Sam Mahela tena... Hivi ITV management hamyaoni haya?

Sam Mahela tena... Hivi ITV management hamyaoni haya?

Nali

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
1,155
Reaction score
813
Huyu jamaa vipi jamani?! Nimefuatilia kipindi cha DK45 ITV na leo mgeni ni N/Waziri wa Muungano na Mazingira na mada ilikua ni Mazingira.

Huyu Sam Mahela, kama kawaida yake kuingilia mzungumzaji wakati anatiririka vizuri kwenye mada husika. Anageuka kuwa mzungumzaji Mkuu, anatoa maoni yake Mfano...."Mimi/sisi waandishi wa habari tumefanya tafiti na ni kweli/sio kweli kwamba Kuna uharibifu wa Mazingira"..... Sasa kama ulikua unajua ukweli/uongo wa jambo ya nini kumwalika mgeni studioni wakati ulikua na misimamo yako kwenye topic husika?

Mfano alipokua akiagana na N/W huyo, akawa anamsisitiza "Fanya kazi, umesikia, fanya kazii, umepewa kazi ufanye, sawa... maana hata mm hapa ITV napiga kazi"..... Hapa ni kiherehere tu cha huyu maana sio wajibu wake kumweleza hayo.

Nimekuwa nikifuatilia kipindi hiki lakini watu wengi wanakereka sana na huyu jamaa..... Atulie, atoe nafasi ya mgeni husika kusema na baada ya hapo maswali.

Mwanzilishi wa kipindi hiki na Buholela walikua wazuri sana sio kama huyu kijana.
 
Nimeshangaa sana...Tatizo la Waandishi wa Habari wengi Tz ni walifeli elimu za awali,huku kwenye uandishi likawa chaka li kujifichia pale DSJ Ilala...Chuo alichosoma Sinta wa Juma Nature

Ujuwaji mwingiiiiii...mtu hatoi nafasi hata kwa mzungumzaji aongee,yeye anauliza swali,muhusika akianza kujibu na yeye anaingilia...
 
Nimeshangaa sana...Tatizo la Waandishi wa Habari wengi Tz ni walifeli elimu za awali,huku kwenye uandishi likawa chaka li kujifichia pale DSJ Ilala...Chuo alichosoma Sinta wa Juma Nature

.
Juma Nature si alishasema kitambo kwamba "Sitaki Demu"? Sasa kwa nini bado mnambambikia huyo Sinta, kwani hajapata mwanamume mwingine jamani?
 
Nimeshangaa sana...Tatizo la Waandishi wa Habari wengi Tz ni walifeli elimu za awali,huku kwenye uandishi likawa chaka li kujifichia pale DSJ Ilala...Chuo alichosoma Sinta wa Juma Nature

Ujuwaji mwingiiiiii...mtu hatoi nafasi hata kwa mzungumzaji aongee,yeye anauliza swali,muhusika akianza kujibu na yeye anaingilia...
Chuo alichosoma Sinta wa Juma Nature,mhh!
 
Hawa jamaa sijuagi wanafundishwa nn huko wanakosemea upaparazi!
 
Ni kweli Sam Mahela ana bore sana uendeshaji wa dakika 45. Ni kama anakuwa na misimamo yake na maelezo yake kichwani halafu wakati muhojiwa anatoa ufafanuzi huwa anamkatisha na kuchomeka ya kwake. INAKUWA KAMA MAZUNGUMZO TU NA SI MAHOJIANO.

Halafu maswali yake mengine ni maswali yenye majibu tayari. Mfano anamwuliza Mh. Ndalichako: "kwa nini muliwatimua wanachuo UDOM katika mazingira yale?" Kabla Mh hajajibu anaendelea: "Au bila shaka kuna sababu mahsusi ya kwamba labda mlishafanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa hawakuwa na sifa au kozi hiyo haikuwa na tija, tueleze"

Huu sio uulizaji wa maswali ya mahojiano. Wawe wanaangalia vipindi kama Hard Talk au watangazaji kama Amanpour, mtu anaulizwa maswali magumu na ya mtego ili tujue ukweli lakini pia tuone kama anajua vizuri context ya maamuzi anayotoa.

SAM MAHELA AACHE MBWEMBWE, ATULIE NA AANDAE VIZURI MASWALI YAKE.
 
Nimeshtuka kidogo, kama wa itv ndiyo hivi wale wa clouds basi hawakupitia Hata kile cha ilala. Duhhh
Nimeshangaa sana...Tatizo la Waandishi wa Habari wengi Tz ni walifeli elimu za awali,huku kwenye uandishi likawa chaka li kujifichia pale DSJ Ilala...Chuo alichosoma Sinta wa Juma Nature

Ujuwaji mwingiiiiii...mtu hatoi nafasi hata kwa mzungumzaji aongee,yeye anauliza swali,muhusika akianza kujibu na yeye anaingilia...
 
Huyu kijana hana uwezo wa kuendesha mijadala..hata kutangaza habari ndo kwanza anajikongoja..
Huyu alifaa abaki kukusanya habari mitaani..

Na pia anapenda sifa Sana na ndio zinazomharibia..

Vinginevyo anaweza zaidi katika kuripoti habari mitaani..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom