Sakata la viroba: Wafanyabiashara nendeni Mahakamani

Sakata la viroba: Wafanyabiashara nendeni Mahakamani

Kweli kabisa..

Waathirika waende mahakamani mara moja na huko lazima watapata haki yao.

Moja wapo ya umaarufu wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano ni UKATILI na UKURUPUKAJI..

Pia serikali hii ni maarufu kwa KUSHINDWA mahakamani.
 
Leta ushahidi kuwa lengo la serikali ni kuwafirisi....else mods naomba mfunge huu uzi na Polisi mkamateni huyu mfanyabiashara wa kariakoo kwa uchochezi.

Acha ujinga wa kitoto hii ni nchi huru, kila mtu anayo haki ya kueleza hisia zake bila kuvunja sheria. kuna kosa gani alilofanya kuhoji uhalali wa kadhia hii inayoendelea? yuko sahihi kwani serikali haikuchukua kodi ya viroba? kama walichukua kodi je wamerudisha kwa wahusika?
 
Kupewa siku kumi tu kumaliza viroba vyote mtaani haikubaliki...........viwanda huenda vina stock ya mwezi mzima alafu uwape siku kumi na huku wamelipa kodi..........Serikali itafaari upya siyo ndiyo mzee tu
 
Unajiuliza walitumia sheria gani kupiga marufuku utengenezaji,usambazaji na uuzaji wa bidhaa ambayo awali ilikuwa inatambulika kuwa ni halali kisheria na serikali ilikuwa inakusanya kodi inayotokana na mauzo ya bidhaa hiyo na hupati jibu.

Nilitarajia ingetungwa sheria ya kupiga marufuku hii biashara ya viroba na hapo hapo wafanyabiashara hawa wangepewa muda wauze stock zao au ziharibiwe na serikali iwafidie lakini sio hivi walivyowafanyia.
Do first, think later...shikamoo mwendo kasi.
 
Mkuu, kwani hujui kuwa hao wafanyabiashara walienda Mahakamani na jana imetolewa hukumu kuwa kesi yao imefutwa kutokana na kukiuka masharti wakati wa kufungua? By the way tangazo la kuzuia vifungashio vya pombe kwenye mifuko ya Plastic lilitolewa tangu mwezi Mei 2016. Walipewa muda wa kutosha. Sema Mtaa wa Ufipa mnapenda kutetea kila ujinga. Mmetetea wauza sembe na sasa mnawatetea wauza Viroba
 
Kupewa siku kumi tu kumaliza viroba vyote mtaani haikubaliki...........viwanda huenda vina stock ya mwezi mzima alafu uwape siku kumi na huku wamelipa kodi..........Serikali itafaari upya siyo ndiyo mzee tu
Mkuu, hao jamaa wauza viroba washenzi sana. Tangu mwezi Mei mwaka jana waliambiwa kuwa ifikapo tarehe 1 Machi 2017, biashara ya viroba iwe imekufa. wao wamekuwa wakaidi na ndio maana wamepigwa kirahisi mahakamani
 
Wewe mimi sibishani na WAPUUZI kama wewe......KWA MTU MWENYE AKILI KAMWE HAWEZI ANGALIA MASLAI YA WACHACHE NA KUWAACHA WENGI WA KIUMIA......acheni kuvuta bangi nakutumika kipuuzi
Hili halina tofauti na biashara ya madawa ya kulevya
 
Lunapokuja suala la afya na Ustawi...tusipende kujali wafanya biashara eti kwakuwa wameinvest...ktk business plan IPO sehemu ya kutegemea Risks na sehemu ya THREATS....hizo zikiangaliwa vema ktk uwekezaji basi wafanya biashara hawa wasingeshangaa maamuzi ya serikali....na kwa uzoefu kidogo hapa nchini hakuna mda wa kutosha kuwapa wafanya biashara ili kuanza kutekeleza, tumezoea sharti likitoka watu wanasikilizia hadi serikali ianze kutekeleza...tofauti na uongozi uliopita...sasaivi sharti likitoka ni kweli utekelezaji...mfano kuna sehemu viroba vimekamatwa vikiwa ktk process ya kutangenezwa...wakati ni baada ya tarehe ya mwisho....kubalini hasara kama hasara zingine...

Swali ingekuwa bidhaa zingine feki huwa wanateketeza kwa moto, hizi pombe sio feki ila ziko ktk viroba serikali itavifanyeje?
 
wewe lazima ni kiongozi muandamizi toka chadema umesahau kuandika kwamba wamtafute na Lissu awe wakili wao mkuu ungebamba kinoma kwa wauza unga wenzio
 
nyie mna laana....NAONA ufipa sasa AROSTO ZA VIROBA zinaanza kuwakabili ipasavyo......
HATA HILI LA VIROBA mna tetea kweli jamani....mnakiaibisha chama chenu....n mnakipa wakati mgumu sana kuja kujisafisha kwa WANANCHI......
Nyie badala ya kupaza sauti zenu BEN apatikane mnaanza kutetea UJINGA......
Madhara ya viroba ndio mmeyajua leo.Wakati mnaruhusu hii biashara haya madhara mlikuwa hamuyajui?Mlikuwa hamkusanyi kodi?Kwanini msiwe wastaarabu kwa kuziharibu hidhi bidhaa na kisha kuwalipa wafanyabiashara hawa fidia?

Mliwashirikisha wafanyabiashara katika kufikia huu uamuzi?Busara ya uongozi iko wapi hapa?

Mnapenda sifa za kisiasa hata kama ni kwa kufanya mambo ya kijinga.
 
Acha kuwa mjinga na mnafiki.Madhara ya viroba ndio mmeyajua leo.Wakati mnaruhusu hii biashara haya madhara mlikuwa hamuyajui?Mlikuwa hamkusanyi kodi?Kwanini msiwe wastaarabu kwa kuziharibu hidhi bidhaa na kisha kuwalipa wafanyabiashara hawa fidia?

Mliwashirikisha wafanyabiashara katika kufikia huu uamuzi?Busara ya uongozi iko wapi hapa?

Mnapenda sifa za kisiasa hata kama ni kwa kufanya mambo ya kijinga.
MWAMBIENI LISSU awasaidie kufungua kesi MAHAKAMANI.........
 
Lazima wana makosa kisheria, na wanalijua hilo ndio maana wamenyamaza.
 
Hawa wanaoanza kupinga watwambie tofauti ya Viroba na konyagi za Chupa,mnapinga upumbavu bila kujiuliza,zile grants unajua zina ukali gani,hapa tatizo zio Viroba ni uchafuzi wa mazingira na zaidi tumeipa thamani kubwa gongo.
 
wewe lazima ni kiongozi muandamizi toka chadema umesahau kuandika kwamba wamtafute na Lissu awe wakili wao mkuu ungebamba kinoma kwa wauza unga wenzio
Kwa kukurupaka kwenu hawa jamaa wataenda mahakamani na kesi mtashindwa na fidia mtawalipa kwa kutumia kodi zetu.

Sasa jiulize hii ndio akili!!
 
Wakuu , kwanza naomba kukiri kwamba mimi ni mfanyabiashara ( siuzi viroba wala pombe ya aina yoyote ) , hivyo ninafahamu gharama za uwekezaji wowote wa halali , haya wanayotendewa wauza viroba , wasambazaji na watengenezaji si sahihi na wala hakuna porojo zozote zinazoweza kuhalalisha jambo hili .

Lengo kuu hapa ni kuwafirisi wahusika , sababu za serikali kutaka kufirisi Raia wake bado hazijafahamika , nawashauri wafanyabiashara , wasambazi pamoja wenye viwanda nendeni mahakamani .

Uzoefu unaonyesha kwamba serikali ya awamu ya 5 haijawahi kuwa na huruma kwa raia wake , kwahiyo haya wanayoyasema na kuyapanga hawatanii , angalieni waliyotendewa wananchi wa Mkwajuni , Mahakama pekee ndio iliyokuja kuokoa wengine wa mabondeni wasidhalilishwe , kuna haja kubwa sana ya kwenda mahakamani sasa .

Ikumbukwe kwamba biashara ya viroba si haramu , na imekwisha lipiwa kodi na wahusika wote , Ni Mahakama pekee inayoweza kuweka utaratibu wa kumaliza kwanza mzigo uliopo sokoni kabla ya kufuata utaratibu mwingine .

Uoga ni umasikini
Kwakua wewe ni mkereketwa WA haki za wafanya biashara jiongeze sasa upeleke hiyo kesi mahakamani ili uonyeshe dhamira yako kwa vitendo.Hata hivyo sidhani kama wafanya biashara WA vinywaji walikua wanauza na kununua vinywaji aina ya package ya viroba pekee.Mantiki ya SERIKALI kupiga marufuku vinywaji vya aina hiyo kwenye vifungashio kama hivyo IPO na ina uzito ndiyo maana wahusika wametii bila shuruti.
 
Unajiuliza walitumia sheria gani kupiga marufuku utengenezaji,usambazaji na uuzaji wa bidhaa ambayo awali ilikuwa inatambulika kuwa ni halali kisheria na serikali ilikuwa inakusanya kodi inayotokana na mauzo ya bidhaa hiyo na hupati jibu.

Nilitarajia ingetungwa sheria ya kupiga marufuku hii biashara ya viroba na hapo hapo wafanyabiashara hawa wangepewa muda wa kutosha wauze stock zao au ziharibiwe na serikali iwafidie lakini sio hivi walivyowafanyia.
Hiyo siyo sahihi, yaani watu waendelee kunyweshwa kitu cha kuharibu miili na akili zao ili kuwapa mda wa kuendelea kuharibu akili na miili zaidi kwa faida ya nani?Kama kitu kimeonekana kua na madhara kwa umma ni budi kipigwe marufuku mara Moja.
 
Kwakua wewe ni mkereketwa WA haki za wafanya biashara jiongeze sasa upeleke hiyo kesi mahakamani ili uonyeshe dhamira yako kwa vitendo.Hata hivyo sidhani kama wafanya biashara WA vinywaji walikua wanauza na kununua vinywaji aina ya package ya viroba pekee.Mantiki ya SERIKALI kupiga marufuku vinywaji vya aina hiyo kwenye vifungashio kama hivyo IPO na ina uzito ndiyo maana wahusika wametii bila shuruti.
Nani kakudanganya kama wametii ?
 
Back
Top Bottom