Sakata la vyeti feki Daudi Bashite Vs Makonda Paulo

Lyagwa

JF-Expert Member
Feb 3, 2013
1,639
900
Kuna vitu huwa sielewi hapa. Mwaka fulani ilitajwa orodha ya mafisadi wa elimu waliokuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge alikuwa Marehemu Mzee Samwel Sita (Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi, Amina), Spika akaingilia kati kusema PhD ya Dr. Mathayo David ilikuwa halali hivyo katajwa kimakosa, ila wengine wote waliobaki hakuwasemea mf, akina Dialo (Dr.), Merry Nagu (Dr.) nk. Lakini nakumbuka baada ya Mzee Sita kusema hivyo, TCU immediately walitoa tamko, ya kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kusema kama Degree ya mtu fulani ni feki ama vinginevyo na baada ya hapo hata vile vijarida na yule bwana aliyekuwa kinara wa ile scandal sijui walipotelea wapi.

Nirejee kwenye hii scandal maarufu ya Daudi Bashite Vs Paulo Makonda, tunazo taasisi zetu nyingi kuanzia hizo za kitaaluma alikopita huyo Ndg, anza secondary school both O level and Advanced Level, kuna walimu waliomfundisha, na baraza la Mtihani NECTA nk. Twende kwenye Chuo alichosoma tena hivi majuzi tu kote huko vyombo vya kiuchunguzi vinapajua na panafikika na sio wala nje ya nchi na hakuna gharama kihivyo.

Binafsi naamini kama hiyo ni kweli ni swala la muda tu, let us wait and see, lakini kama ni longo longo kwa nini tunapoteza muda wetu.
Kuna mkubwa mmoja katika taasisi moja hapa nchini, yeye alisema ana PhD, Chuo alichopata hiyo Degree yake SA, watu wakaanza kusema sema alikimbia mwenyewe ofisi, ingawa kiutendaji alikuwa mzuri kabisa na ni kweli aliwahi kufanya hiyo Degree yake huko SA ingawa haiku- materialize.
Kumbe basi ni swala la muda tu, maana tumeshudia watu wengi wakifutika humu makazini kama upepo na wengine wakistafu gafla, ukiuliza unaambiwa vyeti vina utata, hivyo basi kama jamaa naye kuna hila ipo siku ataondoka tu. Binafsi naamini kwa hizi kelele ambazo zimepigwa kuhusu Bashite vyombo vya uchunguzi vilikwisha maliza kukusanya taarifa kuanzia kijijini Kolomije, shuleni msingi na sekondari na hadi chuo.

Nikimwaangalia Makonda bado ni kijana kuliko mimi, lakini mimi nikienda shuleni kwangu msingi bado wapo walimu walionifundisha primary pale kituoni zaidi ya 20 yrs ago, ingawa wengine wamehama na wengine kustaafu, lakini hata wasipokuwepo taarifa zinapatikana tu. Sasa sembuse huyo, Jamani Sefue Ombeni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aliandikwa na Gazeti moja tu, akatoka akakanusha kwa nguvu zote juu ya ile taarifa na vitisho vya kwenda mahakamani na kudai fidia, mbona baada ya muda mfupi aliondoka. Ingawa sijui kama kuondoka kwake kulitokana na ile habari iliyooandikwa na lile gazeti, lakini walau ndio taarifa pekee ya mwisho iliyokuwa na ukakasi kumuhusu yeye binafsi na sio taasisi.

Mamlaka ya uteuzi wa Mkuu wa Mkoa (RC) ambayo ni Rais, ina mikono mirefu na mipana, ina macho mengi na yenye nguvu ya kuona kila sehemu, tuipe ushirikiano chanya katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku likiwemo hili la Daudi Bashite nadhani itatoa majibu nasi tutayaona hata pasipokuambiwa. Hizi kelele nyingi kupita kiasi zinaweza hata kuwapoteza na kuipuuzia hii taarifa kwa kuzani ni kelele za watu walioguswa na utendaji wa Ndg Makonda hasa kwenye dawa za kulevya.

Katika utendaji kazi wake hasa kwa siku za hivi karibuni kama Mkuu wa Mkoa Ndg Makonda sote tunajua amegusa eneo la watu wenye nguvu ya pesa chafu, majuzi nimeona comment ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, juu ya hii vita, kila mtu anajua nguvu ya hao watu, wanaweza fanya jambo lolote hasa kwa watu wa kawaida kama akina RCs nk, maana kuna nchi tunaambiwa hata President anaweza kupinduliwa na drug dealers, hivyo mimi kwa kutambua uwezo mkubwa wa watu walioguswa na RC Makonda hivi karibuni, nitakuwa wa mwisho kuamini kila baya linalozungumzwa kuhusu Makonda kwenye social media na kwingineko mpaka vyombo husika vitakapo toa taarifa aidha in public ama tukaona vitendo kama enzi ya kina Sefue nk. Mwanzoni kuanzia kule Bungeni tuliambiwa ana majumba ya Gorofa ndani mwaka mmoja nk, leo havisemwi tena.
Mwisho kabisa, natamani kuona vyombo vyetu (Responsible Institution) zikifanya kazi yake kwa umakini na kutoa taarifa sehemu husika kwa utekelezaji na sio vinginevyo. Ahsante
 
Ili hayo yote uliyosema ya kiuchunguzi yafanyike ni lazima kuwe na utashi kutoka kwa vyombo hivyo au mamlaka iliyomteua, kama hamna utashi huo unadhani uchunguzi utafanyikaje?

Kwa mazingira ya sasa nguvu pekee ya wananchi walio wengi ni kusema na kusema na kusema tena!

Suluhisho pekee ambalo kwa kweli ni rahisi mno kuliko hata huo uchunguzi unaosema ni kwa bwana mkubwa kujitokeza na kuonesha vyeti vyake basi!
 
yeye mwenyewe anayetuhumiwa yuko kimya utadhani yuko nje ya nchi kumbe yuko hapa nchini anashindwa nini kuitisha press aseme ukweli ni upi, waandishi wamemuhoji amekuwa mkali na kutoa majibu ya kejeli, hii ya kusingizia watuhumiwa wadawa za kulevya halina mashiko, za mwizi ni arobaini zake zilikuwa zimefika, hata isingekuwa kipindi hili lingeibuka tu.
 
Ndo shida ya elimu ya ugoko, hata kama anavyeti vya ukweli anaogopa kuvitoa,

kuna wengine wakiambiwa watoe vyeti, watafunua mpaka vya uanafunzi bora vya STD1
 
Nani alichunguza mv Magumashi fedha zilizoilipia ni halali au kuna mtu kapiga juu kwa juu
Bila utashi wa kisiasa hakuna uchunguzi rasmi ng'o!
 
Katika bandiko langu nimetoa mifano michache ninayoikumbuka, ambayo wengine walitoka hadharani na kujibu shutuma lakini bado walienda na maji, wengine walibaki kimya hadi wengine kuwasemea Mfano Dr. Mathayo David, alikuwa Mbunge huko Moshi Same ingawa sikumbuki specific SAME IPI, na baadaye alikuja kuwa Waziri nadhani kwenye mifugo na uvuvi, lakini inasemekana hakukuwa na utata wa aina yoyote kwenye Elimu yake. Na yeye hakuwa kuita press yoyote akaanza kuonesha vyeti, alikaa kimya na akaendelea kutumikia wananchi wake na Taifa kwa ujumla hadi muda ulipoisha ukiondoa lile sakata la operation ya mifugo/wafugaji

