Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania


Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15/10/2020 amewambia wakazi wa Chunya mkoani Mbeya kuwa wasipige kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata wakipiga kwingine Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.

Amesisitiza kuwa watashinda vikubwa sana Tanzania, na amefananisha kupigia kura kwa chama kingine kama kitendo cha kumwaga sukari Ziwa Viktoria na kutegemea maji yatakuwa matamu, ambacho ni sawa na kupoteza sukari yako.

Mh. Samia amesisitiza kuwa maendeleo watakayoyaleta sio kwa wana CCM peke yake na wale ambao hawatokipigia Chama Cha Mapinduzi basi kura yao itawasuta pale watakapokuwa wanaletewa maendeleo.
Ukitaka kuijua tabia ya mtu, subiri apate hela au nafasi.
Hivi sasa amepata mafasi ndiyo tunaiona tabia yake halisi. Kumbe ni tofauti kabisa na huyu aliekua akiongoa hapa. Kumbe ni mtu asiyependa dhurma, kumbe ni mpenda amani ma Suluhu, kumbe jina la Suluhu lilikua na maana kubwa sana kwa nchi yetu.
Aache tu kuwavumilia hadi yale makundi ya kitapeli yaliyopo kwenye baraza lake la mawaziri
 
Back
Top Bottom