Sakata la Picha ya Mbunge wa Ngara Wananchi Wakana Kulazimishwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

SAKATA LA PICHA YA MBUNGE WA NGARA WANANCHI WAKANA KULAZIMISHWA

Wananchi na wakazi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamekanusha kulazimishwa kuweka picha ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Gerge Ruholo kwenye maeneo yao kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.

Wakiongea na mwandishi wa Wasafi Media Allawi Allawi kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza hisia zao kwa Mbunge wao na kueleza bayana kuwa wamefanya hivyo kwa mapenzi yao kwa Mbunge wao na sio kushurutishwa.

Amri Habibu maarufu kama Fundi Ustadhi ambaye ana Ofisi ya ushonaji wa nguo katika stendi kuu ya mabasi Wilaya ya Ngara amesema kuwa aliomba kupatiwa picha ya Mbunge huyo kwa Zaidi ya miezi miwili nyuma hii ni kutokana na kuvutiwa na shughuli za maendeleo ambazo Mbunge huyo anazifanya jimboni humo.

Wengine walioeleza hisa zao juu ya picha ya Mbunge ni pamoja na kijana Seti Mussa Feruzi Kinyozi mwanachama wa CHADEMA ambaye ameeleza kuvutiwa na kazi nzuri anayoifanya Mbunge Ndaisaba kwenye jimbo la Ngara ambapo amefafanua kuwa ameamua kwa hiari yake kuweka picha hiyo ofisini kwake.

Hata hivyo wasafi Media iliendelea kuwatafuta wafanyabiashara wengine ambao wameweka picha hizo kwenye maduka yao zikiwemo stationary huku wengine wakiendelea kuonyesha uhitaji wa picha hizo na kuomba waletewe.

“Mbunge wa Ngara asichonganishwe na Mhe. Rais kwasababu picha yake inawekwa na wananchi kwenye sehemu zao za biashara na nyumbani na sio kwenye taasisi za kiserikali” - Oscar Oscar, Mtangazaji Wasafi Media

Mzee wa kaliua Oscar Oscar anaesema yeye bado haoni tatizo kwa watu kuweka picha za Mbunge wa Ngara kwenye biashara na nyumba zao. "Sioni tatizo watu kuweka picha za Mbunge Ndaisaba"
 
Attachments

  • sddefaultcfrt.jpg
    sddefaultcfrt.jpg
    39.7 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-06-07 at 16.58.25.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-07 at 16.58.25.jpeg
    53.2 KB · Views: 5

SAKATA LA PICHA YA MBUNGE WA NGARA WANANCHI WAKANA KULAZIMISHWA

Wananchi na wakazi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamekanusha kulazimishwa kuweka picha ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Gerge Ruholo kwenye maeneo yao kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.

Wakiongea na mwandishi wa Wasafi Media Allawi Allawi kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza hisia zao kwa Mbunge wao na kueleza bayana kuwa wamefanya hivyo kwa mapenzi yao kwa Mbunge wao na sio kushurutishwa.

Amri Habibu maarufu kama Fundi Ustadhi ambaye ana Ofisi ya ushonaji wa nguo katika stendi kuu ya mabasi Wilaya ya Ngara amesema kuwa aliomba kupatiwa picha ya Mbunge huyo kwa Zaidi ya miezi miwili nyuma hii ni kutokana na kuvutiwa na shughuli za maendeleo ambazo Mbunge huyo anazifanya jimboni humo.

Wengine walioeleza hisa zao juu ya picha ya Mbunge ni pamoja na kijana Seti Mussa Feruzi Kinyozi mwanachama wa CHADEMA ambaye ameeleza kuvutiwa na kazi nzuri anayoifanya Mbunge Ndaisaba kwenye jimbo la Ngara ambapo amefafanua kuwa ameamua kwa hiari yake kuweka picha hiyo ofisini kwake.

Hata hivyo wasafi Media iliendelea kuwatafuta wafanyabiashara wengine ambao wameweka picha hizo kwenye maduka yao zikiwemo stationary huku wengine wakiendelea kuonyesha uhitaji wa picha hizo na kuomba waletewe.

“Mbunge wa Ngara asichonganishwe na Mhe. Rais kwasababu picha yake inawekwa na wananchi kwenye sehemu zao za biashara na nyumbani na sio kwenye taasisi za kiserikali” - Oscar Oscar, Mtangazaji Wasafi Media

Mzee wa kaliua Oscar Oscar anaesema yeye bado haoni tatizo kwa watu kuweka picha za Mbunge wa Ngara kwenye biashara na nyumba zao. "Sioni tatizo watu kuweka picha za Mbunge Ndaisaba"
Chadema ndio walikuwa nyuma ya hili

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom