Sakata la vyeti feki Daudi Bashite Vs Makonda Paulo

Sakata la vyeti feki Daudi Bashite Vs Makonda Paulo

Usiseme jamii yote.eboh!
Sema sisi tunaokesha kwenye mitandao.
Ni ujinga uliotukuka kusemea mioyo ya wengine
 
Peleka hizo forgery kwa mamlaka husika zifanyiwe kazi.
Sio kusema mmnazo wakati mmeziatamia
 
Bashite aache kulialia aoneshe tu vyeti mambo yaishe, Kama Hana aende Kanisa la ufufuo na uzima akaungame atasamehewa tu
 
Muda unaoutumia kumjadili Makonda ungeutumia kufanya kazi nchi ingekua mbali kimaendeleo.
Lakini umekubali kutumika tumikA jomba
 
Naamin ikitokea Makonda akawa sawa kwenye vyeti,Lazima utapata stroke.
Sio kwa michozi hii kama mbwa mwizi.
6f782c3d8089c140d17486dce1a31f33.jpg
 
Katika bandiko langu nimetoa mifano michache ninayoikumbuka, ambayo wengine walitoka hadharani na kujibu shutuma lakini bado walienda na maji, wengine walibaki kimya hadi wengine kuwasemea Mfano Dr. Mathayo David, alikuwa Mbunge huko Moshi Same ingawa sikumbuki specific SAME IPI, na baadaye alikuja kuwa Waziri nadhani kwenye mifugo na uvuvi, lakini inasemekana hakukuwa na utata wa aina yoyote kwenye Elimu yake. Na yeye hakuwa kuita press yoyote akaanza kuonesha vyeti, alikaa kimya na akaendelea kutumikia wananchi wake na Taifa kwa ujumla hadi muda ulipoisha ukiondoa lile sakata la operation ya mifugo/wafugaji

Ndio maana nimesema katika hili la Makonda siwezi kuamini kila kitu, natamani kuona haki ikitendeka kwa huyu bwana. Ametuhumiwa kwa mengi, haiwezekani kila siku aite press conference kuja kujibu scandal.
Mwanzo tuliambiwa ana mahusiano na Masongange, hiyo aite press akanushe, tukaambiwa ana majumba ya kifahari Mwz na kwingineko, aite press akanushe, tukaambiwa amesafirishwa kwenda nje ya nchi na mafisadi, nayo aite press akanushe na sasa DAUDI BASHITE, aite press akanushe nk nk nk, .
Bado naamini tunazo taasisi makini na zenye watu wenye uweledi katika kazi zao, tuwaache wafanye kazi pasipo papara na shinikizo.
Mheshimiwa JK, akiwa Rais wa awamu ya NNE ya JMT, aliwahi kusema hadharani, kuwa aliwahi kuidhinisha kufukwa kazi kwa afisa mmoja wa serikali, lakini baada ya uchunguzi wa kina ikagundulika kuwa yule afisa hakuwa amefanya kosa lolote bali aliundiwa zengwe na wenzake baada ya kuwa yeye amekuwa kikwazo kwao kupiga deal, na hivyo kulazimika kumrudisha kazini. Huyo ni mmoja tu ambaye Mh. Rais alimsema hadharani pasipo kumtaja jina na Rais alionesha masikitiko makubwa, Je unadhani wangapi wameenda na maji hata pasipo kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Kosa analotuhumiwa kwalo Ndg Makonda ni kibwa sana kutoka na comments za baadhi ya wanasheria ambao nimewasoma kwenye social media, naamini kama lipo tutamuona hadi Mahakamani lakini kama halipo na ni uzushi naamini tutaendelea kumuona ofisini kama RC wa DSM.
Siyo lazima aite press conference, yeye aweke tu vyeti vyake na mambo yatakwisha.
 
Mbona mnatumia nguvu kubwa sana dhidi ya Makonda kuna nini kwani?
Mbona hamlali hamfanyi Kazi kila dakika Makonda makonda kwani kuna tatizo gani?

Hizi thread za Makonda zinaboa kwa sasa
Huo ndio ukweli.
Kila mtu ndo thread anayofungua, hivi hatuna jambo lingine kweli tuzungumzie?
Wiki ya ngapi sasa? Mbona Magufuli yuko kimya? Mbona Makonda yuko kimya?
Acheni hizo habari bhana au mmetumwa na watu flani
amna aliekulazimishaufunguehizo nyuzi znazomzungumzia huyo bwana.....
 
Muda unaoutumia kumjadili Makonda ungeutumia kufanya kazi nchi ingekua mbali kimaendeleo.
Lakini umekubali kutumika tumikA jomba
we nawe umevurugwa kweli..we mwenyew ni mmoja wapo wa walioko kwe huu mjadala muda huu kwenye uzi huu halafu cjui unaongea vitu gani!!
 
