Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Ili kuwe na fairness, ni lazima afuatiliwe huyu... ili tujue anatumia fedha au hoja? Hapa nyie mlio ndani ya hicho chama, kwenye huo umoja tunawategemea... au wote mnahongwa kwa pilau na vijisent? mana jana pia tulimsikia M Nnauye naye akijinadi. Si mbaya kama mtu ana sifa ya kuongoza na vision pia... si umaarufu kama wengi wengine tunaowajua. Tanzania hii nani atakuja kuiokoa?
 
[
Naomba unipe hizo Mbinu za Ushindi.na itakua faida kwa sisi sote tulio na nia ya kuingia katika holy alliance.
Mkuu nenda kwanza ugombee, ukishindwa njoo ulalamike kuwa umenyimwa kwa sababu wewe huna jina au sio mtoto wa kiongozi, lakini kama hujajaribu haya maneno mengi ya kukashifu watoto wa viongozi yanatoka wapi?

Hapa JF ninaamini kuwa kuna the best ya wananchi wa taifa letu, yaani watu wenye macho na wenye kuona karibu na mbali pia, sasa hiki kilio against watoto wa viongozi bila sababu, inaishia ku-create some serious questions kama some of us hapa we are for real!

Kwa sababu usiniambie leo kuwa ukitaka kuwa kiongozi wa chama chochote cha upinzani, ni kuenda na kuchukua fomu na kushinda uchaguzi, is that so? Ukitaka uongozi ni lazima utafute muda wa kuongea na viongozi wakupe mikakati, lakini vilio hata kujaribu bado, ni kijishusha hadhi na ku-reveal unyonge wetu wa kufikiri na kuonyesha kukata tamaa hata bila kujaribu that should never be a spirit ya wana-JF.
 
Rashidi HAKUTUIBIA waTanzania; yeye alikuwa mwanaume wa SHOKA tu. Huenda na Zainabu sio mwizi.

kawawa kahusika na ufisadi sana, ali pressure ma benki yafanye write off mikopo kama bad debts, mmoja wa watu waliochangia kifo cha benki za serikali.

Unasema nini?

January Makamba, Nape Nnauye, Zainab Kawawa, Vita Kawawa, Adam Malima, Hussein Mwinyi, Amani Karume, Ali Karume, Charles Nyerere, Rose Nyerere the list goes on.

Ukiambiwa Tanzania na CCM zina wenyewe utakataa?
 
Mkuu hatuhitaji ubaguzi katika taifa letu, hawa uliowataja ni wa-Tanzania kama sisi wote, maana hata hao wenye akili kuliko zetu mbona mtoto wa Bush ni rais wao?

Nenda ugombeee, ukishindwa kwa sababu hukuwa mtoto wa kiongozi basi uje utoe haya mashambulizi, Jf nilifikiri tunatakiwa kuongea na facts, au? Hii kurusha rusha majina mnawapa vichwa bure hawa watu, ambao ni kwanza ni watu kama sisi wengine wote, na wengi wao wana maisha magumu kuliko sisi wengi wananchi wa kawaida, leo kamuone Charle Nyeree, yuko hoi bin taabani,

kuwa kiongozi sio kushinda maisha ya binafsi, na sio lazima uwe mtoto wa kiongozi, halafu hawana huo ubavu kama tunavyawapa hapa, wangekuwa nao basi Nape angekuwa mwenyekiti UV-CCM, wakuu tujiamini na hasa sisi ni JF, tunapaswa kuwa na fikra kubwa kuliko hizi inferior minds za bila sababu,

kajaribuni kwanza! mkishindwa mje mseme ukweli kwa nini mmeshindwa!
 
Mkataba jengo la UVCCM wazidi kuwakoroga viongozi

*Makamba, Nchimbi wakwepa hoja za Nnauye
*Mwekezaji asogeza vifaa, aanza ujenzi
*Mkataba bado haujasainiwa hadi sasa
*Kamati Kuu kuujadili Julai 29 mwaka huu

Na Kizitto Noya
Mwananchi

SAKATA la utata katika mkataba wa ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa mwekezaji amekwishaanza kazi, wakati viongozi wa CCM wakidai kwamba mkataba haujasainiwa.

Wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Isaac, anasema kuwa vifaa vya ujenzi vimekwishawasili kwenye eneo la ujenzi kama sehemu ya matayarisho, Mwananchi imeshuhudia ujenzi halisi ukiwa umekwishaanza.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, licha ya juzi kusema kwamba, mkataba huo haujasainiwa, jana alishindwa kueleza sababu za mwekezaji huyo kusogeza vifaa eneo la ujenzi akisema kuwa hahusiki na masuala ya ujenzi, ila mkataba ambao ameona kuwa unafaa.

Makamba aliliambia gazeti hili kuwa, mkataba huo una manufaa kwa UVCCM ila hawezi kuzungumzia suala la mwekezaji huyo kusogeza vifaa kabla ya kusainiwa kwa mkataba huo kwani halimhusu.

''Mimi ninachosema, mkataba huo una manufaa kwa UVCCM, kuanza ujenzi ni suala lingine ambalo mimi sihusiki nalo, unaweza kuwapigia wenyewe (UVCCM) waseme kwa nini mwekezaji huyo amesogeza vifaa wakati mkataba haujasainiwa,'' alisema Makamba na kuongeza:

''Ujenzi ni suala la kiufundi, linahitaji vibali na kuthibitishwa na mamlaka mbalimbali siwezi kuzungumzia hilo na ukitaka waulize wenyewe watoe majibu."

Mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Dk Emmanuel Nchimbi, alikwepa kuzungumzia utata huo kwa maelezo kuwa, yeye sio mtendaji wa taasisi, bali kiongozi wa vikao vya taasisi hiyo.

Nchimbi alimtaka mwandishi wa habari hii kuwasiliana na watendaji wa UVCCM kwa maelezo zaidi kwa kuwa ndio wasimamizi wa shughuli za kila siku za jumuiya hiyo.

"Mimi sio mtendaji wa taasisi, kazi yangu ni kuongoza vikao uwatafute watendaji watakuwa na majibu ya swali hilo," alisema Nchimbi na kukata simu.

Alipotakiwa kueleza sababu za mwekezaji huyo kusogeza vifaa vyake katika eneo la ujenzi kabla mkataba huo haujasainiwa, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Isaac alisema suala hilo ni la kawaida katika mikataba.

Alisema mwekezaji huyo amefanya hivyo kama sehemu ya maandalizi ya kuanza kazi na jambo hilo ni la kawaida na lipo kwenye hadidu rejea za mkataba huo utakaosainiwa.

"Huwezi kusaini mkataba wakati mwekezaji hajaleta vifaa kwa sababu kuna mambo mengi, moja ni kusaini mkataba na mtu ambaye hana uwezo na suala hilo lipo kwenye Memorandum of Understanding."

Alipoulizwa endapo Jumuiya itakuwa na wajibu gani kama wajumbe wataghairi kuingia mkataba huo, Isaac alisema, kimsingi jumuiya haina gharama yoyote zaidi ya mwekezaji huyo kuondoa vifaa vyake.

"We are very careful (tuko makini sana), tatizo ni watu kutofuatilia data (kumbukumbu) na kutafuta kura kwa njia ambayo sio sahihi," alisema Isaac.

Isaac jana kama ilivyo kwa Makamba, alisema kwamba mwekezaji katika jengo jipya anasubiri kusainiwa kwa mkataba baada ya kikao cha Kamati Kuu mwishoni mwa mwezi huu.

Viongozi hao wakishikilia kwamba mkataba unasubiri kusainiwa, harakati za ujenzi zimepamba moto kinyume cha madai kwamba, mwekezaji anakusanya vifaa vya ujenzi akisubiri kusainiwa kwa mkataba.

Mkataba huo umekwisha kuamsha mvutano mkubwa ndani ya UVCCM na Makamba juzi alizungumza na gazeti la Uhuru akimtuhumu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Nnape Nnauye, kwamba amewakosea wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya UVCCM kwa kubariki mkataba huo alioueleza kuwa na harufu ya kifisadi.

Nnauye ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, Jumanne iliyopita aliwashambulia Mwenyekiti wa Bodi, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa UVCCM, Dk Emmanuel Nchimbi na Kaimu Katibu Mkuu Isaac akiwahusisha na mkataba huo aliouita tata.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM, Nnauye aliwataka viongozi hao kuwajibika kwa kuwa wamehusika moja kwa moja na mkataba huo mbovu.

