Sakata la Usiku wa Oscars: Jada Smith avunja ukimya, Mauzo ya Show za Chris Rock yaongezeka

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,615
Baada ya kimya cha muda mfupi, hatimayeJada Pinkett Smith amevunja ukimya baada ya tukio la mumewe kumpiga kibao Chris Rock kwa kumfanyia mzaha katika usiku wa utoaji wa Tuzo za heshima za filamu, maarufu kama Oscars. Katika chapisho fupi katika mtandao wa Instagram, mwigizaji huyo aliandika juu ya "msimu wa uponyaji" akimaanisha tukio la Oscars.

Mapema wiki hii Mumewe, Will Smith, alilaaniwa na waandaji wa tuzo na watazamaji hizo kwa kumshambulia stejini Chris Rock kwa kile kilichodhaniwa ni kushindwa kustahimili utani dhidi ya mkewe. Aliomba msamaha siku ya Jumatatu, akiitaja tukio hilo la vurugu kama "sumu na uharibifu". Tukio hilo la Jumapili usiku lilitokea kabla tu ya Smith kutangazwa Mshindi wa tuzo ya Oscar ya Muigizaji Bora, kupitia Dcumentary ya King Richard.Ikiwa ni tuzo yake ya kwanza kabisa tokea kuanzishwa kwa tuzo hizo

Chris Rock alifanya mzaha kuhusu muonekano wa kichwa cha Jada Pinkett Smith (akirejea filamu ya G.I Jane), matokeo ya hali ya upotezaji wa nywele kutokana na ugonjwa ujulikanao kama Alopecia, Pinkett Smith hakutoa maoni yake huku kukiwa na mzozo mkali na mjadala wa hadharani uliofuata kuhusu utani wa Rock na vitendo vya Smith hadi Jumanne, akichapisha kwenye Instagram: "Huu ni msimu wa uponyaji na niko hapa kwa ajili yake".

1648633587129.jpeg

Je tukio hilo litamnufaisha Chris Rock?

Rock bado hajatoa maoni yake hadharani juu ya kile kilichotokea kwenye tuzo za Oscar au msamaha wa Smith.

Hata hivyo, mauzo ya tiketi za maonyesho yake yajayo ya vichekesho yameripotiwa kupanda kutokana na tukio hilo la Jumapili. Tovuti moja ya tikiti za hafla ya moja kwa moja, TickPick, ilisema Jumatatu kwamba iliuza tiketi nyingi usiku uliopita kuliko ilivyokuwa katika mwezi uliopita zikiwa zimeunganishwa.

Msemaji pia aliiambia CBS kwamba bei za onyesho lijalo la Rock siku ya Jumatano huko Boston zilipanda kutoka $46 (£35.16) hadi $411 (£314). Zaidi ya nusu ya mauzo yote ya tiketi kwa ziara ya Rock - ambayo ilianza kuuzwa mwezi mmoja uliopita - ilikuja baada ya tukio la Oscars. Idadi kubwa - 88% - ya mauzo ya tiketi za maonyesho ya Rock kwenye mtandao wiki iliyopita yalikuja baada ya tukio hilo.

Muda mfupi baada ya kipigo hicho cha jukwaani, Smith alishinda tuzo yake ya kwanza kabisa ya Oscar kwa uigizaji wake wa Richard Williams, Baba wa nyota wa tenisi duniani Venus na Serena Williams. Will Smith alimtaja Bwana Williams katika hotuba yake (baaada ya kupokea tuzo) akimwita "mtetezi mkali wa familia yake".

Mnamo Jumatatu, Bwana Williams alilaani kitendo cha ushambulizi wa Smith na kueleza kushangazwa na tukio hilo.

"Hatujui undani wa kile kilichotokea," aliwaambia NBC kupitia mtoto wake, Chavoita LeSane. "Lakini hatuungi mkono mtu yeyote kumpiga mtu mwingine isipokuwa ni katika kujilinda."


1648633520651.jpeg
 
Will naye anazingua tu, ana moyo wa kustahimili mke wake kuliwa lakini anashindwa kustahimili utani tu kwa mkewe
Chris itabdi naye akamle tu Jada apunguze uchungu
Kwahiyo km mkewe analiwa nje, ndo adhalilishwe vile?

Kwan pale alitania au alikua anamsimanga na kumdhalilisha?

Haya nawee nikuulize, mkeo akiwa analiwa nje ndo asimangwe mbele yako tena hadharan utafurahia tyuuh?

Kheeeh makubwa tena uwiiiiih
 
Ningekuwa Chris pale will smith ananiambia ''keep my wife out of your mouth" ningemuuliza
"So you don't want your wife in my mouth but are totally okay with My dik being in your wife's mouth?"
Weeeee! Nadhan makubwa zaidi yangetokea
 
Back
Top Bottom