Ndio maana nimesema katika hili la Makonda siwezi kuamini kila kitu, natamani kuona haki ikitendeka kwa huyu bwana. Ametuhumiwa kwa mengi, haiwezekani kila siku aite press conference kuja kujibu scandal.
Mwanzo tuliambiwa ana mahusiano na Masongange, hiyo aite press akanushe, tukaambiwa ana majumba ya kifahari Mwz na kwingineko, aite press akanushe, tukaambiwa amesafirishwa kwenda nje ya nchi na mafisadi, nayo aite press akanushe na sasa DAUDI BASHITE, aite press akanushe nk nk nk, .
Bado naamini tunazo taasisi makini na zenye watu wenye uweledi katika kazi zao, tuwaache wafanye kazi pasipo papara na shinikizo.
Mheshimiwa JK, akiwa Rais wa awamu ya NNE ya JMT, aliwahi kusema hadharani, kuwa aliwahi kuidhinisha kufukwa kazi kwa afisa mmoja wa serikali, lakini baada ya uchunguzi wa kina ikagundulika kuwa yule afisa hakuwa amefanya kosa lolote bali aliundiwa zengwe na wenzake baada ya kuwa yeye amekuwa kikwazo kwao kupiga deal, na hivyo kulazimika kumrudisha kazini. Huyo ni mmoja tu ambaye Mh. Rais alimsema hadharani pasipo kumtaja jina na Rais alionesha masikitiko makubwa, Je unadhani wangapi wameenda na maji hata pasipo kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Kosa analotuhumiwa kwalo Ndg Makonda ni kibwa sana kutoka na comments za baadhi ya wanasheria ambao nimewasoma kwenye social media, naamini kama lipo tutamuona hadi Mahakamani lakini kama halipo na ni uzushi naamini tutaendelea kumuona ofisini kama RC wa DSM.
 
hua napata ukakasi napoona swala la vyeti vya Makonda (au Bashite) vikihusishwa na madawa ya kulevya.

binafsi mm naamni kua kama mtu ni mhalifu, basi arobaini zake zikifika anakamatwa. arobaini za Mkonda ndio hizi na Mungu amependa arobaini hizo ziwe kipindi hiki. achunguzwe kwa hizo shutuma za uhalifu wake na akibainika kama ni muhalifu aliyefanya uhalifu wa kununua vyeti, basi ahukumiwe kutokana na uhalifu wake.

kuhusu wauza madaya ya kulevya, kwanza naona arobanini zao hazijafikiwa kwani mbinu iliyotumika ilikua ya kurusha jiwe kwenye ndege wengi hivyo wakaruka wote. huwezi kumuambia muuza madawa ya kulevya kua Ijumaa nakuja kukagua madawa nyumabni kwako, kisha yeye awe kayaweka tu kwake akikusubiri uje kuyakamata na kumakamata na yy. Arobaini ya wauza madawa ya kulevya ikifika, wauzaji wataliaa na kusaga meno.
 
Tuchukulie huyu bwana ataendelea kukaa kimya bila kujibu au kuweka vyeti vyake mezani,nini kitafuata baada ya hapo?Me nafikiri mwenye ushahidi uliokamilika kuwa huyu bwana Mkubwa jina analotumia si lake basi kuna sehemu stahiki ya kulifikisha hili,vinginevyo hizi zitakuwa ni kelele tu kama zingine zinazo wahusu wanasiasa na mwisho wa siku litapita.
 
Ili hayo yote uliyosema ya kiuchunguzi yafanyike ni lazima kuwe na utashi kutoka kwa vyombo hivyo au mamlaka iliyomteua, kama hamna utashi huo unadhani uchunguzi utafanyikaje?

Kwa mazingira ya sasa nguvu pekee ya wananchi walio wengi ni kusema na kusema na kusema tena!

Suluhisho pekee ambalo kwa kweli ni rahisi mno kuliko hata huo uchunguzi unaosema ni kwa bwana mkubwa kujitokeza na kuonesha vyeti vyake basi!
Binafsi sasa nafikiri hii issue ishakuwa kubwa sana kwa yeye kujitokeza na kujibu!!

NECTA kwa vile walishaomba taarifa za watu kama hawa. Na huyu bwana jina lake limetawala kwa week kadhaa kwenye vyombo vya habari, ni bora NECTA wakajitokeza hadharani kutuambia ukweli!! Otherwise, NECTA wasitishe hili zoezi maana halina tena uhalali kwa ajili ya double standards!!
 
Kwa mjibu wa watu walisemea hili swala kwa mlengo wa kisheria, inaonesha ni kosa kubwa, (Binafsi sijui sheria, ukiondoa kwa mbali sheria ya ajila ambayo niwahi kuisoma), na kuna watu wamesema wana ushahidi wa kutosha kabisa kuhusu hilo sawala la Daudi Bashite Vs Paulo Makonda, mimi nikadhani labda kama kuna room ya wao kwenda Mahakamani kufungua kesi juu ya hii scandal ya ndg huyu, lakini naona wako busy JF, FB, baadhi ya magazeti basi. Ndio maana binafsi nikadhani kama hawawezi kwenda Mahakani na Makonda yuko kimya, then ni better tuviachie vyombo vyetu vya kiuchuzi kufanya kazi yake. Naamini wakimaliza tutajua ama kwa kuambiwa ama kwa vitendo, nimetoa mifano kwenye bandiko langu. Tufanye kazi jamani hizi kelele zitatutoa kwenye mstari
 
Ndio maana nimesema katika hili la Makonda siwezi kuamini kila kitu, natamani kuona haki ikitendeka kwa huyu bwana. Ametuhumiwa kwa mengi, haiwezekani kila siku aite press conference kuja kujibu scandal.
Mwanzo tuliambiwa ana mahusiano na Masongange, hiyo aite press akanushe, tukaambiwa ana majumba ya kifahari Mwz na kwingineko, aite press akanushe, tukaambiwa amesafirishwa kwenda nje ya nchi na mafisadi, nayo aite press akanushe na sasa DAUDI BASHITE, aite press akanushe nk nk nk, .
mbona yote hayo ukiacha sakata la vyeti aliwahi kuyatolea ufafanuzi!
swala hili lisifanywe kua gumu. kama tatizo ni muda wa kuita press, basi angetumia muda wa jana wa kulia kanisani kusawazisha swala hilo pia; au angetumia muda aliotumia kwenda kuombewa na mashekhe kuzungumzia pia sala hilo.

akikosa muda kabisa, basi akanushe tu kua yeye siye Daud Bashite kasingiziwa hilo jina.
 
Ndo shida ya elimu ya ugoko, hata kama anavyeti vya ukweli anaogopa kuvitoa,

kuna wengine wakiambiwa watoe vyeti, watafunua mpaka vya uanafunzi bora vya STD1
Mkuu umenifurahisha sana. Raha ya kusoma kwa bidii na uhalali ndiyo hiyo unatoa mpaka ripoti za msingi zikionyesha umekuwa wa kwanza,miaka 20 iliyopita.
 
Mfano Dr. Mathayo David, alikuwa Mbunge huko Moshi Same ingawa sikumbuki specific SAME IPI, na baadaye alikuja kuwa Waziri nadhani kwenye mifugo na uvuvi, lakini inasemekana hakukuwa na utata wa aina yoyote kwenye Elimu yake. Na yeye hakuwa kuita press yoyote akaanza kuonesha vyeti, alikaa kimya na akaendelea kutumikia wananchi wake na Taifa kwa ujumla hadi muda ulipoisha
ndugu yangu nimeanza kuona umekuja kumtetea Bashite. Huyu Bashite data zote zipo wazi tiafauti na hao wa zamani uliowataja.
kama lengo lako ni kuja kumrembaremba eti aendelee na kazi wakati jamii yote haina imani naye kutokana na shutuma zake za kuhusika ktk uhalifu wa kununua vyeti, basi umeanza kupoteza mvuto.
 
mimi nikadhani labda kama kuna room ya wao kwenda Mahakamani kufungua kesi juu ya hii scandal ya ndg huyu, lakini naona wako busy JF, FB, baadhi ya magazeti basi.
wewe unataka raia wema wanaofichua uovu ndio wkasimamie kesi mahakani? hiyo kesi ni kati ya jamuhuri na Bashite na sio kati ya raia wema na Bashite. raia wema wamefichua uovu, mamlaka zinazohusika zishughulike na huo uovu. tena zishughulike kwa kasi ile anayoipenda rais wetu Magufuli kwani kila kitu kiko wazi.
 
