Samaki kutoka Mwanza wasiooza wanawekwa nini?

Samaki kutoka Mwanza wasiooza wanawekwa nini?

KAKA NASOKI

Senior Member
Joined
May 25, 2016
Posts
191
Reaction score
212
Kuna samaki kutoka Mwanza pale Ukonga Mombasa, wanaletwa kwenye viroba na ukiwagusa sio baridi wa kuganda lakini wanakaa hata siku tatu bila kuoza, je samaki hawa wanawekwa nini kuzuia kuoza au ndio zile tetesi wanatumia dawa za hospitali zinazozuia kuoza (Formaline)?
anayejua anijuze
 
Samaki wasiooza siku tatu tena wakiwa nje ya friza...
Mchele wa plastic...
Mayai ya plastic...
Kuku wanaokua ndani ya wiki mbili na kuliwa...
Matunda yanayokuzwa na madawa hatarishi....
Bidhaa za viwandani zisizo na ukaguzi makinifu...

NDUGU ZANGU TWAFAAAAAA.NI MAREHEMU TUNAOTEMBEA ASEEEE.
 
Kuna samaki kutoka Mwanza pale Ukonga Mombasa, wanaletwa kwenye viroba na ukiwagusa sio baridi wa kuganda lakini wanakaa hata siku tatu bila kuoza, je samaki hawa wanawekwa nini kuzuia kuoza au ndio zile tetesi wanatumia dawa za hospitali zinazozuia kuoza (Formaline)?
anayejua anijuze
Dawa za maiti labda.
 
Wale samaki wanahifadhiwa kwa formalin ile dawa ya kuhifadhi maiti ndiyo maana hawaozi
 
Wale samaki wanahifadhiwa kwa formalin ile dawa ya kuhifadhi maiti ndiyo maana hawaozi
Jesus Christ, binadamu wamekuwa wauaji kwa kweli mpaka samaki wanawekewa formaline ? Maskini walaji pole kwao.
 
Hao samaki hawafai kwa matumizi ya kiumbe hai chochote! Hata mbwa wako usimpatie. Wauzaji si waaminifu, huwadunga dawa ya kuhifadhia maiti ili waweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

Ukitaka kuhakikisha hili, nunua samaki mmoja, peleka kwa mkemia mkuu kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi. Kamwe hauta nunua tena hao samaki.
 
Jaribu kuonja kama utaona test ya ajabu ajabu tuambie inaweza kuwa kweli wanaweka Formaline,ila huku kwetu Ubungo wanaletwa na ndege wakiwa fresh kila wiki,wakifika wanahifadhiwa kwenye mafriji na ukienda kununua unanunua kutoka kwenye hizo Friji akiwa ameganda barafu.
 
Muhimu kama wahusika wamo humu walishughulikie ipasavyo hilo tatizo,na pia uangaliwe upya utaratibu uliopo wa jinsi ya kupata hizo dawa za formaline,

hizo dawa ziwe zinapatikana mahospitalini tu na sio hovyo hovyo kama wanavyozipata kiurahisi hao wauza samaki kwa sasa.
 
Daah. Aisee binadamu wanalishwa vitu vya ajabu pasi wenyewe kujua na mpaka umegundua ni wengi sana ambao washajilia pasi kuwa na hofu ya aina yeyote.
 
Wafanyabiashara wengi ujali zaid kuhusu pesa na sio afya yako, ni umakini unatakiwa, ila kwa siku tatu bila kuooza kuna ulakini hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuu wanajali pesa na kusahau kwamba inawezekana katika hao walaji hata ndugu zao nao wanaweza wakawa wamo.

Ila hatua inahitaji kuchukuliwa aisee ili kupata ukweli wa kinachowekwa katika hao samaki.
 
Inasikitisha sana lakini naona watu wamekomalia samaki tu , niwakumbushe kuwa kuna vyakula vingi sana vinavyo kuwa injected na formaline, hususan vya kwenye masoko funge, hivyo tuwemakini na aina hizi za vyakula madhara yake ni makubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom