Salute kwa waliosoma PCB/PCM

Salute kwa waliosoma PCB/PCM

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,475
Reaction score
33,038
soldier-294475_1280.png
lol

hao waliosoma hizo kombi walikua wanasoma sana jamani,

Leo nataka kujua was it worth?LOL

naomba mliosoma hizi kombi msaidie watoto wafanye right choice..

ningependa kujua;ulisoma nini kati ya hizo?matarajio yako yalikua nini? umeachieve?nini changamoto ulizokumbana nazo mpaka umefikia hapo?

currently huku mtaani,PCB ni madaktari na PCM ni ma engineer

nauliza hivi kwa nini mnatoka kusoma kozi ngumu advance then mnachagua masomo magumu Zaidi huko chuo???😀😀😀😀😀😀😀😀

je wanafanya hivi kwa kuwa hamna choices nyingi?
 
Kiswahili na History mbona ndio magumu. Yaani mimi kukariri miaka ya watu kuzaliwa, kupigana, kufa nk ilinishinda kabisa. Masomo ya sayansi yamenifikisha mbali lakini hata hivyo kwa sasa natamani uchumi. Najua hii ni nature ya binadamu tu - kutaka kile asichokuwa... Mrefu anataka kuwa mfupi, mfupi anataka kuwa mrefu nk.
 
Nilisoma PCM kwa sababu Sikuwa na interest na Masomo kama English na Kiswahili, ila ukweli Advance kulikuwa na Challenge kubwa ya Physics.. Mbaya..Zaidi ni Engineering Huko Chuo.. Maybe Ukutane na Kitu Kinaitwa Staticaly Determinate Structures (Civil II).. Moto wake si wa Kawaida.. Haulali!
 
Kijana wangu akikusikia unauliza hivo atakushangaa sana! Ila kusema ukweli hakuna somo rahsi kama hesabu! Mwanangu kuongea Kiingereza ni kazi yaani mpaka uje ufanye watu wacheke siyo rahisi kivile!! Kiswahili na yale ma mofimu yao sijui ndio nini??
 
Kuna mtabe mmoja wa PCM tulkutana chuo kwenye course ya finance.
Nkawa namuuliza Newton's laws zinakusaidia nini hapa tulipo??

Hadi kesho hajanipa majibu huyu banker wa sasa hivi na pcm wa zamani.
hahaha
 
PCM sio ngumu ni perception za watu ndiomaana one za 3 zinakua nyingi PCM kuliko arts.

Physics mziki lakini, hesabu na kemia maji tu lakini wanafunzi wanaogopa hesabu sijui kwanini
Kikubwa malengo,halafu wengine husoma PCM kwani ina uwanja mpana wa kuchagua course chuo IKIWA UMEFAULU, arts kufaulu si ngumu kama science,ila ni njia ipitwayo na wengi hivyo ushindani mkubwa,mtu aweza pata div 2,akakosa chance nzuri chuo,kupata Div one pt 3 ni ngumu kwa arts lakini kufail sio rahisi,nmechoka kuandika
 
Hawa walisoma 'historia' tu ya sayansi(pcb and pcm), ukitaka kujua walisoma historia ya haya masomo waulize ni kipi walichogundua. Wanakariri theory zilezile za kina Isaac newton, au archimedes hahahaha, afterall tunafurahi kuwa nao,simply because they give us challenges...
 
H
Hawa walisoma 'historia' tu ya sayansi(pcb and pcm), ukitaka kujua walisoma historia ya haya masomo waulize ni kipi walichogundua. Wanakariri theory zilezile za kina Isaac newton, au archimedes hahahaha, afterall tunafurahi kuwa nao,simply because they give us challenges...
Haha,first world war na second manayosoma history mmegundua nyie?halafu ukikosa ajira arts utafanya nn km sio kukimbilia business au kilimo?sayansi waweza kuwa fundi.
 
....Narudia ndugu Motcu, moja ya misingi mikubwa ya sayansi(pcb and pcm) ni ugunduzi, na sio historia ya uanasayansi. Tatizo huanzia kwenye ufahari wakati wa uchaguzi kuliko inavyodhaniwa katika application yake. Mathalani, unajihitaje mwanasayansi kwa kutumia chemicals, za wanasayansi wenzio maabara au whatever? Unajitofautisha na hawa waliosoma history kwa lipi?....(ingawa history nayo ni sayansi, refer Dk leaky-olduvai george)....ukija kwenye hoja ya kuajiriwa ni kweli ,lakini ukija kwenye innovation, theories ni zilezile miaka nenda rudi. Wanasayansi mjiongeze ili kuendana na kasi ya viwanda, na uchumi wa kati. Kumbuka mnategemewa sana.
 
Back
Top Bottom