Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Mpita njia,
Mkuu naomba umpe ukaribisho wa hapa jamvini kijana Nape.Najua atakubali na pia sina hakika kama si miongoni mwetu hapa
 
MwanaHalisi Toleo Na. 106

Rais Kikwete atapeliwa
Na Saed Kubenea

Ni katika mradi wa mabilioni
Edward Lowassa ahusishwa


Na Saed Kubenea
BARAZA la Wadhamini la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), limemtapeli Rais Jakaya Kikwete katika mradi wa mabilioni ya shilingi, MwanaHALISI limeelezwa.

Baraza la Wadhamini, chini ya mwenyekiti wake Edward Lowassa, limeingia ubia na mfanyabiashara Shubhash Patel kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa mabilioni ya shilingi kinyume cha taratibu, na rais hakupewa taarifa sahihi.

Mradi huo ni ule unaohusisha Jengo la Umoja wa Vijana uliopo Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam, kiwanja Na. 108/2.

Mgogoro uliopo ni kwamba wakati Baraza Kuu la UV-CCM limekataa mradi huo unaokadiriwa kuwa wa zaidi ya Sh. 12 bilioni, Baraza la Wadhamini, chini ya Lowassa, limeruhusu mradi kuendelea.

Tayari ujenzi wa kitegauchumi umeanza nyuma ya jego la sasa la makao makuu ya UV-CCM bila kuwepo hati maalum kuidhinisha ujenzi wa mradi.

Kwanza, hakuna mkataba kati ya UV-CCM na mwekezaji. Pili, Baraza Kuu la Vijana limekataa mradi huo. Tatu, Baraza la Wadhamini lililopitisha mradi huo halina mamlaka ya kufanya hivyo.

Jambo la nne, Kamati Kuu ya CCM haijajadili mradi huu na kuupitisha, na kwa vyovyote vile haiwezi kuepukwa.

Tano, kwa mujibu wa mkataba ambao haujasainiwa, na ambao ni msingi wa Baraza Kuu la UV-CCM kuukataa, ni kwamba inapendekezwa mwekezaji amiliki kitegauchumi bila ukomo.

Sita, na muhimu zaidi ni kwamba kauli za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba na zile za Rais Kikwete zinasigana kiasi kwamba inaonekana moja kwa moja kwamba Makamba anapinga mapendekezo ya rais ambayo kawaida huwa ni amri.

Saba, wawekezaji wanadai wamilikishwe ardhi ili waitumie hati kukopa fedha benki, jambo ambalo inadaiwa kuwa baadhi ya viongozi wa UV-CCM wanakubaliana nalo.

Hii ina maana kwamba "mwekezaji" hakuwa na fedha za kuwekeza isipokuwa alitaka kutumia hati kukopea fedha benki.

Imefahamika kwamba mwekezaji tayari ametumia Sh. 6 bilioni katika mradi wa ujenzi wa majengo mawili ya ghrorofa 25 kila moja.

Mradi mwingine unahohusiana na huo ni kukarabati jengo la sasa la UV-CCM ambamo "mwekezaji" – kwa mwaka wa pili sasa amefukuza wapangaji wote na kukosesha UV-CCM mapato yapatayo Sh. 7 milioni kila mwezi.

MwanaHALISI limeelezwa kuwa ni vurugu hizo zilizofanya Rais Kikwete kuagiza chama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.

Imeelezwa kuwa Kikwete alimwandikia Katibu Mkuu Makamba akimtaka kusimamia uchunguzi huo.

Kwa upande mwingine, Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM, ilimwandikia Makamba ikimtaka kufuatilia suala hilo, lakini katika hali ambayo haijaeleweka, Makamba hakuchukua hatua.

Kamati ya Maadili haikukata tamaa bali ilimwandikia Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mipango na Oganaizesheni, Kidawa Hamid Salehe wakati Makamba alipokuwa safari ya matibabu nchini India.

