Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,745
- 239,399
Wakuu , kwanza naomba kukiri kwamba mimi ni mfanyabiashara ( siuzi viroba wala pombe ya aina yoyote ) , hivyo ninafahamu gharama za uwekezaji wowote wa halali , haya wanayotendewa wauza viroba , wasambazaji na watengenezaji si sahihi na wala hakuna porojo zozote zinazoweza kuhalalisha jambo hili .
Lengo kuu hapa ni kuwafirisi wahusika , sababu za serikali kutaka kufirisi Raia wake bado hazijafahamika , nawashauri wafanyabiashara , wasambazaji pamoja na wenye viwanda nendeni mahakamani .
Uzoefu unaonyesha kwamba serikali ya awamu ya 5 haijawahi kuwa na huruma kwa raia wake , kwahiyo haya wanayoyasema na kuyapanga hawatanii , angalieni waliyotendewa wananchi wa Mkwajuni , Mahakama pekee ndio iliyokuja kuokoa wengine wa mabondeni wasidhalilishwe , kuna haja kubwa sana ya kwenda mahakamani sasa .
Ikumbukwe kwamba biashara ya viroba si haramu , na imekwisha lipiwa kodi na wahusika wote , Ni Mahakama pekee inayoweza kuweka utaratibu wa kumaliza kwanza mzigo uliopo sokoni kabla ya kufuata utaratibu mwingine .
Uoga ni umasikini