Alisema, viongozi hao wanapaswa kuwajibika kwani mkataba huo ni tata kwa kuwa moja ya vipengele vyake kinasema, utakuwa wa maisha na mwekezaji atamiliki asilimia 75 ya hisa wakati UVCCM itamiliki asilimia 25 tu.

Nnauye pia alisema utata mwingine katika mkataba huo ni mwekezaji kutumia hati za jengo la UVCCM kuomba fedha za kazi hiyo kutoka benki, badala ya kutumia mtaji wake, jambo alilosema kuwa lingeweza kufanywa hata na jumuiya yenyewe.

Alisema, Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, kwa mamlaka yake ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya UVCCM na wenzake Nchimbi na Isaac, wangeweza kuzuia suala hilo kwa kuwa ndio wenye jukumu la kusimamia mali za Jumuiya hiyo.

Hata hivyo, hoja ya Nnauye ilipata pingamizi kutoka kwa mgombea mwingine wa nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM taifa, Hussein Bashe, ambaye alimlaumu kwa kuwashambulia viongozi hao na kuwahusisha na utata katika mkataba huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kabla na baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo, Bashe alimtaka Nnauye kuwajibika kwa kujiuzulu nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu na Baraza Kuu la CCM, badala ya kuwataka viongozi hao kuchukua hatua hiyo kwa kuwa naye alishiriki kwenye maamuzi kwa mujibu wa nafasi yake.

"Kitu kikiamriwa na kamati, kinatakiwa kuwa collective responsibility (uwajibikaji wa pamoja). Iweje, Nnauye aseme hilo leo miezi saba baada ya maamuzi ambayo pia alishiriki?" alihoji Bashe.

Nnauye ambaye baada ya kauli hiyo aliitwa na Katibu Mkuu wa CCM, aliliambia gazeti hili jana kuwa ingawa hapendi kuendeleza malumbano juu ya suala hilo kutokana na heshima aliyonayo kwa Makamba, bado anasisitiza kuwa mkataba huo ni mbovu na viongozi hao wanatakiwa kuwajibika.

Alisema hawezi kujiuzulu nafasi zake za ujumbe wa Halmashauri na Baraza Kuu la CCM kwa kuwa msimamo huo alianza kuuonyesha tangu awali kwa kushawishi Baraza Kuu kuishinikiza kamati ya utendaji irekebishe upungufu huo bila mafanikio.

"Nisengependa kuendeleza malumbano hayo kwani Makamba ni mzee wangu, lakini kwa kuwa watu wananitaka nijiuzulu, nasema siwezi kufanya hivyo kwa kuwa msimamo wangu niliuonyesha kwenye vikao halali bila mafanikio," alisema.

Nnauye jana aliendelea kuhoji sababu za mwekezaji huyo kusogeza vifaa eneo la ujenzi endapo mkataba huo haujasainiwa kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi hao wa CCM akiwamo Makamba.
 
Sasa Bongo usije ukashangaa kesho wanabadili sheria na kuwa nchi ya kutawaliwa na wafalme na malkia, angalau hata wenye siasa hizo wengine nchi zao zimeendelea, kwetu itakua MFALME waziri mkuu MTOTO wa mfalme. Usicheze mbali mwanangu, UGALI NUSU!
 
Nimesoma mtu mwingine wa SUMATRA Bi Mbwala eti anakataa magari ya abiria yaliyo tumika zaidi ya miaka mitano ulaya eti yasiingizwe Tanzania. Mimi nadhani serikali kabla yakuwapa majukumu watu kama akina Bi Mbwala iwalete huku ulaya waoshe macho waone yapo magari ya miaka mingapi ambayo yanatumika kwa usafiri wa abiria Ulaya. Swala sio magari yazamani Jamani. Uwepo mpango mahususi wa kukagua magari na madereva! Tatizo RUSHWA.

Posted by: Mambo Jambo
Original Content:
Mi nashauri wote tumpe support, kama kuna wana ccm tafadhari mchagueni Ridhiwani JK.
Nawaomba sana, kwa kuwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza ccm tayari kulitumbukiza ardhini.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hatuhitaji ubaguzi katika taifa letu, hawa uliowataja ni wa-Tanzania kama sisi wote, maana hata hao wenye akili kuliko zetu mbona mtoto wa Bush ni rais wao?

Nenda ugombeee, ukishindwa kwa sababu hukuwa mtoto wa kiongozi basi uje utoe haya mashambulizi, Jf nilifikiri tunatakiwa kuongea na facts, au? Hii kurusha rusha majina mnawapa vichwa bure hawa watu, ambao ni kwanza ni watu kama sisi wengine wote, na wengi wao wana maisha magumu kuliko sisi wengi wananchi wa kawaida, leo kamuone Charle Nyeree, yuko hoi bin taabani,

kuwa kiongozi sio kushinda maisha ya binafsi, na sio lazima uwe mtoto wa kiongozi, halafu hawana huo ubavu kama tunavyawapa hapa, wangekuwa nao basi Nape angekuwa mwenyekiti UV-CCM, wakuu tujiamini na hasa sisi ni JF, tunapaswa kuwa na fikra kubwa kuliko hizi inferior minds za bila sababu,

kajaribuni kwanza! mkishindwa mje mseme ukweli kwa nini mmeshindwa!

Unajuaje kama sijagombea na kushindwa?
 
Sasa hapa ni mahali tunapokuja kupeana elimu, labda useme ulishindwaje, au ulishindwa na mtoto wa kiongozi aliyepewa bure bila kugombea?

Weka wazi hapa tuchambue, hapa ni JF mkuu huwa hatuogopi mtu ila tunataka hoja tu ili ipimwe!
 
Hakuna tatizo lolote kuzaliwa mtoto wa kiongozi, wala sio kuvunja sheria Tanzania ya sasa ni ubavu wa mwananchi tu, Zitto sio mtoto wa kiongozi, wala Dr. Slaa, tutafute mbinu na sisi tujitose,

Maana hivi vilio bila sababu za msingi, tutaishia kuwa sour grapes, Lowassa na Rostam sio watoto wa viongozi, mafisadi wanajulikana na sijui kama kuna mtoto hata mmoja wa official fisadi, ambaye ni kiongozi,

suala la ufisadi ni lazima tuliseme kwa mantiki yake, ama sivyo tunakuwa kama wananchi wa vijiweni, hasa baada ya kufahamika wazi kuwa kuna mpaka viongozi wa upinzani ambao wanapewa hela na mafisadi, na kwamba sio viongozi wote,

Tukachukue fomu za kugombea badala ya kukata tamaa, kila m-Tanzania anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote mradi tu anatimiza masharti ya anachogombea, ni suala la kufikiri kidogo tu kabla ya kurusha unfounded accusations, JF we are not anti-watoto wa viongozi kwa sababu tu ni watoto wa viongozi, maana mawazo ya namna hiyo ni mufilisi kama sio ulofa!

Kama maji ni ya shingo omba msaada utasaidiwa, lakini sio kulaumu tu bila sababu kwa sababu tu huwezi au mvivu wa kufikiri na kutenda kama viongozi wetu, na kama wewe huwezi haina maana kuwa wananchi wengine wote hatuwezi, wewe ni kukaa pembeni, maana kulia lia bila kujaribu watatuwala kweli hao mpaka kufa!

Suala la Zitto nililisoma hapa hapa kuwa ni mtoto wa fukara,sikuamini lakini ilitokea siku nikaambiwa kuwa huyu ndiye mama yake Zitto. jamaa akaniambia kuwa Zitto ni single parent kama alivyolelewa OBAMA lakini baya zaidi mama yake Zitto katika mihangaiko yake ya maisha amewahi kukaa gerezani kwa miezi sita Ukonga.

Zitto ametokea chini kabisa lakini mama yake ni mpiganaji mzuri katika harakati zake alihakikisha mtoto wake anasoma shule,kuna mengine siwezi kuyaandika hapa ili kumpa hadhi mbunge wetu ila ilipaswa Zitto Kabwe aandike kitabu cha maisha yake kama changamoto kwa wengine.

nachoweza kusema msiwe waogo wa kujaribu maisha, Obama angesema kuwa siwezi kugombea na Bill Clinton kwa vile ni mke wa kigogo na mume wake alikuwa rais mwenye kupendwa na zaidi ni pure mzungu, lakini Obama aliamini anaweza na ameweza. acheni uoga kuweni wajasiri kama mama yake Zitto Kabwe.
 
Mkuu hatuhitaji ubaguzi katika taifa letu, hawa uliowataja ni wa-Tanzania kama sisi wote, maana hata hao wenye akili kuliko zetu mbona mtoto wa Bush ni rais wao?

Nenda ugombeee, ukishindwa kwa sababu hukuwa mtoto wa kiongozi basi uje utoe haya mashambulizi, Jf nilifikiri tunatakiwa kuongea na facts, au? Hii kurusha rusha majina mnawapa vichwa bure hawa watu, ambao ni kwanza ni watu kama sisi wengine wote, na wengi wao wana maisha magumu kuliko sisi wengi wananchi wa kawaida, leo kamuone Charle Nyeree, yuko hoi bin taabani,

kuwa kiongozi sio kushinda maisha ya binafsi, na sio lazima uwe mtoto wa kiongozi, halafu hawana huo ubavu kama tunavyawapa hapa, wangekuwa nao basi Nape angekuwa mwenyekiti UV-CCM, wakuu tujiamini na hasa sisi ni JF, tunapaswa kuwa na fikra kubwa kuliko hizi inferior minds za bila sababu,

kajaribuni kwanza! mkishindwa mje mseme ukweli kwa nini mmeshindwa!

Ilikuwa zamani enzi ya awamu ya kwanza kulikuwa na maadili yanayoeleweka. Ilikuwa si rahisi mtu ama kiongozi kutumia madaraka yake kujinufaisha. Lakini kwa sasa hakuna tena maadili hayo. Vigogo wamekuwa wakitumia vyeo vyao kuwanufaisha watoto wao.
Tumeona wazi kwamba watoto wa vigogo hapa Tanzania ni miungu watu. Wanafanya watakavyo na hakuna wa kuwaambia kitu. Mfano Kinje

Kwa misingi hiyo si rahisi kwa mtoto wa masikini kuwa na sauti ama nafasi ndani ya chama tawala (CCM). Unaonaje kuhusu ajira BOT?.
 
[

Mkuu nenda kwanza ugombee, ukishindwa njoo ulalamike kuwa umenyimwa kwa sababu wewe huna jina au sio mtoto wa kiongozi, lakini kama hujajaribu haya maneno mengi ya kukashifu watoto wa viongozi yanatoka wapi?

Hapa JF ninaamini kuwa kuna the best ya wananchi wa taifa letu, yaani watu wenye macho na wenye kuona karibu na mbali pia, sasa hiki kilio against watoto wa viongozi bila sababu, inaishia ku-create some serious questions kama some of us hapa we are for real!

Kwa sababu usiniambie leo kuwa ukitaka kuwa kiongozi wa chama chochote cha upinzani, ni kuenda na kuchukua fomu na kushinda uchaguzi, is that so? Ukitaka uongozi ni lazima utafute muda wa kuongea na viongozi wakupe mikakati, lakini vilio hata kujaribu bado, ni kijishusha hadhi na ku-reveal unyonge wetu wa kufikiri na kuonyesha kukata tamaa hata bila kujaribu that should never be a spirit ya wana-JF.

Hapa issue ni uongozi huo wa UVccm.
Sasa kwa uelewa wangu ni kuwa huwezi kugombea nafasi hiyo kama wewe si mjumbe wa NEC...Na ndio maana nikasema wekeni majina ya wajumbe hao wa NEC hapa.
Kwani hakuna kiongozi wa ccm asiyetokea NEC.
Na wengine huchaguliwa si kwasababu ni watoto wa vigogo...Bali kwasababu wanaweza kuwasemea na kuleta upambe wa mipasho....

Mmmiliki wa TOT Plus Kapteni John Komba ambaye pia alichaguliwa kuwa mjumbe wa NEC pamoja na Khadija Kopa.
 
kuchaguliwa nafasi ccm ni kutizama kwa kiasi gani tu unajuulikana kwenye circle ya vigogo wa ccm

as long as wewe ni mtoto wa kigogo mmoja, basi njia ya kuingia madarakani imesha tengwa kwa ajili yako.
 
Lets be serious, ina maana huko UVCCM hakuna watu talented au wenye moyo na uwezo wa kuongoza mpaka awe yeye tu??? Je atasimamaje wakati kahusishwa na uchafu wa IMMA consult akiwa nafanya kazi na kampuni iliyosimamia mikataba hewa ya kifisadi??
 
Hii UVCCM Mwalimu aliianzisha ili kuwa na mtiririko mzuri wa viongozi wa baadaye wa Taifa hili. Vipaji vya uongozi vilianza kuonyeshwa hapa. Sasa imegeuzwa KIJIWE fulani hivi cha kupandia ngazi hata kama uongozi hauuwezi.
 
kuchaguliwa nafasi ccm ni kutizama kwa kiasi gani tu unajuulikana kwenye circle ya vigogo wa ccm

as long as wewe ni mtoto wa kigogo mmoja, basi njia ya kuingia madarakani imesha tengwa kwa ajili yako.

Mkuu I think its more than kuwa mtoto wa kigogo..vinginevyo Makamba na wengine wasingemkaripia Nape Nnauye vile walivyofanya...
May be kuwa mtoto wa kigogo ni advantage tu...
 
Ilikuwa zamani enzi ya awamu ya kwanza kulikuwa na maadili yanayoeleweka. Ilikuwa si rahisi mtu ama kiongozi kutumia madaraka yake kujinufaisha. Lakini kwa sasa hakuna tena maadili hayo. Vigogo wamekuwa wakitumia vyeo vyao kuwanufaisha watoto wao. Tumeona wazi kwamba watoto wa vigogo hapa Tanzania ni miungu watu. Wanafanya watakavyo na hakuna wa kuwaambia kitu. Mfano Kinje Kwa misingi hiyo si rahisi kwa mtoto wa masikini kuwa na sauti ama nafasi ndani ya chama tawala (CCM). Unaonaje kuhusu ajira BOT?.

Mkuu vilio kama hivi mimi ninaita ni vilio vya wananchi walioakta tamaa bila kujaribu na pia huwa vina-reveal inferiority ya mwananchi, kwa sababu yote hapa ni uzandiki mtupu hakuna ukweli,

Enzi za mwalimu watoto wengi wa viongozi walikuwa ni wadogo, sasa ndio wengi wao ni watu wazima ndio hivyo wamenaza kujitokeza kugombea uongozi, mambo mengine ni life reality ambayo hata uafnye nini huwazei badili, mimi kama ni mtoto wa kiongozi ninataka kugombea uongozi, wewe mtu wa nje kabisa na uongozi utanishindaje?

Kwenye hili noana kwa wale msiolielewa mtateseka sana maana simjui baba wa mtoto yoyote dunaini ambaye mtoto wake antaka kufanya kazi kama yake, halafu baba yake akamkatalia kumsaidia, lakini ninasubiri siku mwananchi mmoja hapa atakapoenda kujaribu akishindw akwa sababu ya mtoto wa kiongozi basi tutakubali, lakini hizi so far ni kelele za mlango tu!
 
Ni kazi kweli,simshauri agombee kwa sababu CCM haiendi kwa ukoo,akijiingiza tutayajua mengine ambayo labda hatukutakiwa kuyajua kwa wakati huu
 
Watarukaruka na kupinduana sana lakini dawa ni kuukabili ufisadi head on. Wakiamua kuendelea na vitisho na maneno ya blah blah, ufisadi utaendelea kushamiri na tuhuma hizi hazitaondoka kamwe
 
Nnauye anasema mambo mazito mahala pasipo! Namhurumia kwamba kwa kauli zake hizi, na kwa kawaida ya CCM, tayari ameshakwama.

Ila madai yake mengine pia ni mepesi kidogo; kusema kwamba Lowasa amefanya ufisadi kwenye hilo jengo kwa kuwa tu ni mwenyekiti wa bodi ya udhamini kunatia shaka umakini wake huyu bwana mdogo. It is very easy these days to make sweeping statements so that you are also seen to be hating or even fighting ufisadi. But such statements, as much as they may boost our politicians' popularity, they don't add any value to the real war against ufisadi!
 
Back
Top Bottom