Samson Mwigamba aelezea makucha ya Mbowe na CHADEMA

Mar 30, 2018
62
57
Na. Mwandishi wetu.

Kada wa chama cha Mapinduzi CCM ambaye kwa nyakati tofauti amepata kuwa mwenyekiti wa mkoa wa wa Arusha chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na baadae kutimkia ACT WAZALENDO kuwa muasisi na katibu mkuu wa kwanza wa chama hicho Samson Maingu Mwigamba amewasikitikia watanzania wa vyama vyote wanaohama vyama vyao na kujiunga na CHADEMA na kusema hawana tofauti na mtu anayeruka vumbi na kukanyaga moto na kusisitiza kuwa sifa kuu ya kukuwezesha kuishi kwenye chama hicho ni UNDUMILAKUWILI.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mkoani Arusha hivi karibuni, Mwigamba amesema kwamba chama hicho chake cha awali kimepoteza uwezo wake wa asili wa kujisimamia na hivyo kujikuta kinaenda enda tu sambamba na kusema kuwa chama hicho sio mfano mzuri wa kimbilio la demokrasia na utawala wa sharia unaofuata katiba na usimamizi bora wa fedha akitoa mifano kadhaa.
upload_2018-4-6_19-53-32.jpeg


‘’huwezi hama CCM halafu useme unafuata Demokrasia CHADEMA, utakuwa unachekesha rafiki yangu, pale CHADEMA demokrasia ni Mwenyekiti na mwenyekiti ndio Demokrasia, analotaka ndio huwa na ukijaribu kumkosoa lazima uende na maji’’. Anaanza kueleza Mwigamba

‘’Mimi ni kama nimekulia ndani ya Chadema nikishiriki katika nafasi mbalimbali za ndani ya chama, nakuhakikishia kama kuna chama kinasigina katiba basi CHADEMA ni namba moja…kumbuka namna mbowe na wenzake walivyokinyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ili kimpe yeye nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kudumu, na kumbuka siku tu niliyoanza kuhoji kuhusu hilo nilivyofurumushwa kama kuku pori’’. Anaongeza Mwigamba huku akicheka

Mwigamba anaendele kusema kuwa mara baada ya mbowe kuchukua kijiti cha uenyekiti wa chama hicho alijidhatiti kuhakikisha chama hicho kinakuwa na agenda ya kuisimamia ili kipate kuaminiwa na wananchi na hatimaye kupewa dola jambo ambalo chadema ilifanikiwa kwa kujitanabaisha wazi kuwa wao ni watetezi wa rasilimali za nchi na wapinga ubadhilifu na ain azote za ufisadi.

anasema aliwahi kusimuliwa kisa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kuhusu chanzo chama hicho kushikilia ajenda ya kupiga vita ufisadi ambapon alimwambia kuwa mwaka 2004 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti taifa alialikwa kwenye mikutano mikuu ya vyama vya Republican na Democrats vya Marekani alipokutana na Mwanasheria Kivuli aliyetokana na chama cha Democrats wakati huo Republican ikiwa inaongoza nchi chini ya Rais George Bush na mwanasheria huyo kumweleza Mbowe kwamba haijalishi chama kina sera nzuri kiasi gani, lazima kiaminiwe na wananchi.

samson-mwigamba.jpg

Samson Mwigamba siku alipojiunga CCM.

Aidha mwigamba anasimulia zaidi kuwa mwanasheria huyo alimweleza mbowe kwamba ameishi Tanzania kwa vipindi tofauti na katika kufanya kazi zake na utafiti aligundua kwamba nchi ilikuwa inapoteza pesa nyingi kupitia ufisadi na kumwambia Mbowe kwamba kama nchi ikifanikiwa kuzuia pesa zinazopotea kwa ufisadi, haitahitaji tena kuwa na bajeti tegemezi kwa mataifa ya nje na kumshauri kuangalia vitabu vya taarifa za Mdhibiti na MKaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anazozitoa kila mwaka ataona pesa nyingi zinavyopotea na huo ndio ukawa mwanzo wa Mbowe wakati huo akiwa mbunge wa Hai, kuanza kuzunguka mikoani akiambatana na wabunge wengine wa CHADEMA ya wakati huo ambao ni Marehemu Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Dr. Willibrod Slaa (Karatu), Dr. Amani Walid Kabourou (Kigoma mjini) na Grace Kiwelu (Viti maalum) kuelezea mapungufu waliyoyaona wakiwa na ripoti za CAG wakiwaeleza wananchi jinsi ufisadi ulivyokuwa unatafuta mabilioni ya pesa za watanzania maskini.

‘’Huo ndio ukawa mwanzo wa CHADEMA kushikilia ajenda hiyo ya ufisadi mpaka wakaingia nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo Mbowe aligombea urais na kushindwa na Jakaya Kikwete lakini wakapata wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa viti maalum. Ni uchaguzi huo ndio uliowaleta bungeni akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na wenzao na hoja ya ufisadi ikawa ni hoja hasa’’. Anaendelea Mwigamba

Mwigamba anasema kuwa Mbowe alimwambia kwamba waliamua kwenye kamati kuu kwamba kabla ya wabunge wao hawajaenda bungeni, chama kiwe kimefanya utafiti na kuvumbua madudu ya ufisadi ili wanapoenda bungeni wayasimamie hayo na ndio zama zilizoibuka kashfa ambazo majina yake yamebaki kwenye kumbukumbu za watanzania kashfa kama za Meremeta, Deep Green, EPA, Richmond, Buzwagi, na nyinginezo

“Ajenda hiyo ikaipelekea CHADEMA kuwa maarufu sana nchini kiasi cha uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa akagombea urais na kuchuana vikali na Kikwete.

Ingawa hakushinda, chama kilichupa kutoka wabunge watano wa majimbo mpaka 23 na baadaye 24, na kutoka wabunge 6 wa viti maalum mpaka 25. Chama kikawa maarufu kiasi cha kufikiriwa kuingia madarakani mwaka 2015.

Mbowe alirudia kunihadithia kisa cha huyo mwanasheria kivuli wa kimarekani mara pili tukiwa Karatu mwaka 2012 akitamba juu ya kuutumia vizuri ushauri wa mwanasheria huyo”, anasema Mwigamba.

Mwigamba anasema kwa kipindi kirefu chama hicho kilifanikiwa kujijengea sura ya kuwa watetezi wa Rasilimali za nchi na waoinga ufisadi wakiwa nje lakini wanapokuwa ndani ya chama wanakuwa na madudu makubwa hasa yanayohusu matumizi ya fedha hasa zinazotokana na ruzuku na hivyo kusababisha mitafaruku mikubwa miongoni mwa wananchama na viongozi wao kama ile iliyowahusisha Mbowe na Marehem Chacha Wangwe, na huu wa karibuni baina ya Mbowe na Zitto kabwe ulioishia kwa Zitto kufukuzwa uanachama na hatimaye kutimkia ACT WAZALENDO

“Lakini ndugu mwandishi hebu rejea mwaka 2013 uone Mbowe alivyofanya juhudi kubwa kuvuruga chama kwa matayarisho ya kuja kumpokea yule waliyempachika nembo ya ufisadi. Walianza na Zitto, Kitila na mimi wakamalizia kwa Slaa 2015 na gia ikawa imebadilishiwa angani.

Muulize leo Mbowe kuhusu ushauri wa yule mmarekani na wapi wameipotezea ajenda yao ya ufisadi mpaka wananchi wanakosa Imani na chama chao, atakuambia alibadilisha gia angani’’. anasema

‘’alibadilisha gia angani akamchukua Lowassa ambaye Lema alisema kumzomea fisadi kama Lowassa ni heshima kwa Mungu, Msigwa akasema anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili, Lissu akasema CCM wamempa fomu ya kugombea urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani.

Leo Nyalandu anaenda kujiunga na chama cha kubadilishia gia angani!!!? ameshajua Mbowe 2020 akibadilisha gia angani ataelekeza wapi chama?” anahoji Mwigamba huku akicheka kwa utani.
‘’huwezi kuwaelewa chadema kama ni popo au ndege, mchana wanasimamia hili, jioni lile basi ilimradi tu…hebu ona mbowe alivyokuwa anasema Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA…leo amebanwa nayeye kwenye madili yake amegeuka anasema Magufuli dikteta/…hakuna Dikteta katika siasa za Tanzania kumzidi Mbowe nakuambia mimi, chadema wanalijua hilo na UKAWA halikadharika’’.

‘’akigeuka huku anaona waliojihusisha na ufisadi wanapukutishwa kutoka serikalini, akigeuka anaona utumishi wa umma unavyorejea kwenye uadilifu na uchapakazi, miradi ya maji inatekelezwa hata iliyolala kwa miaka, miradi ya barabara za juu iliyohubiriwa kwa miaka inaanza, reli ya standard gauge iliyoishia kusemwa midomoni kwa karne inanyanyuka, miradi ya umeme, nk, akaona hapo hana jinsi, akasema rais anatekeleza ilani ya CHADEMA’’.

