Samia: Tanzania tunamuunga mkono Museveni kuimarisha usalama Maziwa Makuu

Samia: Tanzania tunamuunga mkono Museveni kuimarisha usalama Maziwa Makuu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kumuunga mkono Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, katika juhudi za kuimarisha amani na usalama katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu, kufuatia nafasi yake kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Rais Samia amesema hayo leo Jumamosi, Februari 7, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Rais Museveni, Ikulu ya Dar es Salaam.

"Rais Museveni sasa hivi ni mwenyekiti wa nchi za Maziwa Makuu ana mkakati wa kuanza mazungumzo ya kuleta usalama ndani ya Maziwa Makuu, na sisi Tanzania tumemwambia tunamuunga mkono na tuko tayari kumsaidia atakavyoona inafaa katika jambo hilo," amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana kikamilifu na nchi wanachama wa ukanda wa Maziwa Makuu katika kuhakikisha kunakuwepo na utulivu wa kudumu, akibainisha kuwa amani ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za eneo hilo.

Comments kama hizi ndizo zinazowaudhi Watanganyika.For Gods' sake how can you side with an evil man like Museveni.Very disgusting indeed.Yeah nimeamini kuwa ndege wanaofanana ndio wanaoruka pamoja.
 
Back
Top Bottom