Sakata la umeme nchini sasa limeingia ktk sura nyingine - LUKU

Nimelala giza kila nikinunua umeme naambiwa wapo kwenye matengenezo....natamani kuivunja vunja hiyo luku...
 
Kwanini ujiumize kukimbilia matatizo?
Siku Upinzani wakijipanga, wakawa na sera za maana na zenye tija..nitawaunga mkono!
Mtu mwenye akili zako huwezi kusupport vyama vya kuhuni kama CDM!

Kwa hiyo kwako wewe sera nzuri ni:

Ufisadi
wizi wa maliasili za nchi
mikataba mibovu kila sekta
EPA
TRL
MEREMETA + KAGODA
KIWIRA
UKOSEFU WA UMEME, MAJI
MFUMUKO WA BEI KILA KUKICHA
KUKITHIRI KWA RUSHWA KILA KONA

Kwa hiyo sera hizo ndiyo zimekufurahisha sana wewe ukajiona una akili zako!!!???? Pumba kabisa
 
utalia sana!!!
ikifika wakati wa kulia, kilio kitakujia kama radi, hutakisoma humu!
Mjusi gurugunda hufurahia jua lichangamshalo mgongo wake, wala hashtuki linapochoma nyama yake.
Mjusi gurugunda.
 
Nakumbuka baada ya uchaguzi mkuu! Kuna thread humu zilizungumzia yatakayotokea baada ya mkuu wa kaya kushika usukani magogoni, bei juu kila kitu chini kimpangilio na haya ndo yametokea! Mweeeeeeeeeeeeee!!
 
Habari za asubuhi wana jamii wenzangu, hivi.mna habari kuwa kama tatizo halitatatuliwa Leo itakuwa ni siku ya nne tangu kukosekana kwa mauzo ya umeme nchi nzima...na sababu network hakuna.

Hii nimeshuhudia mwenyewe jana mara baada ya kuzunguka.mji mzima na kukuta kundi la watu wakisubiri huduma ambayo haijulikani itapatikana au laa...hali watu wakiwa wenye hasira kali walilaani na kutoa maneno makali sana jambo ambalo hata mimi nilijikuta napandwa na hasira juu ya sirikali hii ambayo kimsingi inaonekana wazi imevurugika na kukosa.mwelekeo, ambapo sasa naweza kusema kuwa, pamoja na kuwa na mgao mkali wa umeme bado hata upatikanaji wa umeme huo mdogo ni wakusuasua.

Hivi unapokwenda kununua umeme halafu unaambiwa network hakuna, inakuja na kuondoka....jambo lakusikitisha sana, jana nikiwa katika kuhangaika kutafuta umeme nilikutana na shuuda mmoja aliyekuwa anatafuta umeme tangu majuzi na Lu.ishuhudia kuwa hawa mawakala wanaouza umeme wa luku wamekuwa wakidai rushwa ili mtu apewe favour Kila network inaporudi na wamekuwa wakitoa 5000/- . Hii imenisikitisha sana sana.
Sijui siku ya leo itakuwaje Ndigu zangu ila habari ndo hiyo.

Wewe umaifanyia nini serikali zaidi ya kuilaumu kila kukicha? Hata mtandao mkishindwa muumanage mnataka Rais aje kuutengeneza? Yeye sikisha wawekea mkonga wa kisasa kabisa? Au mnataka aje kuwaunganishia na kwenye Luku?

Unapoona kuna tatizo fikiria ni vipi utalitatuwa si kulalamika tu.
 
Hii serikali inakera sana matatizo chungu nzima leo hili kesho lile. Tumechoka na vimbwanga vyao ipo siku inakuja watalia na kusaga meno.
 
Wewe umaifanyia nini serikali zaidi ya kuilaumu kila kukicha? Hata mtandao mkishindwa muumanage mnataka Rais aje kuutengeneza? Yeye sikisha wawekea mkonga wa kisasa kabisa? Au mnataka aje kuwaunganishia na kwenye Luku?

Unapoona kuna tatizo fikiria ni vipi utalitatuwa si kulalamika tu.

Umerudi na matatizo yako yale yale. Pumba kabisa
 
Umerudi na matatizo yako yale yale. Pumba kabisa

Watu wenye maana wakiona tatizo huona "opportunities" zilizopo katika hilo tatizo na si kukaa kulalama kila wakati. Mnanshangaza.

Badala ya kulifanyia ubunifu tatizo.

Mfano watu wa IT hapa wangetazama namna ya kuweka data (localy) vituo vya Luku ambayo inamuwezesha mteja kupata umeme japo limited mpaka mitandao itaporudi na hizo data kuwa integrated centrally tatizo linapoondoka. System au program ambayo inawezekana kabisa.

Sio kukaa kulalama tu.
 
Hili la LUKU ni kero ya muda sasa.

Kero huondolewa kwa utatuzi na si kwa kulalama.

Nimewapa changa moto vijana wa IT (wenye kufikiri wataelewa). Waje na program simple ya ku collect na ku retain data localy wakati wa matatizo ya mtandao na hiyo program iweze ku update data centrally (sync) wakati mtandao unarudi.

Tanesco watapata biashara, wateja hawatakosa umeme kwa kuwa mtandao hakuna na ataeitengeneza software ataiuza. Win win solution.

Kama kuna mtu wa IT anaweza kujaribu ani PM tuifanye hii project, mimi nipo tayari kutafuta finance.

Haya vijana, kazi kwenu.
 
Nasikitika kuwa sasa kimbilio hlipo kwani luku imekuwa issue kuanzia jana hadi leo. Wenyewe wanaona kawaida, uchumi kuendelea kudolara. Kwani umeme ukiwepo luku hamna eti mtandao haupo, luku zikiwepo umeme haupo> hivyo ndivyo mambo yanavyojichanganya ndani ya bongo. Nasikitika kuona TANESCO ina vyojichimbia kaburi na nani wa kuwazika. Raia wanapoteza muda mwaingi wakisaka mahali pa kupata luku. Kesho utagsikia nishati ya gas haipo kweli nchi ya JK ni ngumu sasa.
 
Tafadhali mimi nina swali dogo linahitaji majibu sahihi toka kwa wahusika hasa TANESCO, Serikali na CAG.

Fedha zinazokusanywa za LUKU zinawekwa Acount gani?

Zinafanya shughuli gani kwa maendeleo ya umeme nchini Tanzania, ni kiasi gani kilicho kusanywa hadi leo?

Tunaomba mchanganuo na majibu tafadhali.

Nawasilisha!
 
Bado nauliza kwenye bunge hizo fedha za LUKU zilijadiliwa kama mapato ya TANESCO????????? Kweli hizo fedha zipo au zipo kwenye mifuko ya watu???????
 
wewe jamaa maswali gani hayo? mbona sioni la maana ulilouliza, si kuna accounts zinaandaliwa mkuu. Labda ungeuliza kwa nini hiyo system ya luku haifanyi kazi. hayo mengine ni obvious, rudi darasa kidogo utaelewa.
 
wewe jamaa maswali gani hayo? mbona sioni la maana ulilouliza, si kuna accounts zinaandaliwa mkuu. Labda ungeuliza kwa nini hiyo system ya luku haifanyi kazi. hayo mengine ni obvious, rudi darasa kidogo utaelewa.
Hilo swali lina maana yake ndg yangu, mapato na matumizi ya TANESCO yako vipi????????? Uliona matumizi ya matanuzi ya Ngorongoro, mbona waziri alizuia safari za wakurugenzi!!!!!! Tunahitaji matumizi na mapato ya fedha za LUKU, MBONA NI RAHISI TUU tuwekewe hapa kwenye jamvi tujiridhishe bila hivyo kuna siri nzito inayofichwa isijulikane!!!!!!!!!!
 
Unaponuna LUKU ile vending station huwasiliana moja kwa moja na servers zizolizopo TANESCO na mwisho wa siku agent huenda kuchukua commision yake baada ya kuwasilisha mapato ya makusanyo ya LUKU alizouza. kwa hiyo ni mfumo ambao fedha zote hurudi TANESCO na agent anaambuliwa commision tu. Nadhani nimetoa mwanga kdg
 
Unaponuna LUKU ile vending station huwasiliana moja kwa moja na servers zizolizopo TANESCO na mwisho wa siku agent huenda kuchukua commision yake baada ya kuwasilisha mapato ya makusanyo ya LUKU alizouza. kwa hiyo ni mfumo ambao fedha zote hurudi TANESCO na agent anaambuliwa commision tu. Nadhani nimetoa mwanga kdg
Hayo makusanyo hayana shida ila fedha hizo zinaingia Acount ipi TANESCO na mapato yake hadi hii leo ni fedha ngapi, zinatumika vipi kwa maendeleo ya nchi hii?????????Bungeni kwenye budgeti ya TANESCO zilitajwa??? Mbona wenyewe TANESCO hawajajibu, hivi hawaingigi hapa JF?????
 
Hivi hawa tanesco katika hii teknolojia ya luku wamekulupa au vipi,mana siku 2 leo kila kituo cha mauzo network hakuna. Kama mmeshindwa matumizi ya hii teknolojia turudi kwenye mita zetu za zamani mana mnatutesa sana.
 
Back
Top Bottom