GE2025 Samia: Nitasambaza umeme Tanzania yote

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
971
Reaction score
1,945
Hii hadithi tumeisikia kuanzia Nchi imepata Uhuru. Najiuliza umeme utakasambazwa nchi nzima ndo huu huu unaokatika kila baada ya masaa nane au?

My take suala sio kusambaza umeme swali ni huo umeme unaosambazwa utaweza kukidhi mahitaji ya Watanzania nchi nzima na utakuwa reliable?
=======================

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa nishati ya umeme itasambazwa katika maeneo yote ili wananchi kupata huduma hiyo kwa uhakika zaidi.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumanne Septemba 9,2025 akiwahutubia wananchi wa Manyoni mkoani Singida katika mwendelezo wa kampeni zake za kusaka kura za urais, akiwa siku ya kwanza mkoani humo.

“Kama kuna vitongoji ambavyo havijapata umeme, tutakwenda kuisambaza nishati hii Tanzania yote,” amesema Dkt Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Manyoni waliofuruka kumsikiliza. Kwa asilimia kubwa Serikali imefanikiwa kufikisha umeme karibu vijiji vyote nchini na hivi sasa wapo katika mchakato wa kumaliza vitongoji.

Katika hatua nyingine, huku akiendelea kushangiliwa na wananchi wa Manyoni, Dkt Samia amewaahidi wakazi wa Singida kuboresha sekta za elimu, afya na maji ili kuhakikisha wanazipata huduma hizo kwa ufanisi zaidi. “Kadri idadi ya watu inavyongezeka na ndivyo mahitaji yanyavyokuwa, mkitupa ridhaa tutahakikisha tunawatumikia watu ikiwemo kupata huduma bora za afya.

“Tulisema tutaanza na bima ya afya kwa wote kwa majaribio ndani ya siku 100, mkitupa kura zenu.Tutaangalia mwenendo unakwendaje, ukiende vizuri tutafungua nchi nzima, nani kama CCM,” aliuliza Dkt Samia huku akiitikiwa na ‘hakuna…’
 
IMG-20250909-WA0070.jpg
IMG-20250905-WA0041.jpg
 
Umeme kusambazwa nchi nzima upo kwenye mpango wa REA. Hata angeshinda kilaza mwingine yeyote yule kwenye wale vilaza 17, bado huo umeme ungesambazwa tu.
 
Dah.. kwahiyo kuwa au kutokuwa na umeme ni matakwa ya chama cha siasa, sio mipango ya nchi ambayo haitegemei siasa za majukwaani.
 
FOH!

Zaidi ya miaka 60 madarakani hamjaweza!

Incompetent nincompoops.
 
Na ile koswa koswa ya kutaka kumpa ADANI Dili ili awasambazie vipi imewekwa Pause au itafufuliwa watu wapige Bakshishi zao ?
 
Hii hadithi tumeisikia kuanzia Nchi imepata Uhuru. Najiuliza umeme utakasambazwa nchi nzima ndo huu huu unaokatika kila baada ya masaa nane au?

My take suala sio kusambaza umeme swali ni huo umeme unaosambazwa utaweza kukidhi mahitaji ya Watanzania nchi nzima na utakuwa reliable?
=======================

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa nishati ya umeme itasambazwa katika maeneo yote ili wananchi kupata huduma hiyo kwa uhakika zaidi.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumanne Septemba 9,2025 akiwahutubia wananchi wa Manyoni mkoani Singida katika mwendelezo wa kampeni zake za kusaka kura za urais, akiwa siku ya kwanza mkoani humo.

“Kama kuna vitongoji ambavyo havijapata umeme, tutakwenda kuisambaza nishati hii Tanzania yote,” amesema Dkt Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Manyoni waliofuruka kumsikiliza. Kwa asilimia kubwa Serikali imefanikiwa kufikisha umeme karibu vijiji vyote nchini na hivi sasa wapo katika mchakato wa kumaliza vitongoji.

Katika hatua nyingine, huku akiendelea kushangiliwa na wananchi wa Manyoni, Dkt Samia amewaahidi wakazi wa Singida kuboresha sekta za elimu, afya na maji ili kuhakikisha wanazipata huduma hizo kwa ufanisi zaidi. “Kadri idadi ya watu inavyongezeka na ndivyo mahitaji yanyavyokuwa, mkitupa ridhaa tutahakikisha tunawatumikia watu ikiwemo kupata huduma bora za afya.

“Tulisema tutaanza na bima ya afya kwa wote kwa majaribio ndani ya siku 100, mkitupa kura zenu.Tutaangalia mwenendo unakwendaje, ukiende vizuri tutafungua nchi nzima, nani kama CCM,” aliuliza Dkt Samia huku akiitikiwa na ‘hakuna…’
Asilimia 35 ya watanzania wote ndiyo wanatumia umeme, Asilimia 65, hawana umeme wanalala giza, wanapikia kuni na wanaishi maisha ya umaskini sana. LEO ANASEMA ATAPELEKA UMEME TANZANIA NZIMA, JE ALIKUWA WAPI MIAKA 10 ILIYOPITA AKIWA MAKAMO WA RAIS NA RAIS? Aache kutudanganya huyo mama, Huyo ni muongo tangu kuzaliwa, tatizo tunaongozwa na wamama wa mtaani.......wacheza ngoma.
 
Nani kakwamhia tunahitaji umeme? Sisi tunaitaka Tanganyika yetu na tutaipata tu.
 
Umeme kusambazwa nchi nzima upo kwenye mpango wa REA. Hata angeshinda kilaza mwingine yeyote yule kwenye wale vilaza 17, bado huo umeme ungesambazwa tu.
Eti jamani mbona hili liko bayana haihitaji siasa kila raia anatambua REA ipo kufanya majukumu hayo haijalishi nani kashinda waache siasa nyepesi ahadi lukuki. Miundombinu hasa ya barabara sehemu nyingi kwa sasa haiko vizuri kwa wanaosafiri kwa barabara mashahidi wa hili njia ziko taabani Tanroads nao hoi wako hawalipi wakandarasi inavyistahili mpaka wakandarasi wameacha kuomba kazi zao.
 
Hii hadithi tumeisikia kuanzia Nchi imepata Uhuru. Najiuliza umeme utakasambazwa nchi nzima ndo huu huu unaokatika kila baada ya masaa nane au?

My take suala sio kusambaza umeme swali ni huo umeme unaosambazwa utaweza kukidhi mahitaji ya Watanzania nchi nzima na utakuwa reliable?
=======================

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa nishati ya umeme itasambazwa katika maeneo yote ili wananchi kupata huduma hiyo kwa uhakika zaidi.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumanne Septemba 9,2025 akiwahutubia wananchi wa Manyoni mkoani Singida katika mwendelezo wa kampeni zake za kusaka kura za urais, akiwa siku ya kwanza mkoani humo.

“Kama kuna vitongoji ambavyo havijapata umeme, tutakwenda kuisambaza nishati hii Tanzania yote,” amesema Dkt Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Manyoni waliofuruka kumsikiliza. Kwa asilimia kubwa Serikali imefanikiwa kufikisha umeme karibu vijiji vyote nchini na hivi sasa wapo katika mchakato wa kumaliza vitongoji.

Katika hatua nyingine, huku akiendelea kushangiliwa na wananchi wa Manyoni, Dkt Samia amewaahidi wakazi wa Singida kuboresha sekta za elimu, afya na maji ili kuhakikisha wanazipata huduma hizo kwa ufanisi zaidi. “Kadri idadi ya watu inavyongezeka na ndivyo mahitaji yanyavyokuwa, mkitupa ridhaa tutahakikisha tunawatumikia watu ikiwemo kupata huduma bora za afya.

“Tulisema tutaanza na bima ya afya kwa wote kwa majaribio ndani ya siku 100, mkitupa kura zenu.Tutaangalia mwenendo unakwendaje, ukiende vizuri tutafungua nchi nzima, nani kama CCM,” aliuliza Dkt Samia huku akiitikiwa na ‘hakuna…’
Yan huyu Bi.Chura Kiziwi dah😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom