Samia Complex Kujengwa Ndani ya Ikulu ya Chamwino Dodoma

Samia Complex Kujengwa Ndani ya Ikulu ya Chamwino Dodoma

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
82,312
Reaction score
88,342
Ikulu haijakamilika ujenzi unaendelea,this time around ni Samia Complex

=====
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma leo amesema baada ya kukamilika kwa Ikulu sasa wanatarajia kujenga jengo la kisasa (Samia Complex) ndani ya eneo hilo kubwa la Ikulu lenye Ekari 8473 na tayari michoro ipo tayari ambapo kwa sasa wanahangaika kutafuta fedha ili ujenzi uanze.

Rais Dkt. Samia amesema “Eneo hili bado kuna kazi ya kufanya na hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la kisasa ambalo Wasaidizi wangu wameliita Samia Complex ambalo litakuwa na ukumbi wa mikutano wa Watu Elfu mbili mpaka Elfu tatu, nyumba za Viongozi hasa Majirani zetu wa EAC na SADC kutakuwa na Zanzibar Lounge, East Africa Lounge, uwanja wa golf, viwanja vya michezo, njia za ndege na sehemu za historia za Viongozi wa Nchi zetu”

My Take
Ilifaa pia kuwe na Serengeti, Ngorongoro Lounge na Kilimanjaro Lounge
 
Kweli remote ipo msoga.amemshauri auite jina lake kama alivyofanya yeye ule wa magogoni kuitwa jina lake.pesa ni zetu lakini mnajipachika majina yenu pasipokutuuliza sisi wananchi.kwa nini usiitwe ukumbi wa ikulu?
 
Nani Alimshauri Jiwe aite Mji wa Serikali Mtumba Magufuli City?
Chuki na wivu ,Je hapo ingeitwa Kikwete ingekuaje? 😁😁

Nenda ukafute basi jina likiandikwa 😂😂
 
Back
Top Bottom