Samia: Tanzania tunamuunga mkono Museveni kuimarisha usalama Maziwa Makuu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kumuunga mkono Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, katika juhudi za kuimarisha amani na usalama katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu, kufuatia nafasi yake kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Rais Samia amesema hayo leo Jumamosi, Februari 7, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Rais Museveni, Ikulu ya Dar es Salaam.

"Rais Museveni sasa hivi ni mwenyekiti wa nchi za Maziwa Makuu ana mkakati wa kuanza mazungumzo ya kuleta usalama ndani ya Maziwa Makuu, na sisi Tanzania tumemwambia tunamuunga mkono na tuko tayari kumsaidia atakavyoona inafaa katika jambo hilo," amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana kikamilifu na nchi wanachama wa ukanda wa Maziwa Makuu katika kuhakikisha kunakuwepo na utulivu wa kudumu, akibainisha kuwa amani ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za eneo hilo.

Your browser is not able to display this video.
 
tarehe 29 october 2025 kuna askari wa kiganda walikuwa wanauwa watu kama kuku.....leo ndio nimefahamu maana yake
 
Rais wa kugandisha😂
 
Tz na Uganda wote tunarukaruka tu. Charity begins at home,tupo waongo waongo tu..
 
 
Kagame na Tsishekedi wameona ni porojo tu zinaendelea wakeenda kupatanishwa na Trump, na bado hawajapatana kinawaka, ndio itakuwa haya majizi ya kura yawapatinishe?
 
Wale mapolisi wa humu humu nchini, hakuna askari kutoka nchi yoyote aliyeshiriki kwenye kadhia ile.
Hapa Mwanza walikuwepo polisi wa Uganda na walishiri kuua watu kwa risasi na baadhi yao walikuja kuuwawa na wanajeshi wa JWTZ. Usitetee ujinga watu bado tuna machungu maiti za ndugu zetu hadi leo hatujazipata.
 
Hapa Mwanza walikuwepo polisi wa Uganda na walishiri kuua watu kwa risasi na baadhi yao walikuja kuuwawa na wanajeshi wa JWTZ. Usitetee ujinga watu bado tuna machungu maiti za ndugu zetu hadi leo hatujazipata.
Mkuu hakuna mwanajeshi kutoka nje ya nchi, walitoka hapo Ngerengere kikosi maalum wakasambazwa nchi nzima.

Shughuli ya uchaguzi ilituhusu sisi watanzania, waliotuliza ghasia ni polisi wa kikosi maalum hawana shughuli miaka na miaka.

Sitetei ujinga nakwambia kitu ninachokifahamu vizuri. Poleni kwa kupoteza ndugu zenu.
 
Ndege wafananao huruka pamoja!

Huyu M17 angeifanya Uganda Monarchy tu, mambo yasiwe mengi!
Imagine from 1986 hadi leo?
TUnajifunza nn hapa?
 
Kagame na Tsishekedi wameona ni porojo tu zinaendelea wakeenda kupatanishwa na Trump, na bado hawajapatana kinawaka, ndio itakuwa haya majizi ya kura yawapatinishe?
Hiyo jumuiya ya maziwa makuu ilishashindwa kitambo kutatua mizozo ya hii Kanda.
 
Usalama maziwa mkuu ???

Duuuh, Congo vipi ?

Mengine ngoja ninyamaze.
 
Aseme yeye na genge lake wanamuunga mkono m7!

M7 hapaswi kuigwa kwa tabia zake ziliokosa utu!
Rais wa milele wa falme ya Uganda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…