Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,384
Wanahabari wa TZ hakika ni kichefuchefu...usiku huu katika kipindi cha DK.45 cha ITV, presenter wa kipindi hicho Sam Mahela amedai kuwa wakati wa JK kulikuwa na mpango wa kutoa mil. 20 kwa kila kijiji Tanzania Bara - amechapia hilo wakati akimhoji Bi.Bengi Issa ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuhusu Mpango wa kutoa mil.50 kwa kila kijiji; hoja yake ilikuwa ni kwamba kama Mpango wa JK wa "mil.20 kwa kijiji" ulishindwa, Magufuli atabadili nini ili mil.50 kwa kila kijiji nao usiwe ni mpango hewa.
Siku ya Kupatwa Jua watangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds Media walihangaika mno kuelezea jinsi kupatwa kwa jua kunavyotokea...ajabu pamoja na kuonekana wazi hawaelewi chochote kuhusu hilo tukio lakini walijitia kujua na wakaishia kupotosha. Sasa mimi nauliza swali, kwanini mtu usifanye utafiti wa kutosha na kujielimisha kabla ya kusikika kwenye mass media kujadili mada asiyoijua na kuishia kupotosha?
Ajabu eti hawa ndo baada ya siku chache unasikia kateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, au Mwandishi wa hotuba za Rais, au Mkurugenzi wa Jiji...huu kama si uchochezi wa wazi wazi ni kitu gani?