Samson Mwigamba aelezea makucha ya Mbowe na CHADEMA

Thibitisha. Hili ni miongoni mwa magazeti yanayoendeshwa kijinga, yanaandaliwa kijinga kwa ajili ya wajinga. Haya pamoja na Tanzanite, Tazama; na the like ukienda kwa printer unakuta yamelipiwa matoleo hata matano ya mbele ili yaandike ujinga kwa ajili ya wajinga! Sales zake hata 1/100 haifiki. Kawadanganyeni wajinga wanzenu!
Lengo la gazeti kama chombo cha habari ni kuongoza sales au kueneza habari ? Ukiwa na gazeti linalojikita kwenye mauzo ukawa na gazeti linalojikita kwenye habari, lipi lina probability kubwa ya kuandika ujinga?
 
Ukija kwenye appreciation hoja yangu ni kwamba vyama pinzani vimekosa hio appreciation kwa taifa lao na wanaoliongoza sasa sioni sababu why samson inabidi amuappreciate mbowe ikiwa mbowe kwa akili zake timamu amegoma kuappreciate juhudi za serikali...hatuezi kua na double standards zinazoruhusu appreciations kwa mbowe na matusi kwa raisi kama tunajikita kwenye mapungufu ya mtu basi mwigamba ana haki kuanika mapungufu ya mbowe..
Nafikiri kumbukumbu zetu zinatofautiana ndo maana mara nyingine in vizuri kukubaliana kutokukubaliana. Mimi nakumbuka mara kadhaa Mbowe ame-appreciate kazi ya serikali (siyo ya magu).

Hata hivyo, katika mazingira ya sasa kisiasa, maovu ya serikali yanafunika uzuri wake kwa shela nyeusi na kufanya wapinzani kushindwa kutoa comments ambazo in chanya. Anyway, bado no wajibu wa wapinzani kukosoa serikali; na hawalazimiki kuisifia inapotimiza wajibu wake.

Obviously hata Mwigamba si lazima kuonyesha appreciation kwa Mbowe lakini ukweli anaujua!
 
Kama hujaona hoja yeyote kwenye hayo majibu niliyokupa kuhusu askofu na waraka umejitukana mwenyewe tayari soma tena ona hoja yangu niliyokupa kwanzia zama za yesu mpaka zama zetu maaskofu wamekua wakitumika kwa maslahi yao binafsi...askofu sio malaika ni binadamu kama wewe aliyosoma dini tu na sio kila msomi ana maadili ya taaluma aliyosomea..wenye maadili hawawezi tumia taaluma yao kufanya kazi za wengine
Mbona hujibu nimekuuliza shida ya maskofu nini ya waraka wao unahusu nini.
Hayo mengine ninyongeza yako cha muhimu ni malalamiko yao yafanyiwe kazi
 
Mbona hujibu nimekuuliza shida ya maskofu nini ya waraka wao unahusu nini.
Hayo mengine ninyongeza yako cha muhimu ni malalamiko yao yafanyiwe kazi
Hayawezi yakasikilizwa ihali maaskofu wao wenyewe wanajieka kwenye hali ya maswali kwa waumini wao,maaskofu sio wanasiasa na hawana taaluma yakuwafanya wajadili mambo ya siasa kwenye waraka wa pasaka na sio kazi yao..hio ndio shida ya maaskofu..waraka wa pasaka ulibidi ukemee dhambi kama ushoga,uhaini,matusi,wizi,uzinzi,kutokua na hofu ya Mungu na dhambi nyengine kadhalika
 
