Sakata la vyeti feki Daudi Bashite Vs Makonda Paulo

Sakata la vyeti feki Daudi Bashite Vs Makonda Paulo

Hivi ile polisi jamii imeishia wapi? Tuliambiwa kutoa taarifa polisi pale tunapohisi uhalifu hivi kwa mfano ingekuwa taarifa hizi za zero bashite ni za majambazi mahala fulani hivi tungeambiwa tukathibitishe mahakamani ndo serikali ichukue hatua? Mbona polisi jamii kwa bashite sifuri ina ganzi ya lignocane au tetrachloromethane ( Chloroform)? Wewe unaesema tupeleke ushahidi mahakamani kwa hiyo serikali ipo likizo au? Inamaana kule mtaani kwenu ukiona tukio baya au dalili zake ukienda kuwatonya polisi watakuambia uende ukafungue jalada ndo waje wachunguze?
 
Toka iibuke hoja ya vyeti fake kumuhusu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda na baadae kuchagizwa na Mch. Gwajima kutokana na kisasi cha kutajwa ktk orodha ya wauza madawa ya kulevya, jambo hili limekuwa ndio habari ya mjini, kila mmoja kwa namna yake amekuwa msemaji kulingana na upande anaoshabikia!

Wapo wanaotumia kama fimbo ya kumchapia Makonda,
Wapo wanaojaribu kumtetea, na wapo wanaojaribu kuhoji ukweli wa habari yenyewe....


Moto ukawaka zaidi pale Mh. Alipovamia Studio za Clouds media!
Bali hali ikawa tete zaidi pale Mheshimiwa Nape alipovuliwa uwaziri kwa kile kilichosemekana kuingilia mamlaka ya Rais.
Ajenda kuu ni vyeti, vyeti, vyeti, vyetiii..!!


Kinachoipa promo zaidi ajenda hii ni kule kulindwa zaidi na Mkuu wa kaya RC huyu, kiasi cha kuitwa "Untouchable"
Lakini pia kutojitokeza hadharani kukanusha au kuthibitisha madai haya ya kughushi vyeti..!!

Mengi yamesemwa na kujadiliwa, lakini kitu kimoja ningependa kuhoji leo na yeyote mwenye majibu itakuwa ndio mwisho wa utata huu!!

Huyu mtu wa kuitwa DAUDI ALBERT BASHITE au PAUL CHRISTIAN MAKONDA kwa mujibu wa Mange Kimambi na Gwajima, nasaba yake ni ipi?
Hapa nakusudia ni mtoto wa familia ya nani, ni mtoto wa ngapi kwa kuzaliwa, ndugu zake ni kinanani na wako wapi! Ndugu zake wa kiume wanatambulikaje??

Kwa kufanya hivyo tutajua kama kweli RC ni Daudi Bashite kama ambavyo wanatuaminisha au Paul Makonda kama anavyojitambulisha mwenyewe.

Kwani, kama walizaliwa watoto wanne ktk familia ya mzee Bashite, na yeye alibadili jina kwasababu ya vyeti. Hapa itajulikana kwani ndg zake bado watatumia ubini ule ule wa Bashite.
Yaani atakuwepo Joseph Albert Bashite,
Agness Albert Bashite, Paul Christian Makonda/Daudi Albert Bashite na Anna Albert Bashite

Vinginevyo kama ndugu zake wa damu wanatumia ubini wa Makonda, ni wazi atakuwa amedhulumiwa kwa kusingiziwa na kutuhumiwa ktk mambo yasiyo ya kweli..!!!

Nawasilisha! Wale wa matusi mbele pia karibuni..!!!
 
Ile ishu ya kutinga clouds tu ilithibitisha,lisemwalo lipo bro.
 
Kwani umeambiwa tatizo ni jina?tatizo sio jina.jina MTU anaweza kubadili,tatizo ni vyeti vya MTU mwingine
 
Mkuu hoja ni nzuri sana hii,hapo mwanza siyo China wala haitaki passport kufika. Anayetaka kidhati kumjua yule bwana aende huko akutane na wazazi wake waliomzaa,siyo tunaletewa stori za walezi hapa,kwani ni yatima huyu?
Ukitaka ukweli gharamia. Vinginevyo tutaishia tu hewani.
 
inashangaza kwamba unaweza kugombana na mtu yeyote hata waziri, hautapata shida, ila ukigombana na mkuu wa mkoa utahatarisha maisha yako. I wonder how special is this man compared to others. ana nini cha ziada kuwazidi hata mawaziri?
 
Kuna vitu huwa sielewi hapa. Mwaka fulani ilitajwa orodha ya mafisadi wa elimu waliokuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge alikuwa Marehemu Mzee Samwel Sita (Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi, Amina), Spika akaingilia kati kusema PhD ya Dr. Mathayo David ilikuwa halali hivyo katajwa kimakosa, ila wengine wote waliobaki hakuwasemea mf, akina Dialo (Dr.), Merry Nagu (Dr.) nk. Lakini nakumbuka baada ya Mzee Sita kusema hivyo, TCU immediately walitoa tamko, ya kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kusema kama Degree ya mtu fulani ni feki ama vinginevyo na baada ya hapo hata vile vijarida na yule bwana aliyekuwa kinara wa ile scandal sijui walipotelea wapi.

Nirejee kwenye hii scandal maarufu ya Daudi Bashite Vs Paulo Makonda, tunazo taasisi zetu nyingi kuanzia hizo za kitaaluma alikopita huyo Ndg, anza secondary school both O level and Advanced Level, kuna walimu waliomfundisha, na baraza la Mtihani NECTA nk. Twende kwenye Chuo alichosoma tena hivi majuzi tu kote huko vyombo vya kiuchunguzi vinapajua na panafikika na sio wala nje ya nchi na hakuna gharama kihivyo.

Binafsi naamini kama hiyo ni kweli ni swala la muda tu, let us wait and see, lakini kama ni longo longo kwa nini tunapoteza muda wetu.
Kuna mkubwa mmoja katika taasisi moja hapa nchini, yeye alisema ana PhD, Chuo alichopata hiyo Degree yake SA, watu wakaanza kusema sema alikimbia mwenyewe ofisi, ingawa kiutendaji alikuwa mzuri kabisa na ni kweli aliwahi kufanya hiyo Degree yake huko SA ingawa haiku- materialize.
Kumbe basi ni swala la muda tu, maana tumeshudia watu wengi wakifutika humu makazini kama upepo na wengine wakistafu gafla, ukiuliza unaambiwa vyeti vina utata, hivyo basi kama jamaa naye kuna hila ipo siku ataondoka tu. Binafsi naamini kwa hizi kelele ambazo zimepigwa kuhusu Bashite vyombo vya uchunguzi vilikwisha maliza kukusanya taarifa kuanzia kijijini Kolomije, shuleni msingi na sekondari na hadi chuo.

Nikimwaangalia Makonda bado ni kijana kuliko mimi, lakini mimi nikienda shuleni kwangu msingi bado wapo walimu walionifundisha primary pale kituoni zaidi ya 20 yrs ago, ingawa wengine wamehama na wengine kustaafu, lakini hata wasipokuwepo taarifa zinapatikana tu. Sasa sembuse huyo, Jamani Sefue Ombeni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aliandikwa na Gazeti moja tu, akatoka akakanusha kwa nguvu zote juu ya ile taarifa na vitisho vya kwenda mahakamani na kudai fidia, mbona baada ya muda mfupi aliondoka. Ingawa sijui kama kuondoka kwake kulitokana na ile habari iliyooandikwa na lile gazeti, lakini walau ndio taarifa pekee ya mwisho iliyokuwa na ukakasi kumuhusu yeye binafsi na sio taasisi.

Mamlaka ya uteuzi wa Mkuu wa Mkoa (RC) ambayo ni Rais, ina mikono mirefu na mipana, ina macho mengi na yenye nguvu ya kuona kila sehemu, tuipe ushirikiano chanya katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku likiwemo hili la Daudi Bashite nadhani itatoa majibu nasi tutayaona hata pasipokuambiwa. Hizi kelele nyingi kupita kiasi zinaweza hata kuwapoteza na kuipuuzia hii taarifa kwa kuzani ni kelele za watu walioguswa na utendaji wa Ndg Makonda hasa kwenye dawa za kulevya.

Katika utendaji kazi wake hasa kwa siku za hivi karibuni kama Mkuu wa Mkoa Ndg Makonda sote tunajua amegusa eneo la watu wenye nguvu ya pesa chafu, majuzi nimeona comment ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, juu ya hii vita, kila mtu anajua nguvu ya hao watu, wanaweza fanya jambo lolote hasa kwa watu wa kawaida kama akina RCs nk, maana kuna nchi tunaambiwa hata President anaweza kupinduliwa na drug dealers, hivyo mimi kwa kutambua uwezo mkubwa wa watu walioguswa na RC Makonda hivi karibuni, nitakuwa wa mwisho kuamini kila baya linalozungumzwa kuhusu Makonda kwenye social media na kwingineko mpaka vyombo husika vitakapo toa taarifa aidha in public ama tukaona vitendo kama enzi ya kina Sefue nk. Mwanzoni kuanzia kule Bungeni tuliambiwa ana majumba ya Gorofa ndani mwaka mmoja nk, leo havisemwi tena.
Mwisho kabisa, natamani kuona vyombo vyetu (Responsible Institution) zikifanya kazi yake kwa umakini na kutoa taarifa sehemu husika kwa utekelezaji na sio vinginevyo. Ahsante
Makonda au Bashite ni mkuu wa mkoa kwa sababu rais kaamua.Kwa hiyo sio vyeti feki, ujambazi wake wala utekaji watu utamfanya rais atengue ukuu wake wa mkoa. Lazima ujue kua kitu ambacho Bashite anamfanyia rais ni kikubwa kuliko uvunjifu wowote wa sheria za nchi hii.Makonda au Bashite ni RC wa Dar kwa sababu binafsi za mkuu!
 
inashangaza kwamba unaweza kugombana na mtu yeyote hata waziri, hautapata shida, ila ukigombana na mkuu wa mkoa utahatarisha maisha yako. I wonder how special is this man compared to others. ana nini cha ziada kuwazidi hata mawaziri?
Nani ana samb..nda zaidi yake?
 
Amalize kwanza madawa ya kulevya Dar na kwingineko hiyo ya kufoji vyeti ni baadaye
 
Ww inakuuma nn makonda kuwa na vyeti feki.....umepungukiwa nn kwa makonda kuwa na vyeti feki....
 
Amejikuta anaogeshwa maji ya baridiiii (na waganga) ili eti Lisu aahirishe mashtaka.
 
Ww inakuuma nn makonda kuwa na vyeti feki.....umepungukiwa nn kwa makonda kuwa na vyeti feki....
Amewahi kusababisha kubenea akapatikana na hatia mahakamani kumbe yeye makonda msababisha tafrani hakupaswa kuwa na cheo hicho kilichomsukuma kuwadharau wawakilishi wetu!!!!!
 
Na mbowe asingepona kwenye hilo sakata
Waambieni wawabadilishie mikakati.
Hii ya mbowe mnajichoresha tu kwa jamii.

Zibeni lile pakacha pale magogoni.
Linatoa maboko sana.
 
Back
Top Bottom