Wakati napita pita kwenye milardayo dot com nimeona kuna hii habari ipo kwenye kichwa cha habari cha gazeti la MIKASA. Kwa wale watakaobahatika kuisoma naomba mje mnihadithie ni mimba ya nani na ina miezi mingapi..? Asante
Umbea bana...hebu ngoja nitengeneze picha ya hili..
Saa kumi na mbili alfajiri nasikia mlango unagongwa kwa fujo...nashtuka na kujaribu kutaka kujiridhisha kama ni kweli au naota...mlango unagongwa tena, safari hii inaambatana na sauti 'fungua bana kuna habari nzito huku' ........najikusanya kujiinua na kujongea mlangoni kwa kasi.....nafungua mlango na kabla ya salamu wala nini nakumbana na sauti kali "Salama Jabir kapigwa mimba'"...nami nashtuka na kujikuta nasema "TOBA" huku naziba mdomo.