Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
ATC ni shirika la Serikali na viongozi wake huteuliwa na Rais kwa hiyo bosi wao Mkuu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakuna kipendelea kinachosema kuwa Mtanzania akipata matatizo katika masuala yake yanayohusiana na dini basi asisaidiwe. Mbona Mrema alienda kusuluhisha migogoro kibao ya kule ARUSHA kwenye KKKT??
Kuchanganya Dini na Siasa na vitu viwili tofauti na kusaidia wananchi wako ambao wako katika matatizo yawe ya dini au ya Siasa. Kwa hiyo hili suala halihusiani kabisa na kuchanganya dini na siasa. Hili suala ni la viongozi wa juu wa serikali kusaidia moja ya Idara yao ambayo imekithiri uzembe, Ugoigoi, ujinga, na isiyoheshimu wateja wake. Hiyo Idara inaongozwa na viongozi ambao walichaguliwa na hawa Viongozi wakuu wa nchi. Uzembe wa kina Mataka na Nyang'anyi unaashiria kabisa pia kuna Uzembe kwa Viongozi wa juu ambao waliwachagua kwenye hizo nafasi zao.
Kwa hiyo rukhsa kwa serikali kuchanganya dini na siasa?
mbona wale wanafunzi wa UKRAINE hawakupewa msaada wowote na hiyo hiyo serikali iliyo kimbelembele na hili ya kwenda MACCA?
kilichopo ni KIINI macho na unfortunately waislama wa BAKWATA hili hawalioni
Kwanini kwenye mambo huhimu ya waislam serikali hii hii haionekani?
Mrema naye probably aliona sawa kuingilia mambo ya KKT kwa sababu bosi wake Mwinyi alikuwa anafuturisha waislam Ikulu
Wanachokifanya viongozi wa Serikali ni kusaidia watumishi wao wazembe wa pale ATC hasa Mustapha Nyang'anyi na David Mataka ambao wameshindwa kulishughulikia hili tatizo katika muda muafaka.
Kuchanganya Dini na Siasa na vitu viwili tofauti na kusaidia wananchi wako ambao wako katika matatizo yawe ya dini au ya Siasa. Kwa hiyo hili suala halihusiani kabisa na kuchanganya dini na siasa. Hili suala ni la viongozi wa juu wa serikali kusaidia moja ya Idara yao ambayo imekithiri uzembe, Ugoigoi, ujinga, na isiyoheshimu wateja wake. Hiyo Idara inaongozwa na viongozi ambao walichaguliwa na hawa Viongozi wakuu wa nchi. Uzembe wa kina Mataka na Nyang'anyi unaashiria kabisa pia kuna Uzembe kwa Viongozi wa juu ambao waliwachagua kwenye hizo nafasi zao.
Nadhani Bakwata walishapeleka mahujaji wao kupitia Emirates Airlines.
Hivi Nyanganyi na Mataka wanahitaji msaada wa serikali nzima kufanya kazi yao?
Mbona BAKWATA wako kimya?
Mbona SHURA YA MAIMAMU kimya?
Mbona ANNUR liko kimya?
Mbona DAR ES SALAAM ISLAMIC CLUB wako kimya?
Mbona MSAUD wako kimya?
Mbona MWAMKO wako kimya?
Mbona HAJJ TRUST wako kimya?
au ndio mamabo ya ku pick and chosing battles?
No wonder serikali inawaburuza waislam kila angle kwani hawa wanajuana
Kama kusaidia huko kwa nini wanafunzi wa UKRAINE hawakusaidiwa?
Kuchanganya dini na siasa kupo kuanzia NYIMBO YA TAIFA, wanasiasa kuingilia mambo ya kwenda hijja mpaka lile la kuwafuturisha watu ikulu kwa kutumia kodi za wasio na dini na wasio waislam
huo ni udini
Serikali ilitakiwa ikae pembeni na kazi yake ilitakiwa kuhakikisha kuna usalama na siyo kuanza na kuja na initiatives ambazo clearly zinaonyesha upendeleo wa hali ya juu
Je wakristo leo wakilalamika kuwa waislam wanapendelewa na serikali ilijaa udini itakuwaje?
Nadhani Bakwata walishapeleka mahujaji wao kupitia Emirates Airlines.
Sidhani kuna umuhimu wa hizo jumuiya nyingine za kiislamu kuingilia kwenye hili suala kwa sababu mhusika mkuu ni ATC. Kwa sababu hata Bakwata wakiingilia nani atalipa gharama za kuwasafisha hao watu wakati ATC imeshaweka hela mfukoni. Serikali inawajibika moja kwa moja kuwasaidia ATC, maana hapa sio kuwasaidia mahujaji maana yake wao wameshalipa pesa lakini kutokana na upumbavu unaoendelea serikalini basi wameshindwa kusafiri. Kwa hiyo hapa Lowassa na Mwenzake Kikwete wako pale kusaidia wazembe wenzao kina Mataka na Nyang'anyi.
Kwa hiyo unataka kuniambia zile fund raising zinazofanyika makanisani na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi zinapendelea wakristo?? Na mwisho utasema hata viongozi wa nchi wasialikwe kwenye sherehe mbalimbali za kusimika maaskofu makanisani, kwenye sherehe za maulidi, kwenye sherehe za X-mas, kwenye sherehe za Pasaka???
ATC kwa miaka yake yote ya kufanya kazi imeshindwa hata kukodi ndege ya KQ au SAA? Nakubali ni jukumu la serikali kusaidia raia wake lakini hapa kwenye hili ni kutetea uzembe huyo Nyang'anyi na Mataka hawajasikika wakiomba radhi au hata kuelezea msimamo wa shirika.
Serikali yetu nayo ina double standards huo ndio ukweli wenyewe, wale vijana waliokwama Ukraine walikanwa na huyo huyo waziri mkuu aliishia kukata simu akisema anakwenda kula.
Suala hili ni dogo halihitaji Waziri Mkuu, huyu Bwana ana kazi nyingi, kama Mataka anawajibika kwake ni kumpa maagizo watu waondoke. Kuna njia nyingi za yeye kufanya labda kama waliwachelewesha hili awaondoe na kujipandisha kisiasa kupitia kwa maujaji.
at whose expense?
hivi kodi zetu kazi yake ni kuwasafirisha watu kwenda kuhiji au? kesho wakitaka wanunuliwe kanzu serikali itakubali au ndio mamabo ya political correctness?
Tena kule Ukraine kulikuwa na baridi balaa. DSM unaweza kulala nje hakuna baridi, yaani derava na utingo wake wote wanarusha changa la macho kwa wabongo.
mbona serikali hii hii haikuingia kati kuwasaidia wanafunzi wa UKRAINE?
Mjomba hii ni PR excercise at the expense of walipa kodi ambao si waislam
JF mnasifika kwa kuwa ma free thinkers mbona hili hamtaki kuliangalia kwa undani zaidi?