Dr. Msafiri
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 471
- 154
Wahenga: 'Unapoishi nyumba ya vioo, usitupe mawe!'
Bila jiwe tungezipata taarifa za Stivu supastaa na Mama Wema....! Unajua wanazo clip nyingi za hao ndege unaosema wameruka...!kuhusu wauza madaya ya kulevya, kwanza naona arobanini zao hazijafikiwa kwani mbinu iliyotumika ilikua ya kurusha jiwe kwenye ndege wengi hivyo wakaruka wote. huwezi kumuambia muuza madawa ya kulevya kua Ijumaa nakuja kukagua madawa nyumabni kwako, kisha yeye awe kayaweka tu kwake akikusubiri uje kuyakamata na kumakamata na yy. Arobaini ya wauza madawa ya kulevya ikifika, wauzaji wataliaa na kusaga meno.
walioruka ni wengi. hata hivyo naunga mkono vita dhidi ya madawa ya kulevya na naunga mkono pia vita dhidi ya wanaonunua vyeti. wote ni wahalifu na wachukuliwe hatua. pia majambazi na wahalifu wengie wakamatweBila jiwe tungezipata taarifa za Stivu supastaa na Mama Wema....! Unajua wanazo clip nyingi za hao ndege unaosema wameruka...!
kwa upande wangu naaunga mkono vita dhidi ya:Nime jiuliza sana chanzo cha yote ni nini? Je ni RC wa dar, dawa za kulevya, au kutajwa hadharani kwa watu tulip justice tunawapenda? Jib ukipata utajijua wewe upo upande wa kupambana na madawa ya kulevya , au kupambana na vyeti fek, au kupambana na makonda.....mi sijui jibu langu nlisha pata..... Pia tuna jua ma drug diller wananguvu kubwa je unajua wanapambanaje na makonda au una fkir wange kaa kimya makonda aendelee kuharib Mishe zao kila mtu akitafakar jesh wanalotumia hawa ma drug diller tukipata jibu ndi tuwaze mengine.......tusije tukawa wanajesh wa kuwasaidia ma drug diller bila kujijua kwa sabab ya ushabiki.........!!!!!!!
Sawa kabisa umenena vema nasikia huyo ndugu alisoma Mucobs Moshi je kuna umbali gani kwenda hapo Moshi?Kuna vitu huwa sielewi hapa. Mwaka fulani ilitajwa orodha ya mafisadi wa elimu waliokuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge alikuwa Marehemu Mzee Samwel Sita (Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi, Amina), Spika akaingilia kati kusema PhD ya Dr. Mathayo David ilikuwa halali hivyo katajwa kimakosa, ila wengine wote waliobaki hakuwasemea mf, akina Dialo (Dr.), Merry Nagu (Dr.) nk. Lakini nakumbuka baada ya Mzee Sita kusema hivyo, TCU immediately walitoa tamko, ya kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kusema kama Degree ya mtu fulani ni feki ama vinginevyo na baada ya hapo hata vile vijarida na yule bwana aliyekuwa kinara wa ile scandal sijui walipotelea wapi.
Nirejee kwenye hii scandal maarufu ya Daudi Bashite Vs Paulo Makonda, tunazo taasisi zetu nyingi kuanzia hizo za kitaaluma alikopita huyo Ndg, anza secondary school both O level and Advanced Level, kuna walimu waliomfundisha, na baraza la Mtihani NECTA nk. Twende kwenye Chuo alichosoma tena hivi majuzi tu kote huko vyombo vya kiuchunguzi vinapajua na panafikika na sio wala nje ya nchi na hakuna gharama kihivyo.
Binafsi naamini kama hiyo ni kweli ni swala la muda tu, let us wait and see, lakini kama ni longo longo kwa nini tunapoteza muda wetu.
Kuna mkubwa mmoja katika taasisi moja hapa nchini, yeye alisema ana PhD, Chuo alichopata hiyo Degree yake SA, watu wakaanza kusema sema alikimbia mwenyewe ofisi, ingawa kiutendaji alikuwa mzuri kabisa na ni kweli aliwahi kufanya hiyo Degree yake huko SA ingawa haiku- materialize.
Kumbe basi ni swala la muda tu, maana tumeshudia watu wengi wakifutika humu makazini kama upepo na wengine wakistafu gafla, ukiuliza unaambiwa vyeti vina utata, hivyo basi kama jamaa naye kuna hila ipo siku ataondoka tu. Binafsi naamini kwa hizi kelele ambazo zimepigwa kuhusu Bashite vyombo vya uchunguzi vilikwisha maliza kukusanya taarifa kuanzia kijijini Kolomije, shuleni msingi na sekondari na hadi chuo.
Nikimwaangalia Makonda bado ni kijana kuliko mimi, lakini mimi nikienda shuleni kwangu msingi bado wapo walimu walionifundisha primary pale kituoni zaidi ya 20 yrs ago, ingawa wengine wamehama na wengine kustaafu, lakini hata wasipokuwepo taarifa zinapatikana tu. Sasa sembuse huyo, Jamani Sefue Ombeni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aliandikwa na Gazeti moja tu, akatoka akakanusha kwa nguvu zote juu ya ile taarifa na vitisho vya kwenda mahakamani na kudai fidia, mbona baada ya muda mfupi aliondoka. Ingawa sijui kama kuondoka kwake kulitokana na ile habari iliyooandikwa na lile gazeti, lakini walau ndio taarifa pekee ya mwisho iliyokuwa na ukakasi kumuhusu yeye binafsi na sio taasisi.
Mamlaka ya uteuzi wa Mkuu wa Mkoa (RC) ambayo ni Rais, ina mikono mirefu na mipana, ina macho mengi na yenye nguvu ya kuona kila sehemu, tuipe ushirikiano chanya katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku likiwemo hili la Daudi Bashite nadhani itatoa majibu nasi tutayaona hata pasipokuambiwa. Hizi kelele nyingi kupita kiasi zinaweza hata kuwapoteza na kuipuuzia hii taarifa kwa kuzani ni kelele za watu walioguswa na utendaji wa Ndg Makonda hasa kwenye dawa za kulevya.
Katika utendaji kazi wake hasa kwa siku za hivi karibuni kama Mkuu wa Mkoa Ndg Makonda sote tunajua amegusa eneo la watu wenye nguvu ya pesa chafu, majuzi nimeona comment ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, juu ya hii vita, kila mtu anajua nguvu ya hao watu, wanaweza fanya jambo lolote hasa kwa watu wa kawaida kama akina RCs nk, maana kuna nchi tunaambiwa hata President anaweza kupinduliwa na drug dealers, hivyo mimi kwa kutambua uwezo mkubwa wa watu walioguswa na RC Makonda hivi karibuni, nitakuwa wa mwisho kuamini kila baya linalozungumzwa kuhusu Makonda kwenye social media na kwingineko mpaka vyombo husika vitakapo toa taarifa aidha in public ama tukaona vitendo kama enzi ya kina Sefue nk. Mwanzoni kuanzia kule Bungeni tuliambiwa ana majumba ya Gorofa ndani mwaka mmoja nk, leo havisemwi tena.
Mwisho kabisa, natamani kuona vyombo vyetu (Responsible Institution) zikifanya kazi yake kwa umakini na kutoa taarifa sehemu husika kwa utekelezaji na sio vinginevyo. Ahsante
kazi tunafanya na kazi zingine ndio hizi za kufichua wahalifu. hatuwezi kuishi na wahalifu na kuwaficha.
kwakua yeye kakosa namna ya kujitetea, basi mamalaka zinazohusika zitumie muda mfupi kuchunguza. uhakiki wa vyeti Tanzania nzima haukuchukua zaidi miezi miwili, kumbe uhaakiki wa kumahakiki Makonda utatumia wiki moja tu na kila kitu kitakua wazi.
Mama Daudi, kamuhudie Daudi. alishatoka kanisani kulia na kwa mshekh kuombewa dua.Napita naona bado umo, utapasuka kichwa na ulipoguswa juu ya Mh. Makonda. Hahaaaaaa, unakazanaaaaa watu wakubali, hiyo imetokaaaaa
Hotuba ya Mh. JPM hujuhisikia juzi re kelele za vyeti unavyokazania? Hahahahaaaaaa
Hiyo media wameibania haswaaa, ili wazidi juona wivu na tamaa za watu zinavyoongezeka na wanaovunja sheria wajitokeze nao wauze magazeti yao hahahaaaaaaa
Makonda oyeeeeeeeee
Wewe pumzika sisi tunaendelea...Jamani naona tunajadili sana suala LA Bashite tukiamini hatua zitachukuliwa dhidi take. Lakini kwa muda muziki juu Wa Bashite umeanza kuimbwa Sizonje angekwisha xhukua hatua. Mi naomba tuache mjadala tuendelee na kazi zetu Sizonje hawezi kumtoa
Wewe wacha sisi hatuachiHili suala ni nyeti sana lakini wakuu wamekaa kimya kuna kitu wanakipanga jaman hebu tuwaache