Nimeamini watanzania wengi uwezo wao wa kufikiria ni mdogo baada ya kuwaona wengi wakishindwa kung'amua ukweli kwamba Makonda hana vyeti halisi kwa sababu ameshindwa kuvitoa ilihali hakuna ugumu wowote km vipo na pia kulia bila sababu ya msingi.
 
Katika mjadala huu huko nyuma nilisema, Tanzania ina vyombo vyake vingi tu na vina wataalamu wengi na wenye uweledi wa kutosha, tuwape nafasi wafanye uchunguzi wao kusuhu sakata la Bashite, wakimaliza tutajulishwa ama hadharani ama kwa vitendo.

Kitendo cha leo Ndg Paulo Makonda Mkuu wa Mkoa DSM, kuadhimisha mwaka wake mmoja kwa RC wa DSM na adhimisho hilo kufanyika public na kuhudhuliwa hadi na viongozi wa dini na kuwa covered na reputable media kama Azami TV nk,
itoshe kusema kuwa Makonda yuko safi na hakuna magumashi juu ya Elimu yake.

Nilisema kwa kuzingatia kazi alizofanya kwa siku za karibuni kabla ya hii skendo kuibuka na kuangalia nguvu ya watu walioguswa negatively na utendaji wa Ndg Makonda, nitakuwa wa mwisho kumunyoshea kidole kuhusu sakata lililokuwa likisemwa.

Narejea kusema tupige kazi, haya majungu yatatupotezea muda pasipo kupata faida yoyote ile. Kumsaidia drug dealer katika kumuchafua kiongozi yeyote yule wa serikalini ama sekta binafsi huwezi pata mgao toka kwa huyo drug dealer hata kama kwa bahati mbaya mkishinda hiyo vita yake haramu.
 
Kuna vitu huwa sielewi hapa. Mwaka fulani ilitajwa orodha ya mafisadi wa elimu waliokuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge alikuwa Marehemu Mzee Samwel Sita (Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi, Amina), Spika akaingilia kati kusema PhD ya Dr. Mathayo David ilikuwa halali hivyo katajwa kimakosa, ila wengine wote waliobaki hakuwasemea mf, akina Dialo (Dr.), Merry Nagu (Dr.) nk. Lakini nakumbuka baada ya Mzee Sita kusema hivyo, TCU immediately walitoa tamko, ya kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kusema kama Degree ya mtu fulani ni feki ama vinginevyo na baada ya hapo hata vile vijarida na yule bwana aliyekuwa kinara wa ile scandal sijui walipotelea wapi.

Nirejee kwenye hii scandal maarufu ya Daudi Bashite Vs Paulo Makonda, tunazo taasisi zetu nyingi kuanzia hizo za kitaaluma alikopita huyo Ndg, anza secondary school both O level and Advanced Level, kuna walimu waliomfundisha, na baraza la Mtihani NECTA nk. Twende kwenye Chuo alichosoma tena hivi majuzi tu kote huko vyombo vya kiuchunguzi vinapajua na panafikika na sio wala nje ya nchi na hakuna gharama kihivyo.

Binafsi naamini kama hiyo ni kweli ni swala la muda tu, let us wait and see, lakini kama ni longo longo kwa nini tunapoteza muda wetu.
Kuna mkubwa mmoja katika taasisi moja hapa nchini, yeye alisema ana PhD, Chuo alichopata hiyo Degree yake SA, watu wakaanza kusema sema alikimbia mwenyewe ofisi, ingawa kiutendaji alikuwa mzuri kabisa na ni kweli aliwahi kufanya hiyo Degree yake huko SA ingawa haiku- materialize.
Kumbe basi ni swala la muda tu, maana tumeshudia watu wengi wakifutika humu makazini kama upepo na wengine wakistafu gafla, ukiuliza unaambiwa vyeti vina utata, hivyo basi kama jamaa naye kuna hila ipo siku ataondoka tu. Binafsi naamini kwa hizi kelele ambazo zimepigwa kuhusu Bashite vyombo vya uchunguzi vilikwisha maliza kukusanya taarifa kuanzia kijijini Kolomije, shuleni msingi na sekondari na hadi chuo.

Nikimwaangalia Makonda bado ni kijana kuliko mimi, lakini mimi nikienda shuleni kwangu msingi bado wapo walimu walionifundisha primary pale kituoni zaidi ya 20 yrs ago, ingawa wengine wamehama na wengine kustaafu, lakini hata wasipokuwepo taarifa zinapatikana tu. Sasa sembuse huyo, Jamani Sefue Ombeni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aliandikwa na Gazeti moja tu, akatoka akakanusha kwa nguvu zote juu ya ile taarifa na vitisho vya kwenda mahakamani na kudai fidia, mbona baada ya muda mfupi aliondoka. Ingawa sijui kama kuondoka kwake kulitokana na ile habari iliyooandikwa na lile gazeti, lakini walau ndio taarifa pekee ya mwisho iliyokuwa na ukakasi kumuhusu yeye binafsi na sio taasisi.