Anaendelea Mwigamba
‘’ Mbowe na CHADEMA yake walipoona rais anawashughulikia mpaka wale waliowachangia wao pesa za kampeni na hatimaye kumgusa Mbowe mwenyewe kwa ufisadi mkubwa aliolifanyia shirika la nyumba la taifa kwa makumi ya miaka, hali yao ikawa ngumu vijana wa mtaani wanasema siku hizi vyuma vikakaza, wakaanza kusema rais anavunja sheria na hatimaye wakaibuka na udikteta’’. Mwigamba anaongeza

Tukio jingine alilolibainisha Mwigamba ni la Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye.

’’ Ni Sumaye huyu huyu aliyeshambuliwa sana na Mbowe na CHADEMA yake miaka ya 2000 pale wafanyabiashara wasio wana CCM walipolalamika kunyanyaswa na mamlaka ya serikali hususani TRA.

Sumaye akaibuka na kusema,…. Kama mfanyabiashara unataka mambo yako yakunyookee, tundika bendera ya CCM kwenye biashara yako….

Walimtukana Sumaye kila matusi na kuonyesha anavyotumia vibaya madaraka ya uwaziri mkuu lakini leo Sumaye ni nguzo kuu kwenye CHADEMA’’.

‘’Hauwezi kuwa na akili timamu halafu uwaamini chadema si unakumbuka Kwenye uchaguzi wa 2015 kimsingi Sumaye ndiye alikuwa mpiga zumari mkuu na sasa ni mmoja wa watu wanaopigiwa upatu ndani ya CHADEMA kugombea urais 2020 mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote lakini anayeongoza kwa kukosa alama hata moja aliyoiacha eti leo agombee urais!!!? Hiyo ndiyo CHADEMA’’. Anazidi kueleza

IMG-20150727-WA0027.jpg


“Mtazame hata huyuNyalandu mwenyewe. Angalia clip ya video ya Joshua Nassari bungeni, angalia tweets za Mch. Msigwa na Halima Mdee.

Hivi hawaoni hata aibu mtu ambaye haijapita hata miaka mitatu tangu mmwite majina ya kila aina (mshika makalio ya mabinti askari wa wanyamapori, mtalii wa kutumbua kodi za watanzania na wasanii Marekani, fisadi wa hati za rais za uwindaji, nk) leo mnamwita kamanda, jembe, mara dume, mmh!”
Mwigamba anawapa pole sana wale wote wanaokimbilia CHADEMA na wale wanaojiandaa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.

''Kama ni mafisadi waende maana kwenye seerikali ya Magufuli hamna namna ya fisadi kusurvive. Ni sawa na kumwambia mwenye dhambi asurvive mbele ya nuru ya Mwenyezi Mungu.

Haiwezekani. Wa namna hiyo watangulie tu CHADEMA ndiko kwenye ngome mpya ya mafisadi. Lakini wale walio waadilifu wanaodhani kule ni kimbilio, wamuulize Dr. Slaa atawasimulia vizuri zaidi.

CHADEMA mchana unaweza kuwaona malaika safi toka mbinguni na usiku ukakuta ni mashetani wenye mapembe kabisa!''. alimalizia
 
Nyalandu amehama.vyama vingapi so far na mimi nimeongelea Mwigamba kahama vyama vingapi? Umemsikia Nyalandu akipayuka kuhusu CCM?

Tumia akili hata kama uliyonayo ni ndogo.
Ukiwa unadai demokrasia ukumbuke demokrasia inaruhusu mtu yeyote kua chama chochote na kutoka muda wowote kwenda chama chochote au demokrasia mnayotaka ni ya kuanika ujinga wenu mitandaoni??
 
Mwigamba njaa ni mbaya sana ndugu yangu. Ulikuwa m1 wa watu walionishawishi kuipenda Chadema kwa makala zako za Kalamu ya mwigamba. Ila pale ulipotaka kuanzisha uasi wewe na wenzako kina Heavy kabwe na Kitila Mkumbo ndio ukawa mwisho wako.

Hutamsahau ben wa saa8.
 
Bosala Bokungu
Mwigamba mm ni mwanaccm ila jibu ni hili jitahidi kuweka akiba ya maneno na hili ni andishi la pili nakujibu.
Ninaamini bila chadema usingefika ulipo kwa sasa kwani ktk lile kundi lenu mm mlilokuwa mmeliasisi ndani ya chadema mpaka Act mara uko ktk chama changu karibu lakini najua ulikuwa wakala wetu hata hiyo mm ilikuwa faida kwetu sasa ndio umefika au safari bado imo.
Jitahidi kusifu Mbowe kwani alikutengeneza kwani alikupokea na akakutengeneza aliye kutengeneza msifu tuu sio kwa ujinga kumbuka ni Mwenyekiti bora Tanzania kwa Afrika Viongozi kama yy ni wachache kwani ni mpenda Diplomasia.
 

Similar Discussions

16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom