Samahani kwa Kuuliza hivi Daraja Jipya la Mto Wami limeshazinduliwa? Na kama bado ni Kwanini?

Ina maana huyu bibie hana vision ? Yeye kufubgua nchi na bakuli waarabu na uza uza rasilimali?
 
Kazi yangu Kubwa ni kusoma tu Comments zenu, ila popote pale ulipo Hayati John Pombe Magufuli Roho yako ilale mahala pema peponi. Amen.
Kwani wakati unaenda Lutindi, huwa unapita njia gani? Acha kuchosha watu hapa. Halafu ukumbuke hilo daraja limejengwa kwa fedha zilizotokana na kodi yako.
 
unadhani maendeleo yanapatikana huku ukibembeleza watu? Unataka ufanye miradi ya maendeleo huku unafanya anasa? Unataka uliridhishe kila mtu, utasimamiaje sheria? Utakusanya vipi kodi? Unakusanya wakuu wako wote wa wilaya na wewe mkuu wa mkoa kupeleka makusanyo ya hela za kusaidia watu Hanang, utafinance vipi maendeleo kwa spending culture ya namna hiyo? Hata wewe binafsi bila kua na roho mbaya, maendeleo sahau. All great nations on earth, had to take ruthless measure kua wakubwa hivyo.
Yawezekana ukawa una elekeza mtu wa miaka ya 2000 hajui nchi China, Japan, Vietnam n.k maendeleo yalikuja vipi? Tena mbaya zaidi kwa mwafrika eti umbembeleze hakuna maendeleo yatakayopatikana hadi mwisho wa dahari.
 
Kwani lisipozinduliwa inakuaje?
Inaonyesha ni jinsi gani tusivyotaka Mambo makubwa na mazuri ya Mwamba Hayati John Pombe Magufuli yaendelee Kujulikana na kila Siku azidi Kukumbukwa tofauti na Waigizaji Filamu wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
 
Tunapenda sana kila kitu sijui kuzindua sijui nini, je watu kwa sasa wanapita wapi ? Siyo kila kitu tuzoee kuzinduliwa wananchi tunataka kuona maendeleo na matatizo yetu yameisha au kutatuliwa hivo kama tayari linatumika ni vizuri maana limesaidia punguza ajali.
Sahihi, waswahili wanapenda shughuli sana.
Kwao hakuna jambo dogo.
 
Shida ya wananchi haikuwa kuzindua daraja bali kulitumia! Mwisho tenda wema usepe zako siyo unasubiri misifa kama shetani!
Hata sio kutenda wema,sio hisani hiyo.
Ni kuwajibika kodi za raia waliolipia hilo daraja na wanaokutunza kama kiongozi.
 
GENTAMYCINE nitakuwa maradufu yake.
Awapi. Ukitaka kuwajua Watz jaribu kuomba kazi hata ya kujitolea kwa Mtendaji wa Kijiji. Halafu uje hapa uniambie umeona nini.

Kwanza utagundua kwamba washawishi wakubwa wa rushwa ni wananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom