Samia au mtoto kwa kikwete walikuwa wana nafasi nzuri ya kushinda uraisi kwa haki sio kwa njia hii wanayoitumia

Samia au mtoto kwa kikwete walikuwa wana nafasi nzuri ya kushinda uraisi kwa haki sio kwa njia hii wanayoitumia

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
3,560
Reaction score
7,914
Katika uhalisia samia alianza vizuri na alikuwa na njia zote za kujenga akubalike kama raisi ambapo hata tungeweka tume huru angeshinda lakini amefanya makosa na amechagua njia mbaya inayomchafua kwenye sura za nchi na za kimataifa njia mbaya sana.

Mtoto wa raisi mstaafu kikwete pia alikuwa na nafasi nzuri ya kujenga siasa ili kuwania uraisi na ninaamini angeweza kumshinda hata Lissu, ila na yeye nasikia anatembea nyumba kwa nyumba kugawa fedha kupata urais anakosea sana nimesikia anagawa fedha nchi nzima.

Maswala haya yanatupa picha gani ? ni kwamba wao ni watu wenye uwezo mdogo sana. lakini pia njia waliyoichagua inaenda kuondoka na damu za watu, na wengine kupewa kesi za uongo, utekaji nyara, inaenda kuondoa haki na demokrasia vitu ambavyo ukiviangalia ni vitu vya kimbumbumbu

Wamechagua njia mbaya sana mimi naziita za kimbumbumbu, bado wana nafasi ya kufanya vizuri na kuanza upya hii njia ya sasa ni mbaya sana inaweza kuwagharimu.
 
Kama ni pesa wanayo
Kuna kitu gani cha ziada wanachokitafuta hawa watu?
 
Back
Top Bottom