Hayawezi yakasikilizwa ihali maaskofu wao wenyewe wanajieka kwenye hali ya maswali kwa waumini wao,maaskofu sio wanasiasa na hawana taaluma yakuwafanya wajadili mambo ya siasa kwenye waraka wa pasaka na sio kazi yao..hio ndio shida ya maaskofu..waraka wa pasaka ulibidi ukemee dhambi kama ushoga,uhaini,matusi,wizi,uzinzi,kutokua na hofu ya Mungu na dhambi nyengine kadhalika
Nimekuuliza malalamiko yao ni nini.
Sijakuuliza kama wao ni wanasiasa kinachotusumbua ss ccm kama chama ni kuwaona watu hawana uwelewa wa mambo kumbe ziii.
Nikuambie tuu ndugu tuhuma walizokuja nazo sina mashiko ndio maana Rais alisema yalipotokea matatizo ya Kibiti na Mkuranga Maskofu hawakuongea na kumbuka hili sio jibu la waraka wao.
Zaidi imezidi kuibua mjadala inakuwa baada ya majibu au kufanyiwa kazi tuzidi kuongeza sitofamu juu ya jambo lenyewe.
Mku ukizidi kukaa na tatizo kinachofuata ni kuongeza tatizo juu ya tatizo kwani halitaki kujibiwa
 
Ukiwa unadai demokrasia ukumbuke demokrasia inaruhusu mtu yeyote kua chama chochote na kutoka muda wowote kwenda chama chochote au demokrasia mnayotaka ni ya kuanika ujinga wenu mitandaoni??
Demokrasia ya kuacha ukondoo
 
Sasa kama Wananchi wamepoteza imani na Chadema kwanini CCM haitaki tume huru ya uchaguzi?!
 
Lengo la gazeti kama chombo cha habari ni kuongoza sales au kueneza habari ? Ukiwa na gazeti linalojikita kwenye mauzo ukawa na gazeti linalojikita kwenye habari, lipi lina probability kubwa ya kuandika ujinga?
Una wazimu kweli? Wewe na wapuuzi wenzako mnafikiri kama hatujui kuwa pesa zinazoendesha huo uchafu ni kodi zetu? Wewe na wajinga wenzako wala hamuumizi kichwa kuhusu gharama za kuchapa huo uchafu halafu unakuja hapa na hoja ya kijinga ya kuongeza sales. Hizo takataka mnazochapisha ndiko "kujikita kwenye habari"?
 
Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.

Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake. CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini?

Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu.

Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwanachama.

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.

Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.
Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.

Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA.

Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao.

Leo nitaainisha mambo machache tu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa.

Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti.

Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.

Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe, bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

2. Matumizi ya fedha za chama:

Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha.

Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha.

Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michango ya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje.

Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.

3. Taarifa za fedha

Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama.
Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao.
Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama

Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio.

Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana.

Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi

Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa.

Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana.

Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari na pikipiki zote za M4C.

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana.

Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si ufisadi ni nini?

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama

Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vitu.
 
Huyo gaidi wanamchelewesha tu kama alifikia hatua ya kutapeli familia yake kwa kujimilikisha mali zote za urithi wampige haraka mvua 50
 
Si alianzisha chama chake ACT hyu bwana, cha kushangaza waliyokua wanampinga Mbowe wameyafanya wao wenyewe. Wakaishia kumuita Zitto dikteta vile vile.

Kiufupi kusimamisha chama nchi nzima sio kitu kidogo, at least watamheshimu Mbowe kwa hilo. Changamoto walizopitia CHADEMA ni kubwa ila wapo imara kitu ambacho vyama vingine vilipotea kabisa.
 

Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.​


Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.​

Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake. CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini?​

Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?​

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu.​

Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwanachama.​

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.​

Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.​

Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.​

Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.​

Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.​

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA.​

Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao.​

Leo nitaainisha mambo machache tu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:​

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano.​

Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa.​

Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.​

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti.​

Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.​

Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe, bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.​

2. Matumizi ya fedha za chama:​

Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha.​

Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha.​

Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.​

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michango ya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje.​

Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.​

3. Taarifa za fedha​

Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama.​

Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao.​

Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.​

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama​

Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio.​

Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana.​

Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.​

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi​

Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa.​

Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana.​

Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari na pikipiki zote za M4C.​

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana.​

Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si ufisadi ni nini?​

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama​

Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vitu.​

Kwanza taja namba yako ya uanachama,pili hizi nguvu za kuichokonoa Chadema,zielekeze ccm na Serikali yao,maana ndio wameshika hazina ya nchi
 
Back
Top Bottom