Taarifa zinasema Kidawa hakulikawiza suala hili. Alimwandikia Rais Kikwete na ilikuwa katika hatua hii, taarifa zikaanza kuvuja ndani na nje ya chama.

Baada ya Kikwete kupata taarifa ya Kidawa, alimwandikia Makamba akitaka wote waliohusika katika sakata hilo wahojiwe.

MwanaHALISI lina taarifa za uhakika kwamba tayari Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Lowassa amehojiwa juu ya kuhusika kwake.

Taarifa zinasema Lowassa amekubali kuwa baraza lake lilibariki mradi huo, lakini akasema lilishauri mkataba usisainiwe hadi Kamati Kuu (CC) ikubaliane nao.

Hata hivyo, wakati Lowassa anasema mradi usisainiwe mpaka kupatikana kwa kibali cha CC, tayari ujenzi wa mradi huo umeshaanza, jambo linalotafsriwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni utepeli kwa Kikwete.

"Hapa hakuna mradi. Kuna ufisadi. Mwekezaji atachukua asilimia 75 ya hisa, huku UV-CCM wakiambulia asilimia 25. Lakini kibaya zaidi, mwekezaji anaruhusiwa kuhamisha mpaka senti ya mwisho ya hisa zake," anasema mtoa taarifa.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, mwekezaji amemilikishwa kwa muda wote wa maisha yake, na kwamba anaruhusiwa kuhamishia hisa zake kwa mrithi wake kwa jinsi anavyoona inafaa.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia ujenzi ukiendelea kwenye sehemu ya mradi. Alipomuuliza Kaimu Katibu Mkuu wa UV-CCM, Francis Isack, iwapo mkataba tayari umesainiwa, alithibitisha ujenzi unaendelea lakini akamtaka mwandishi aende kukutana naye ofisini kwake.

Isack alisema mwandishi anaweza pia kumwona Katibu Mkuu Makamba kwa ufafanuzi zaidi.

Juhudi za akumpata Makamba hazikuweza kufanikiwa. Simu yake Na. 0784 483878 ilikuwa ikijibu kuwa haipatikani.

MwanaHALISI lilifanya juhudi pia kuwasiliana na Lowassa lakini simu yake Na. 0754 800000 iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Wachunguzi wa mambo wanasema mradi wa UV-CCM unaweza kuwagawa vijana na hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu katika umoja huo.
 
Last edited by a moderator:
Sasa ndo naanza kupata picha kwanini Makamba anamtetea sana Lowasa kwa kila Jambo
 
Mpita njia,
Mkuu naomba umpe ukaribisho wa hapa jamvini kijana Nape.Najua atakubali na pia sina hakika kama si miongoni mwetu hapa
Nape yupo hapa na amejaa tele..

iinvisible,Check your db..kuna watu nahisi wananusa nusa.....
 
Wandugu,

Naomba Cv ya Nnauye.

Zaidi ya kuwa ameshiriki kikamilifu kufungua Tawi ya CCM India, sijui kingine alichokifanya.

Pia, 2005 alikuwa kambi ya ip, Mtandau au ile zile nyingine?

Kitumia Neno Fisadi kunaweza kumuharibia; sababu CCM wanalikataa hili neno kwa sababu limeazishwa na Chadema.

huyu siyo mmoja wao,siyo mmoja wa wale wansohiriki ushirika usio mtakatifu.....nahisi ila naendelea kuhisi,ninaye mwamini kati ya ninaowafahamu amebaki kuwa zitto
 
I hope Nape hajachukua hela toka kwa Rostam, kama Mtikila,

Lakini otherwise ni mwanzo mzuri huu aliouanza, piga nyoka kichwani bila kujali where the chips may fall, Tanzania tunahitaji wanasiasa kama huyu bwana mdogo wanaoweza kuita Spade a Spade,

Sio akina Pinda, wanaotuambia Meremeta ni mali ya jeshi huyu kijana hata akishindwa tutajua ni uzembe wetu wananchi lakini ukweli uko wazi kuwa kwa mara nyingine tena Lowassa na Nchimbi, yaani wale wale ni mafisadi hata huko kwenye UV-CCM, sasa ni wakati wa wananchi werevu wa siasa kuanza kumpa msaada huyu kijana kwa sababu kwanza anajua mengi na atasema mengi sana mpaka huu uchaguzi uishe,

Mimi nitampa mchango wangu kumsaidia asonge mbele, maana huyu ana ubavu huyu wa kusema wazi, ambao wengi bongo hatuna, kuanzia wananchi mpaka viongozi wetu na hasa wanaotuambia kuwa Lowassa alionewa, so much na kuonewa, Fisadi bwana kila mahali yeye ni ufisadi!

Sasa wale watetezi wake Lowassa hapa vipi na hizi shutuma za Nape? Au naye ametumwa na Mwakyembe kumuonea Lowassa?

Bravo Nape!

Najua Pesa ya Nape inapotoka,Na nimekumbuka jambo moja zito sana..i will connect to the dot.. hivi karibuni,Do you know who was supposed to open CCM India Branch?

hawa wanompa pesa ndiyo wanamtuma hivi hakuna anyeweza akiwa peke yake?...
 
Inaonekana una siri moyoni mkuu Gembe. Sijui nani alitakiwa kufungua tawi la India lakini kama nakumbuka vema, alilifungua Samuel Sitta na akatoa mchango wa nadhani dola 500. Nape ndiye aliandika stori kuhusu tukio hilo na kuzisambaza kwenye newsroom karibu zote
 
Inaonekana una siri moyoni mkuu Gembe. Sijui nani alitakiwa kufungua tawi la India lakini kama nakumbuka vema, alilifungua Samuel Sitta na akatoa mchango wa nadhani dola 500. Nape ndiye aliandika stori kuhusu tukio hilo na kuzisambaza kwenye newsroom karibu zote
una uhakika sitta alikuwapo??
 
Subhash Patel ameonekana kwenye shughuli nyingi za fund raising ambazo JK amekuwa akihudhuria na kuna incidence kama mbili hivi Patel amewahi kupewa jukumu la kujenga darasa/madarasa kwa hela yake mwenyewe. Na aliyetoa jukumu hilo ni JK.

Makamba ana mahusiano ya karibu sana na Subhash Patel na sasa hivi jua linamchwea (karibu anaachia ngazi ya Katibu Mkuu wa CCM) kwa hiyo hapo lazima iko namna, watu wako mbioni kusaka mafao ya uzeeni, wanaogopa kuja kuwa kama akina Sozigwa ambao sasa hivi wanaishi maisha ya kubangaiza.

Makamba amekuwa akituhumiwa na wabunge wa CCM kwamba amekumbatia mafisadi na magazeti yaliwahi kuweka wazi kwamba Makamba was against Report ya Mwakyembe na hakutaka hata iwasilishwe Bungeni. Unganisha dots ......

Kamati ya Maadili ya CCM mwenyekiti ni AC na tuliona wazi alivyosimama Bungeni akipinga kuwasilishwa kwa report ya Mwakyembe. Hivi sasa yuko kwenye shimo refu sana ambalo anajua akijiweka kando ama akijifanya mnoko anaweza kuzama zaidi huko ndani na akapotea moja kwa moja, so the best option ni ku-side na likes wa kwake kama akina Lowassa na RA.

Kutokana na hayo mazingira hili swala litawekwa kapuni na sina hakika kama kuna hatua za maana zinaweza kuchukuliwa kwa wale wote waliohusika na huo ufisadi wa wazi.
 
una uhakika sitta alikuwapo??

Nadhani kuna picha pia za tukio hilo zilipigwa na kusambazwa kwenye blogs nyingi. Ngoja nizisake na unaweza kumuona Mzee Sitta akiwa mgeni rasmi kama sikosei.
 
Mkuu Gembe,

Nenda kwenye hii link: http://mjengwa.blogspot.com/2008/05/spika-sitta-afungua-tawi-la-ccm-mysore.html#comments

Sijui namna ya ku-upload pic na kuweka hapa. Ila kuna pic ya Mzee Sitta na chini ya picha kuna maelezo haya hapa:

Jana Tar 20/5/2008, tawi la CCM-Mysore lilizinduliwa rasmi na Mh. Samuel J. Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Katika uzinduzi huo Mh. Sitta alisisitiza vijana kujitambua na pia kufanya mambo kwa kutumia akili zaidi kuliko mabavu na akasisitiza kuwa lazima vijana wakajenge nchi. Pia Spika aliwaambia kuwa swala la mafisadi linashughulikiwa kweli kweli. Mjumbe wa NEC Taifa Nape M. Nnauye nae alimwambia Spika kuwa hawa ni vijana makini na walichokuambia hapa kifanyiwe kazi maana wanafuatilia kila taarifa ya nyumbani na pia hao mafisadi watoke hadi kwenye chama.
 
Naona Nnauye anautaka uenyekiti kwa nguvu zote!sisi atusaidie tu kufichua mafisadi
sema nape usiogope ila tu Take care usijezahishwa mbele ya haki kabla ya siku zako!maana kuna wachache wabinafsi wanachukia
 
Mkuu Gembe,

Nenda kwenye hii link: http://mjengwa.blogspot.com/2008/05/spika-sitta-afungua-tawi-la-ccm-mysore.html#comments

Sijui namna ya ku-upload pic na kuweka hapa. Ila kuna pic ya Mzee Sitta na chini ya picha kuna maelezo haya hapa:

Jana Tar 20/5/2008, tawi la CCM-Mysore lilizinduliwa rasmi na Mh. Samuel J. Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Katika uzinduzi huo Mh. Sitta alisisitiza vijana kujitambua na pia kufanya mambo kwa kutumia akili zaidi kuliko mabavu na akasisitiza kuwa lazima vijana wakajenge nchi. Pia Spika aliwaambia kuwa swala la mafisadi linashughulikiwa kweli kweli. Mjumbe wa NEC Taifa Nape M. Nnauye nae alimwambia Spika kuwa hawa ni vijana makini na walichokuambia hapa kifanyiwe kazi maana wanafuatilia kila taarifa ya nyumbani na pia hao mafisadi watoke hadi kwenye chama.
Kuna mtu ambaye hakwenda na haumjui..kuna picha flani naipata..the next thread nitakayoandika wiki ijayo itakuwa na picha kamili ..stay Tuned,I will point out who should be the next Chairman of UVCCM.Nitamtaja mtu amabye hajapata pesa yoyote kutoka kambi yoyote..nafuatilia,

on my side,Nape ana mtu mzito nyuma yake,Benno ana mtu nyuma yake..kuna mtu,nayupo na namfahamu..ndiyo hana mtu ila namchunguza
 
Haya mambo ndugu zangu tunachukulia mzaha. Na mzaha na hewala ndio zimeifikisha Tanzania na sisi wananchi hapa tulipo sasa.

Miaka ya nyuma(Nyerere) sikuwahi kufikiria kama kuna siku Kikwete na Lowasa watakuwa viongozi wa juu serikalini......lakini sikuwa sahihi,kwa kuwa hewala na mzaha ulikuwa mwingi. CCM inajichukulia kama ndio SERIKALI YA TANZANIA na wala si CHAMA TAWALA. Kuna mambo mengi tu ambayo sisi WANANCHI tuliyafumbia macho na sasa hivi yanatufikia shingoni.

Suala la huyu bwana Ridhiwani lisitupotezee mwelekeo wa kudeal na CCM na Uongozi wa Tanzania. Tusipofanya mchezo CCM itakuwa madarakani kwa karne nyingine ijayo....na sisi kina kajamba nani tukaendelea kugombana wenyewe kwa wenyewe....huku wachache wakifaidi nchi.

Tusisahau kwamba there is such a thing as DYNASTY.....kwa hiyo tusishangae huyo Ridhiwani akaja kuwa Rais katika siku za usoni.

George W. Bush alitayarishwa na baba yake na wafanyabiashara wa mafuta Texas kwa Urais....na wengi tulibisha sana suala la yeye kuchaguliwa.

Well alikuwa Rais kwa term mbili(8yrs) na kuivuruga Marekani hapa tuliko. Tuwe makini ndugu zangu.

Huu ni wakati wa Kuindoa CCM madarakani. Na kuunda serikali ya Wananchi wote ...sio WanaCCM tu.


Wasalaam.
 
Zainab Kawawa naye kugombea uenyekiti vijana CCM

HabariLeo;
Thursday,July 17, 2008


Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameendelea kuchukua fomu kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) akiwamo mtoto wa mwanasiasa mkongwe, Rashid Kawawa, Zainab Kawawa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa, Beno Mulisa.

Kawawa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), anagombea nafasi ya uenyekiti akiwa na Said Mtanda ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa upande wa hotuba za siasa, Joy Pangisa.


Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Isaac aliiambia HabariLeo kuwa wanachama hao walichukua fomu jana ikiwa ni siku ya pili tangu fomu hizo zianze kutolewa. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Jumapili huku uchaguzi umepangwa kufanyika kati ya Desemba 13 na 14 mwaka huu.


Wengine ambao wameshachukua fomu kugombea nafasi ya uenyekiti ni Mjumbe wa NEC Nape Nnauye, Mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Anthony Mataka na Mjumbe wa NEC Wilaya ya Arusha Mjini Dk . Harold Adamson.


Mbali na hao Mwandishi Mwandamizi wa magazeti ya CCM ya Uhuru na Mzalendo, Ester Bulaya alichukua fomu katika ofisi za UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam akigombea nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu Taifa. Nafasi zinazogombaniwa ni sita nchini nzima.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Sixtus Mapunda, Bulaya alisema kuwa "nataka kuitumikia UVCCM kwa maadili kukijenga chama kwani naamini bila UVCCM hakuna CCM. Vijana ndiyo tunaojenga chama". Katibu Mkuu huyo aliwataja wengine waliochukua fomu kugombea nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu Taifa ni Kashinde Juma, Dk. Moses Ringo na David Wembe huku Happiness Mahava akigombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM.
 
.....naona mafisadi wanachaguana wenyewe kwa wenyewe!
 
.....naona mafisadi wanachaguana wenyewe kwa wenyewe!

Hivi huu umoja wa kitaifa utadumishwa vipi. Akina mama wa CCM, wazazi wa CCM, vijana wa CCM na mafisadi wa CCM. Lo, kwa mwendo huu kazi kweli kweli.
Karibu tutashuhudia hata umoja wa vitukuu vya CCM.
 
Huyo jamaa ameshanyweshwa na kuonja utamu wa mvinyo unaoitwa madaraka. Na ile kuitwa mzee na kunyenyekewa kila wakati. Sasa inabidi aweke mazingira ya kujijenga ili na yeye asimame . Mtoto wa Nyoka ni nyoka.

Lakini amekuwa na haraka sana na inaelekea siku hizi hata viongozi wetu yale maadili ya zamani hayapo tena. Nyerere hakuwahi kuwa hivyo labda wakati wa ruksa ambaye alileta ushemeji mpaka State House hapo hadith ndipo ilipo anzia na Mr Clean kamalizia.

Muungwana anajua kuwa na yeye inabidi awe na dynast ya kwake katika system lakini politics ni kama upepo unaovuma na hauna direction ngoja tusubiri tuone.
 
Wote humo ndani ya NEC ni watoto wa vigogo...Sasa nyie mnataka wamchaguwe nani nje ya NEC?
 
Sasa hivi tutasiki na mtoto wa Kikwete, Mkapa, Sumaye, Lowassa etc nao wakichukua fomu. Like Father, like son...
 
Back
Top Bottom