Sam Mahela tena... Hivi ITV management hamyaoni haya?

Sam Mahela tena... Hivi ITV management hamyaoni haya?

Huyu jamaa vipi jamani?! Nimefuatilia kipindi cha DK45 ITV na leo mgeni ni N/Waziri wa Muungano na Mazingira na mada ilikua ni Mazingira.

Huyu Sam Mahela, kama kawaida yake kuingilia mzungumzaji wakati anatiririka vizuri kwenye mada husika. Anageuka kuwa mzungumzaji Mkuu, anatoa maoni yake Mfano...."Mimi/sisi waandishi wa habari tumefanya tafiti na ni kweli/sio kweli kwamba Kuna uharibifu wa Mazingira".....sasa kama ulikua unajua ukweli/uongo wa jambo ya nini kumwaalika mgeni studioni wakati ulikua na misimamo yako kwenye topic husika?

Mfano alipokua akiagana na N/W huyo, akawa anamsisitiza"fanyakazi, umesikia, fanyakazii, umepewa kazi ufanye, sawa...maana hata mm hapa ITV napiga kazi".....hapa ni kiherehere tu cha huyu maana sio wajibu wake kumweleza hayo.

Nimekuwa nikifuatilia kipindi hiki Lakini watu wengi wanakereka sana na huyu jamaa.....atulie, atoe nafasi ya mgeni husika kusema na baada ya hapo maswali. Mwanzilishi wa kipindi hiki na Buholela walikua wazuri sana sio kama huyu kijana.

Mkuu uko sahihi.

Huyu jamaa anahiyo tabia mbaya ya kukatiza wageni wake wanapookuwa wanashusha points.

Nakumbuka siku alipokuwa na Mch. Msigwa. Sikupfurahia kabisa tabia yake hiyo mbaya. N hasa mtu anapotoa maoniyanayotofautia na serikali au kuikososa serikali.
Ajirekebishe.
 
Tatizo anakuwa kama anataka kumuiga mtangazaji fulani hivi hajiweki kama yeye inakuwa kama ana strugle kujiwekea identity yake kama yeye sasa anataka kuwa kama wale wajuu. Kuiga au kujifunza sio kubaya ila chukua vitu kidogo mwisho ubaki kama wewe. Be real. Kuhusu maswali ni wote tu Tz ni bado sana wakajifunze Hardtalk.
 
Semunyu alikua mzuri ukimlinganisha na hao wengine ila km hakua akijiamini sana.
Na uvaaji nao jamaa ilikua cheche,anaweza kukupigia kiatu cheupe kama yai la kienyeji na soksi vya njano
Hahahaha..mkuu ila hata buhohela alikiweza..ila huyu mahela ni kama anasifiwa na analewa sifa..
 
Tangu siku Sam Mahela alipombana Msigwa kwa maswali magumu ambayo msigwa alionekana kuhangaika vijana wa UKAWA hasa chadema mnamchukia sana Sam Mahela.
Hizi chuki zenu hazina msingi wowote acheni jamaa afanye kazi
 
Kweli yule sijui Simiyu sijue Semuyu alikuwa anajitahidi kidogo na Buhohela wa Ikulu.
Tatizo huyu Sam baada ya kuona mwenzake Buhohela kapewa shavu Ikulu basi anadhani na yeye kwenye Dakika 45 akiitetea Serikali basi ataitwa jumba jeupe.....Bure kabisaaaaaa

Anaingilia ingilia mahojiano,anauliza swali halafu anajijibu mwenyewe yaani ni vurugu tupuuuu....Hawa vijana wa Cameroon tabu tupu aseee.

Yule Simiyu mi alikuwa ananiacha hoi uvaaji wake...Utamkuta ana kiatu kirefu kama chopeo,yaani jamaa ana mguu hatari...juu anavaa tai ya kachumbari ndefuuuuu inafika magotini na suruali ya "selebresheni" kama mcheza show wa Madiluuu,huku shati over size kubwaaaaaa...Au koti la kushona kwa fundi Juma pale Mtaa wa Msisiri Kinondoni....Dressing Code ya Simiyu ilikuwa balaaaa!!Hata sijui yukwapi jamaaa!!
 
Semunyu alikua mzuri ukimlinganisha na hao wengine ila km hakua akijiamini sana.
Na uvaaji nao jamaa ilikua cheche,anaweza kukupigia kiatu cheupe kama yai la kienyeji na soksi vya njano
Hahahahahaha
 
Sio wote wanaomkosoa humu ni UKAWA....We mtie ujinga tu wakati wanaomtazama ndio wanaona muelekeo wa kipindi chake.....Yaani we Sam unafikiri unakosolewa sbb ya Msigwa??Kweli DSJ hampikiki
 
Kweli yule sijui Simiyu sijue Semuyu alikuwa anajitahidi kidogo na Buhohela wa Ikulu.
Tatizo huyu Sam baada ya kuona mwenzake Buhohela kapewa shavu Ikulu basi anadhani na yeye kwenye Dakika 45 akiitetea Serikali basi ataitwa jumba jeupe.....Bure kabisaaaaaa

Anaingilia ingilia mahojiano,anauliza swali halafu anajijibu mwenyewe yaani ni vurugu tupuuuu....Hawa vijana wa Cameroon tabu tupu aseee.

Yule Simiyu mi alikuwa ananiacha hoi uvaaji wake...Utamkuta ana kiatu kirefu kama chopeo,yaani jamaa ana mguu hatari...juu anavaa tai ya kachumbari ndefuuuuu inafika magotini na suruali ya "selebresheni" kama mcheza show wa Madiluuu,huku shati over size kubwaaaaaa...Au koti la kushona kwa fundi Juma pale Mtaa wa Msisiri Kinondoni....Dressing Code ya Simiyu ilikuwa balaaaa!!Hata sijui yukwapi jamaaa!!
Hahahahahaha nimecheka mno
 
Itv wajaribu kutumia reporters wao wa mikoani pia ktk kipindi chao hiki ila sio yule wa tabora au futuna
 
Ni kweli, Sam Mahela huwa nataka kmwiga Jerry, lakini placement ya maswali hajui. Sio vizuri kuuliza kisha unatoa sehehu ya jibu wewe mwenyewe, afu mgeni anaishia kusema ni kweli kama unavyosema ndugu mtangazaji. Sipendi hali hiyo, umemleta wa nini basi, si ungeandaa ripoti maalum ututaarifu ulichofanyia utafiti.

Ngoja nimpe sample ya maswali;

1. Mh waziri, Serikali imetekeleza sheria inayoelekeza kutunza vyanzo vya maji kwa kubomoa nyumba za watu hivi karibuni.

a) Watu kukosa makazi ni kinyume cha sheria ya haki za binadamu, nini maoni ya serikali?

b) Kukosa makazi kunafanya watu waichukie serikali unayoiongoza, umejipangaje kuhakikisha vyama vya upinzania havitumii mwanya huu kuwashinda kwenye uchaguzi ujao?

c) Kama serikali, hawa ni watu wenu, watarajie mtawafanyia nini kupunguza makali ya kubomolewa nyumba zao?

KILA SWALI MPE NAFASI ATIRIRIKE WATAZAMAJI WAMJAJI KAMA ANA MAJIBU AU VUMBI?
 
Mahela ajifunze kwa watangazaji wa majuu kama SHAKA SARI mganda wa Voice of America.
 
Semunyu alikua mzuri ukimlinganisha na hao wengine ila km hakua akijiamini sana.
Na uvaaji nao jamaa ilikua cheche,anaweza kukupigia kiatu cheupe kama yai la kienyeji na soksi vya njano
Hahahahaha,dah..ndio maana haonekani cku hizi?
 
Ni reporter mzuri ila sifa zimemjaa sana, kitu ambacho is not good na hakitamfikisha BBC au VOA hata kwa dawa IN CASE asipobadilika.

Halafu ukimchunguza vizuri utaona kabisa anamuiga sijui yule gabriel zakaria wa TBC ambaye huwa ana papara na sometimes anajifanya kama ana kigugumizi..mi siwaelewi hawa jamaa kabisa yaani mtangazaji una act una kigugumizi? ..kweli? Hii taaluma imevamiwa
 
Tatizo la Sam mahela anapritend hayupo real mizuka mingi wenge kibao Ndio tatizo Lake ajui kurelax
 
Huwa namfatilia Facebook ... Duuuuuh kiukweli bora nisiseme
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom