena nafasi ya mwenyekiti sio lazima apewe raisi imezoeleka hivo kwa shauri la baraza kuu la NEC kuepusha conflict of interest kati ya mwenyekiti wa chama na rais kwa kua wote ni chama kimoja...ni maamuzi ya kwa pamoja ya baraza kuu sio ilani wala katiba ya ccm ni kama vile wanachama walipokubali raisi awe mgombea wa chama kwa mihula yote miwili ...ni maamuzi ya chama kwa ridhaa ya wanachama...hio ni demokrasia...
 
Ningemwelewa tu kama angesema na udhaifu wa ACT aliyoihama na kwenda ccm. Hii ni kwa sababu ya mbowe tumemwelewa lakini kitendo chavyeye kuhama act kinamwondolea credibility ya aliyoyazungumza.
Sio kila anayehama chama ameona udhaifu wengine wanahamia ccm kwa sababu ndio chama kilichotawala siasa na ndio chama pekee chenye imani ya nchi na wananchi
 
Hata kwenye ndoa ukishaona mtu anaoa au luolewa mara ya kwanza ya pili ya tatu ujue huyo ni mushkeli. Ni kukosa msimamo kimaisha.
Huyu Mwigamba anahitaji cheo na hana lolote la maana na isitoshe sasa hivi kuna halmashaur hazina wakurugenzi akaze Uzi kwa kumsifia Rais
Ccm wanataka kumpandkiza mtu Chadema ambaye atatekeleza yale wanayoyataka!
 
Hivi huyu jamaa hawajamkumbuka hata U-DC? Maana mtaani hali tete! By the way Jerry Muro yeye vipi? Mbona siku hizi hasikiki?
 
CCM ni chama cha siasa,samson ni mwanasiasa hawezi ona jambo linatokea katika jamii alifumbie macho kisa sio chama chake,sote ni waTanzania
Ila anaendelea kufumbia macho maovu ya ccm sababu ndo chama chake kipya na hasa kwa sababu anategemea kupata uteuzi hivi karibuni!
 
Hata yesu aliposalitiwa baraza la maaskofu na wakuu wa dini walitoa waraka na wakakata shauri yesu asurubiwe acha upuuzi nani kakuambia askofu hawezi kutumiwa na wanasiasa??wewe ni mkristo?waraka wa pasaka uliona wapi ukawa unasemea wanasiasa hio ni kazi ya kanisa na lengo la pasaka kukumbuka mateso ya wanasiasa??
Kwani malalamiko yao ni nini.
 
Sasa kakuambia anamchukia mbowe au amekana mbowe hajamkuza kisiasa??ameeleza mbowe kabadili gia angani ..na hio mwenyekiti bora afrika umeinukuu chombo kipi cha habari?ameainisha jinsi mbowe katumia mabavu kujieka mwenyekiti wa kudumu,jinsi asivyokua na demokrasia na jinsi alivyokua na uchu na utawala kiasi chA kuondoa wale waliompinga kwenye kuendesha chama
Nafiki hoja ya Mkwaru in kwamba Mwigamba anaweza kuwa sahihi kuhusu Mbowe na Chadema lakini maadamu safari yake kisiasa bado inaendelea ni vyema economical with words. Aweke "akiba ya maneno" sababu hao anawananga leo ndiyo waliochangia pakubwa ku- elevate profile yake. Ni suala kuonyesha appreciation pia!
 
Hata yesu aliposalitiwa baraza la maaskofu na wakuu wa dini walitoa waraka na wakakata shauri yesu asurubiwe acha upuuzi nani kakuambia askofu hawezi kutumiwa na wanasiasa??wewe ni mkristo?waraka wa pasaka uliona wapi ukawa unasemea wanasiasa hio ni kazi ya kanisa na lengo la pasaka kukumbuka mateso ya wanasiasa??
Mku hoja ni matusi tena.
Ni vuzuri ukaja na hoja sio bomba la matusi utakuwa umeongeza upeo wako. Kuja na matusi ni kukimbia hoja usiwemwoga wa majukumu
 
Back
Top Bottom