Sakata la viroba: Wafanyabiashara nendeni Mahakamani

Sakata la viroba: Wafanyabiashara nendeni Mahakamani

Sidhani kama unajua kilichokuwa ndani ya Viroba ni nini! Nenda kaulize wataalam (kemia) na Madaktari Muhimbili kwa nini magonjwa ya Figo na Ini yameongezeka kwa kiwango kikubwa miaka ya hivi karibuni!?
Hujanielewa mkuu wangu , sipingi kwamba pombe iliyowekwa ndani ya viroba ina madhara , la hasha , ninachotaka ujue ni kwamba kile kinywaji chenyewe hakijakatazwa , ndio maana konyagi ya kwenye chupa haijaguswa , kisichotakiwa ni kule kifungashio cha nylon tu .
 
Tatizo la watanzania tuna mizaha na kuleta siasa hata kwenye mambo ya msingi. Mleta uzi ameweka bayana hoja juu ya uamuzi wa serikali kuzuia viroba kwamba hakuna timeline ya kumaliza stock zao ambazo walilipia kodi na haijazingatia mitaji waliyowekeza kwa vyovyote vile watafisika kwani wengi wao wamekopa kwenye taasisi za fedha. Sasa tatizo hapo ni nini hasa?
 
Unajiuliza walitumia sheria gani kupiga marufuku utengenezaji,usambazaji na uuzaji wa bidhaa ambayo awali ilikuwa inatambulika kuwa ni halali kisheria na serikali ilikuwa inakusanya kodi inayotokana na mauzo ya bidhaa hiyo na hupati jibu.

Nilitarajia ingetungwa sheria ya kupiga marufuku hii biashara ya viroba na hapo hapo wafanyabiashara hawa wangepewa muda wa kutosha wauze stock zao au ziharibiwe na serikali iwafidie lakini sio hivi walivyowafanyia.
Awamu hii ya tano hakuna cha kufuata katiba wala sheria. Haki hiyo sasa wameibeba Rais na Waziri mkuu wake no more tanga tanga uone unavyofilisika.
Huyu akisema zuia viroba mwenzie anasema Dangote kachimbe mkaa wa mawe kadri unavyoweza huko Mbinga, hakuna anayehoji. Jamani mwaka huu tutaendeshwa kama nyumba ntobhu.
 
Acha kuwa mjinga na mnafiki.Madhara ya viroba ndio mmeyajua leo.Wakati mnaruhusu hii biashara haya madhara mlikuwa hamuyajui?Mlikuwa hamkusanyi kodi?Kwanini msiwe wastaarabu kwa kuziharibu hidhi bidhaa na kisha kuwalipa wafanyabiashara hawa fidia?

Mliwashirikisha wafanyabiashara katika kufikia huu uamuzi?Busara ya uongozi iko wapi hapa?

Mnapenda sifa za kisiasa hata kama ni kwa kufanya mambo ya kijinga.
Mkuu Wanaoshabikia hawaelewi kitu. kilichopigwa marufuku ni VIFINGASHIO VYA PLASTIKI wala siyo pombe yenyewe (CONTENT) wakisema ni bei ndogo,vinachafua mazingira eti wazalishaji watafute vifungashie vingine kama itakavyoamuliwa na serikali (Jan Makamba).Tangu lini haramu ikazaa halali kodi walipe,leseni walipe then unakuja kuchukua bidhaa zake na kufunga kiwanda ambacho kilikuwepo kisheria acha tuisome namba..Hata hawa majuha watakosa kodi ambazo ndo hela wanazotumia kuwahonga ile timu...onea na mwanao..
 
Kwan Tanzania ndy nchi yakwanza kuzuia viloba haya Zambia waliwai kuzuia lkn hawakupata hasara wafanyabiashara.na walipewa muda wakutosha kumalizia mzigo wao
 
Nionacho Mimi serikali inapiga marufuku vifungashio vya plastiki na wala sio pombe. Lengo lingekuwa kukipiga marufuku kilevi chenyewe nadhani wangezuia hata zilizo kwenye chupa.

Kwa mfano; Konyagi ipo ya kwenye chupa na vile vile ipo ya kwenye kifungashio cha plastiki (kiroba)

Valuer ipo ya chupa, pia ipo ya kiroba....

Hii vita inapambana na za kwenye vifuko vya plastiki wakati za kwenye chupa alcohol percentage ni sawa..??


USHAURI KWA WAFANYABIASHARA.

Kwakuwa kinachoonekana kupigwa vita ni vifungashio..njoeni na vifungashio vya aina nyingine visivyo vya plastiki..sio mbaya hata ikiwa kwenye vichupa vidogo kama vya dawa za sindano.
 
Vitisho vina mwisho. Ushahidi gani wakati hata matendo yanaonyesha!
Hivi wewe uko timamu?? Unaweza kumshtaki mtu au taasisi na kusema huitaji ushahidi sababu matendo yanaonyesha?
Ama kweli nimeamini we still have a long walk to freedom
 
Leta ushahidi kuwa lengo la serikali ni kuwafirisi....else mods naomba mfunge huu uzi na Polisi mkamateni huyu mfanyabiashara wa kariakoo kwa uchochezi.

Polisi kule Mahakamani jasho la mgongo linawatoka kwa utelezi wa kisheria wewe unawaongezea kesi nyingine ya uchochezi,
 
Leta ushahidi kuwa lengo la serikali ni kuwafirisi....else mods naomba mfunge huu uzi na Polisi mkamateni huyu mfanyabiashara wa kariakoo kwa uchochezi.
Kweli mkuu, siku hizi jambo litaambatanishwa na mambo mengi ya hovyo ilimradi waweze kupotosha uharisia na kucreate attention za wasiojielewa ili watetewe. Wafanyabiashara aina ya huyu ni bure kabisa, vitu vyenyewe unavyouza ni vileo lakini bado unajaribu kuhamasisha jamii ikuone mwema.
 
Mimi nina wasiwasi sana na kiwango cha weledi na busara za watu wanaomshauri rais.
Haiwezekani mtu kama Bashite / coke zero kuwa karibu kiasi kile na kuaminiwa mno na mkulu wakati amezungusha.
 
Kwan Tanzania ndy nchi yakwanza kuzuia viloba haya Zambia waliwai kuzuia lkn hawakupata hasara wafanyabiashara.na walipewa muda wakutosha kumalizia mzigo wao
Zambia viwanda vilipewa mwaka mmoja na wauzaji mwaka na miezi sita
 
Ukitaka kujua athari za hizi pombe nenda pale Muhimbili kitengo cha Figo itakusaidia kuelewa juu ya hili sakata mkuu. Achilia mbali wagonjwa wa Ini na magonjwa mengineyo yanayosababishwa na hizi pombe kali kwenye plastiki.
hyo inajulikana na athari zake!suala Mbn walikuwa wanachkua kodi

Ova
 
Wakuu , kwanza naomba kukiri kwamba mimi ni mfanyabiashara ( siuzi viroba wala pombe ya aina yoyote ) , hivyo ninafahamu gharama za uwekezaji wowote wa halali , haya wanayotendewa wauza viroba , wasambazaji na watengenezaji si sahihi na wala hakuna porojo zozote zinazoweza kuhalalisha jambo hili .

Lengo kuu hapa ni kuwafirisi wahusika , sababu za serikali kutaka kufirisi Raia wake bado hazijafahamika , nawashauri wafanyabiashara , wasambazi pamoja wenye viwanda nendeni mahakamani .

Uzoefu unaonyesha kwamba serikali ya awamu ya 5 haijawahi kuwa na huruma kwa raia wake , kwahiyo haya wanayoyasema na kuyapanga hawatanii , angalieni waliyotendewa wananchi wa Mkwajuni , Mahakama pekee ndio iliyokuja kuokoa wengine wa mabondeni wasidhalilishwe , kuna haja kubwa sana ya kwenda mahakamani sasa .

Ikumbukwe kwamba biashara ya viroba si haramu , na imekwisha lipiwa kodi na wahusika wote , Ni Mahakama pekee inayoweza kuweka utaratibu wa kumaliza kwanza mzigo uliopo sokoni kabla ya kufuata utaratibu mwingine .

Uoga ni umasikini
Ww ni mmojawapo kati ya wale wasitutakia mema Watz. Au kwenu mnaishi kwa kutegemea kuuza viroba eee???. Hv km nduguyo angekua mpiga viroba ungeandika hayo????.
 
hyo inajulikana na athari zake!suala Mbn walikuwa wanachkua kodi

Ova
Ili kufidia kwenye matibabu ya Figo na Ini mkuu. Ni janga la kitaifa,nashangaa kwa nini Wizara ya Afya haijatoa tamko au takwimu mpaka hivi sasa.
 
Tatizo la watanzania tuna mizaha na kuleta siasa hata kwenye mambo ya msingi. Mleta uzi ameweka bayana hoja juu ya uamuzi wa serikali kuzuia viroba kwamba hakuna timeline ya kumaliza stock zao ambazo walilipia kodi na haijazingatia mitaji waliyowekeza kwa vyovyote vile watafisika kwani wengi wao wamekopa kwenye taasisi za fedha. Sasa tatizo hapo ni nini hasa?
Ubarikiwe sana mkuu .
 
Ww ni mmojawapo kati ya wale wasitutakia mema Watz. Au kwenu mnaishi kwa kutegemea kuuza viroba eee???. Hv km nduguyo angekua mpiga viroba ungeandika hayo????. Nyoka Mkubwa weee
Nimejikuta nacheka tu !
 
Leta ushahidi kuwa lengo la serikali ni kuwafirisi....else mods naomba mfunge huu uzi na Polisi mkamateni huyu mfanyabiashara wa kariakoo kwa uchochezi.
Mkuu Duppy Conqueror, mleta mada ametoa maoni yake sioni mantiki ya kumshambulia kama ulivyofanya.

Ni ukweli uliodhahili kuwa hao watu waliwekeza mitaji mikubwa tu kwenye hiyo biashara ya kufungasha pombe katika mifuko ya plasitiki. Uwekezaji huo umehusisha vitendea kazi kama mashine za kufungashia hiyo pombe, kutengenezesha mifuko (vifungashio) pamoja na mambo mengine. Sasa unaposimamisha biashara ya huyu mtu katika mazingira ya haraka bila kumpa muda unatarajia nini kama si kwenda mahakamani kufungua kesi.
 
Mimi nina wasiwasi sana na kiwango cha weledi na busara za watu wanaomshauri rais.
Haiwezekani mtu kama Bashite / coke zero kuwa karibu kiasi kile na kuaminiwa mno na mkulu wakati amezungusha.
Janga kubwa sana .
 
Back
Top Bottom