Jamani naona tunajadili sana suala LA Bashite tukiamini hatua zitachukuliwa dhidi take. Lakini kwa muda muziki juu Wa Bashite umeanza kuimbwa Sizonje angekwisha xhukua hatua. Mi naomba tuache mjadala tuendelee na kazi zetu Sizonje hawezi kumtoa
 
ahamishiwe kitengo cha madawa ya kulevya maana kwa mujibu wa mashabiki zake yeye pekee nchiii ndo kiboko ya wauza unga na akifika huko achague jina la kutumia kama ni Daudi au Paulo au aende mahakamani akaape tena kubadili jina ajiite petro maana anapenda majina ya watu wema wa kwenye biblia
 
Tufanye kazi jamani hizi kelele zitatutoa kwenye mstari
kazi tunafanya na kazi zingine ndio hizi za kufichua wahalifu. hatuwezi kuishi na wahalifu na kuwaficha.
kwakua yeye kakosa namna ya kujitetea, basi mamalaka zinazohusika zitumie muda mfupi kuchunguza. uhakiki wa vyeti Tanzania nzima haukuchukua zaidi miezi miwili, kumbe uhaakiki wa kumahakiki Makonda utatumia wiki moja tu na kila kitu kitakua wazi.
 
Vyombo vimeshafanyakazi yake ambayo ni rahisi sana kwa nchi kama Marekani wangetumia tu fingerprint na taarifa sahihi amepewa Mkuu, tunasubiri tu kabla jogoo hajawika ajitumbuwe mwenyewe au atumbuliwe.
 
ndugu yangu nimeanza kuona umekuja kumtetea Bashite. Huyu Bashite data zote zipo wazi tiafauti na hao wa zamani uliowataja.
kama lengo lako ni kuja kumrembaremba eti aendelee na kazi wakati jamii yote haina imani naye kutokana na shutuma zake za kuhusika ktk uhalifu wa kununua vyeti, basi umeanza kupoteza mvuto.

Siwezi kukuzuia kuwa na mtazamo negative kuhusu mtizamo wangu, that is normal na ndio uhai nchi. Ukikuta mtu anandika kitu na comment zote ni ndio mzee hiyo jamii inaweza kuwa mfu. Kumbe basi siwezi kukulaumu kwa hilo, lakini ukinisoma vizuri juu ya nilichoaandika hakuna sehemu namtete huyo aitwaye Bashite, lakini siwezi kumhukumu direct as if nina ushahidi mkononi. Sijazaliwa Koromije ladda niseme namfahamu, sijasoma naye na sijawahi kuonana naye ana kwa zaidi ya kumuona kwenye media, mimi sio mwanasiasa kama yeye na wala sipo hapa kutafuta mvuto kwa mtu yeyote yule.

Kama Mtanzania wa wakawaida kabisa na mtumiaji wa mtandao ya kijamii kama jf ambapo ni member wa siku nyingi tu, ingawa ni msomaji zaidi kuliko kuchangia, leo nilidhani ninaweza ku share mtazamo wangu kuhusu hilo swala la DAUDI BASHITE, Lakini sio kwa lengo kwamba kila mtu awe na mtizamo kama wangu ama kutafuta mvuto kwa mtu yeyote. Mvuto ninao kwa mke wangu na familia yangu na labda sehemu yangu ya kazi, siwezi kuhitaji mvuto hata kwa watu tusiofahamiana kama hapa jf ambapo majority tunatumia majina feki, maana naweza kuwa na argue na wewe hapa kumbe tupo ofisi moja ana next door, lakini with our fake names huo mvuto unaousema sijui unakuja vipi
 
Back
Top Bottom