saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 604
- 1,410
TAFAKURI YA KAULI YA RAIS MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIKWETE ALIYOITOA KWENYE MKUTANO MKUU WA 10 WA CHAMA CHA MAPINDUZI 8/12/2022 DODOMA
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amemtaka Mh. Rais Samia Suluhu Hassan asisikilize porojo zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa kuna mawaziri wanaokwenda nje ya nchi kukopa na kutafuta fedha za kumng’oa Rais Samia mwaka 2025, Mh. Kikwete amekanusha kwamba maneno hayo sio ya kweli na ni uongo na upuuzi mtupu.
1. Ninaona kama Mh Kikwete anajaribu kutaka kumfundisha kazi Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi namna ya kushughulikia matatizo ndani chama. Rais aliyeko madarakani anavyo vyombo vyote vya uchunguzi vyenye kuweza kubainisha ukweli au uongo wa kauli ya Mheshimiwa Albert Chalamila juu ya mawaziri kwenda nje ya nchi kukopa matrilioni ya fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2025 na kuchukua hatua stahiki.
2. Nchi yetu inavyo vyombo vya dola kama Usalama wa Taifa, TAKUKURU, Jeshi la Polisi, CAG nk. ambavyo vimepewa mamlaka kisheria kufanya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali na kubaini ukweli wake. Mh Kikwete yeye ni nani hadi atoe taarifa za kiuchunguzi mbele ya umma na kwa Mh Rais kuhusiana na mawaziri kwenda kukopa nje na kujiimarisha kuelekea 2025
3. JK ni mstaafu hana cheo chochote serikalini wala kwenye Chama anajuaje kama hadi sasa hatua hazijachukuliwa kwa Mh. Albert Chalamila juu ya kauli yake kuhusiana na mawaziri
4. Ni kwanini JK ameelekezea lawama nzito upande mmoja tu wa mtoa kauli Mh Albert Chalamila hadi kuagiza achukuliwe hatua na Chama na sio wale waliotajwa na RC Chalamila kuhusika na njama za kumhujumu Rais aliyeko madakarani
5. Je Mheshimiwa Mstaafu Jakaya Kikwete kwanini atumie nguvu kubwa kukanusha kuwepo kwa mawaziri wanao tafuta fedha na mikopo nje ya nchi kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka 2025 na kumbwaga Rais aliyeko madarakani Mama yetu Samia Suluhu Hassan.
Kwa vyovyote vile mawaziri waliotajwa na Chalamila, Mzee Kikwete atakuwa anawajua kwa majina na wizara wanazoziongoza ni washirika wake katika kupanga njama za kumtoa Rais Samia 2025 ndio maana povu jingi likamtoka kuwatetea hadharani bila aibu.
6. Rais Mstaafu Kikwete anamwambia Rais Samia kwamba kwenye utawala wake hakukubali upuuzi huo, Lakini watanzania wote tunakumbuka nchi alivyoitumbukiza kwenye matatizo mengi kama uendeshaji duni wa chama na Serikali mpaka ikafikia hatua hatua ya KUJIVUA GAMBA ili kuinusuru CCM, mikataba mibovu kama Richmond, IPTL, Bandari ya Bagamoyo na Escrow mbayo ilisababisha hasara kubwa kwa nchi yetu lakini pia tunakumbuka bandari ya Dar es Salaam JK alivyoikabidhi kwa GSM hadi kusababisha mfarakano mkubwa na wafanyabiashara hadi watu kumwagiwa tindikali. leo Mzee Kikwete anapata wapi kiburi cha kutamka hayo hadharani kwamba jkwenye utawala wake hakukubali upuuzi huo.
7. Kwanini Rais JK badala ya kumuombea mema Rais wetu yeye anamtabiria mabaya kwa kauli yake eti labda mambo yaharibike sana kuanzia sasa na wakati huo ndio anaweza kujitokeza mwana CCM mwingine kugombea urais. Rais wetu anaongoza nchi vizuri na analeta maendeleo kwa kasi, je hayo mambo anayotarajia yaharibike ni yapi na kwaninji hakuyataja?
8. Tunaomba Mh Jakaya Mrisho Kikwete amuache Mama yetu Samia Suluhu Hassan aendelee kuiongoza nchi nchi yetu kwa misingi ya haki bila ubaguzi wala udini.
9. Endapo JK analo jambo la kushauri alipeleke kwa utaratibu unaofahamika na Mama atalipokea kwa kuwa Mama yetu ni msikivu na mnyenyekevu tofauti na yeye JK ambaye wakati wa utawala wake aliwafukuza marais wastaafu Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ili afanye maamuzi atakavyo.