1.
Sio kweli, mkataba umevuka ngazi zote muhimu umekwenda moja kwa moja kwa Rais, hilo usijaribu kuli-spin, hapa unachojaribu ku-spin ni kuwa eti huu mkataba kwenda huko CC ni kitu cha kawaida, hilo sio kweli mkataba umekwenda huko baada ya Nape kuupigia kelele, na wala haukwenda huko wenyewe ila ulienda straight kwa Rais,
Jaribu kuwa na aibu kidogo na hizi spin, wadhamini wote wameitwa mbele ya Rais wamekataa kuhusika na mkataba, mawakili wa serikali, CCM, na wa binafsi wamekataa kuidhinisha mkataba sasa unapitishwaje na CC?
Utaratibu wa mchakato wa CCM ungetakiwa kufanywa kabla ya kuupitisha mkataba bro hizo ndio kanuni, huendi kuchakata mkataba baada ya jengo kuanza tayari, mbona unatufanya na sisi hapa kama ni UV-CCM? Hebu kitaje ni chama gani duniani kinachoachia mkataba wa jengo linaanza kwanza halafu ndio kinafanya mchakato?
2.
1. Acha kujdanganya, ni lazima CC iatoe mapendekezo ya kwenda NEC kuhusu kufukuzwa kwa Nape, hayo maneno ya Nchimbi ya kujifanya anajua sana sio kanuni za CCM, kanuni za CCM ni lazima hii ishu ijadiliwe CC, ndio iende NEC ninaelewa kuwa kwa mawazo yako Nchimbi ni Mungu, lakini kanuni za CCM ni kwamba lazima hii ishu ikatazamwe CC, na ndivyo Nchimbi alivyokuwa ameagizwa na Rais, hiyo ni kanuni ya CCM kuwa lazima CC waiangalie hilo la Nape kufukuzwa, it has nothing to Nchimbi.
2. Mkataba umechunguzwa tayari na mawakili wengi tu tena mpaka independent kwa shinikizo la Rais, unless ameamua kujichanganya mwenyewe, maana juzi almkemea sana Mengi kuhusu maneno kama yako yaliyokuwepo Nipashe, sasa leo rais atageuka na kuupitisha, basi Nchimbi atakuwa ni very powerful man kama unavyoamini, lakini mimi ninaisubiri kesho in this.
3. Ulisema kwa jina la Fisadi Mtoto, sasa sielewi unapsoema ulisema kwa jina hili tena au?