Samia Complex Kujengwa Ndani ya Ikulu ya Chamwino Dodoma

Fitna Zimeshapigwa Pale Bango Wanelitoa Sasa Hivi Inajulikana Mji Wa Serikali Mtumba
Siyo Tena Mzilankende City Kama Mwanzo
Basi wangemjengea Lounge humo ndani,hata Mimi sikupenda kuita Magufuli City ibakie Mtumba..
 
Zanzibar lounge kwenye ikulu ya Tanganyika??

Haya basi endeleeni na mafutari yenu mpaka 2030 , mtupishe.
 
Kweli remote ipo msoga.amemshauri auite jina lake kama alivyofanya yeye ule wa magogoni kuitwa jina lake.pesa ni zetu lakini mnajipachika majina yenu pasipokutuuliza sisi wananchi.kwa nini usiitwe ukumbi wa ikulu?
Sioni ubaya wowote Kama ikulu itaitwa ikulu ya Magufuli halafu Samia Complex.

RIP JPM jemedari na jabali la Tanzania. Tutaziishi fikra zako kwa Yale mazuri uliyoyasimamia na tutaendelea kukemea yeyote atakaetaka kunyonga demokrasia Kama ilivyokuwa wkt wa utawala wako baba.
 
Ikulu haijakamilika ujenzi unaendelea,this time around ni Samia Complex

=====
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma leo amesema baada ya kukamilika kwa Ikulu sasa wanatarajia kujenga jengo la kisasa (Samia Complex) ndani ya eneo hilo kubwa la Ikulu lenye Ekari 8473 na tayari michoro ipo tayari ambapo kwa sasa wanahangaika kutafuta fedha ili ujenzi uanze.

Rais Dkt. Samia amesema “Eneo hili bado kuna kazi ya kufanya na hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la kisasa ambalo Wasaidizi wangu wameliita Samia Complex ambalo litakuwa na ukumbi wa mikutano wa Watu Elfu mbili mpaka Elfu tatu, nyumba za Viongozi hasa Majirani zetu wa EAC na SADC kutakuwa na Zanzibar Lounge, East Africa Lounge, uwanja wa golf, viwanja vya michezo, njia za ndege na sehemu za historia za Viongozi wa Nchi zetu”

My Take
Ilifaa pia kuwe na Serengeti, Ngorongoro Lounge na Kilimanjaro Lounge
Mambo haya tuyaache kwanza twende na moja moja kwanza
 
Sioni ubaya wowote Kama ikulu itaitwa ikulu ya Magufuli halafu Samia Complex.

RIP JPM jemedari na jabali la Tanzania. Tutaziishi fikra zako kwa Yale mazuri uliyoyasimamia na tutaendelea kukemea yeyote atakaetaka kunyonga demokrasia Kama ilivyokuwa wkt wa utawala wako baba.
Ikulu haiwezi itwa jina la mtu binafsi hata siku Moja
 
Sina tatizo sana na ujenzi ukiwa umelenga kuboresha mambo, nina tatizo kubwa mnoo na hilo jina la Samia complex. Huku ni kulazimisha legacy kwa kujipendelea. Hayo majina wapewe viongozi waliokufa na waliobeba hayo maono.
Itakuwa hujui hata hapo magogoni kuna kikwete Hall mbona hilo hamseme
 
..viongozi wetu ni WABINAFSI sana.

..Samia Complex ya nini wakati wananchi wana changamoto za kila aina.
 
Kwa hiyo Ikulu Isijengeke Kisa Changamoto Zako,Changamoto Zinatatuliwa Huku Ikulu Inajengwa,Watanganyika Acheni Ujuaji wa Mambo Kwa Hyo Mnataka Ikulu Iwe Kama Hall Tu Lazima Makao Ya Raisi Wetu Yavutie.
 
..kwani tangu tupate uhuru tulikuwa hatuna Ikulu?

..serikali lazima iwe na vipaumbele vinavyolenga wananchi badala ya kulenga viongozi wanaopenda anasa.
 
Ikulu haijakamilika ujenzi unaendelea,this time around ni Samia Complex

=====
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma leo amesema baada ya kukamilika kwa Ikulu sasa wanatarajia kujenga jengo la kisasa (Samia Complex) ndani ya eneo hilo kubwa la Ikulu lenye Ekari 8473 na tayari michoro ipo tayari ambapo kwa sasa wanahangaika kutafuta fedha ili ujenzi uanze.

Rais Dkt. Samia amesema “Eneo hili bado kuna kazi ya kufanya na hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la kisasa ambalo Wasaidizi wangu wameliita Samia Complex ambalo litakuwa na ukumbi wa mikutano wa Watu Elfu mbili mpaka Elfu tatu, nyumba za Viongozi hasa Majirani zetu wa EAC na SADC kutakuwa na Zanzibar Lounge, East Africa Lounge, uwanja wa golf, viwanja vya michezo, njia za ndege na sehemu za historia za Viongozi wa Nchi zetu”

My Take
Ilifaa pia kuwe na Serengeti, Ngorongoro Lounge na Kilimanjaro Lounge

Hilo jengo litachangia nini kwenye maendeleo ya nchi na ustawi wa watu wetu?
 
Back
Top Bottom