Mamlaka ya uteuzi wa Mkuu wa Mkoa (RC) ambayo ni Rais, ina mikono mirefu na mipana, ina macho mengi na yenye nguvu ya kuona kila sehemu, tuipe ushirikiano chanya katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku likiwemo hili la Daudi Bashite nadhani itatoa majibu nasi tutayaona hata pasipokuambiwa. Hizi kelele nyingi kupita kiasi zinaweza hata kuwapoteza na kuipuuzia hii taarifa kwa kuzani ni kelele za watu walioguswa na utendaji wa Ndg Makonda hasa kwenye dawa za kulevya.

Katika utendaji kazi wake hasa kwa siku za hivi karibuni kama Mkuu wa Mkoa Ndg Makonda sote tunajua amegusa eneo la watu wenye nguvu ya pesa chafu, majuzi nimeona comment ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, juu ya hii vita, kila mtu anajua nguvu ya hao watu, wanaweza fanya jambo lolote hasa kwa watu wa kawaida kama akina RCs nk, maana kuna nchi tunaambiwa hata President anaweza kupinduliwa na drug dealers, hivyo mimi kwa kutambua uwezo mkubwa wa watu walioguswa na RC Makonda hivi karibuni, nitakuwa wa mwisho kuamini kila baya linalozungumzwa kuhusu Makonda kwenye social media na kwingineko mpaka vyombo husika vitakapo toa taarifa aidha in public ama tukaona vitendo kama enzi ya kina Sefue nk. Mwanzoni kuanzia kule Bungeni tuliambiwa ana majumba ya Gorofa ndani mwaka mmoja nk, leo havisemwi tena.
Mwisho kabisa, natamani kuona vyombo vyetu (Responsible Institution) zikifanya kazi yake kwa umakini na kutoa taarifa sehemu husika kwa utekelezaji na sio vinginevyo. Ahsante

mnapata wapi muda wa kuandika wishes na kuishia kusema unatamani unatamani

waTZ wambeya sana
 
Katika mjadala huu huko nyuma nilisema, Tanzania ina vyombo vyake vingi tu na vina wataalamu wengi na wenye uweledi wa kutosha, tuwape nafasi wafanye uchunguzi wao kusuhu sakata la Bashite, wakimaliza tutajulishwa ama hadharani ama kwa vitendo.

Kitendo cha leo Ndg Paulo Makonda Mkuu wa Mkoa DSM, kuadhimisha mwaka wake mmoja kwa RC wa DSM na adhimisho hilo kufanyika public na kuhudhuliwa hadi na viongozi wa dini na kuwa covered na reputable media kama Azami TV nk,
itoshe kusema kuwa Makonda yuko safi na hakuna magumashi juu ya Elimu yake.

Nilisema kwa kuzingatia kazi alizofanya kwa siku za karibuni kabla ya hii skendo kuibuka na kuangalia nguvu ya watu walioguswa negatively na utendaji wa Ndg Makonda, nitakuwa wa mwisho kumunyoshea kidole kuhusu sakata lililokuwa likisemwa.

Narejea kusema tupige kazi, haya majungu yatatupotezea muda pasipo kupata faida yoyote ile. Kumsaidia drug dealer katika kumuchafua kiongozi yeyote yule wa serikalini ama sekta binafsi huwezi pata mgao toka kwa huyo drug dealer hata kama kwa bahati mbaya mkishinda hiyo vita yake haramu.

asante
 
mnapata wapi muda wa kuandika wishes na kuishia kusema unatamani unatamani

waTZ wambeya sana

Hapa umenipoteza, sijui mimi na wewe ndio miongoni mwa hao wambeya, ama ni mimi na wengineo, maana kama sikosei sote tuu WaTZ. Any na sijui umbea hapo uko wapi maana ungesaidia ku identify hayo maana ya kiumbeya toka kwenye andiko langu walau pia ningekuwa na chakusema. Ahsante
 
Wanasheria naomba mnisaidie, HIVI NAWEZA KUFUNGUA KESI KWA HATI YA DHARURA KUSEMA MKUU WA MKOA WA DAR ANATUMIA JINA NA CHETI AMBAVYO SIO CHAKE. Nakuiomba mahakama kumwita mahakamani kujitetea.
 
Tuchukulie huyu bwana ataendelea kukaa kimya bila kujibu au kuweka vyeti vyake mezani,nini kitafuata baada ya hapo?Me nafikiri mwenye ushahidi uliokamilika kuwa huyu bwana Mkubwa jina analotumia si lake basi kuna sehemu stahiki ya kulifikisha hili,vinginevyo hizi zitakuwa ni kelele tu kama zingine zinazo wahusu wanasiasa na mwisho wa siku litapita.
Una akili sana wewe.Hili la bweka bweka ili mwenye nyumba aamke kuangalia kuna nini halitasaidia.Una ushahidi,beba ushahidi wako peleka kunakohusika.Sheria ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom