Engineer Mohamed
JF-Expert Member
- Jul 27, 2007
- 451
- 9
mhhh sasa hii kazi kweli kweli
Mahujaji Dar: Kumbe hakuna aliyepaa jana!
2007-12-12 16:34:22
Na Sabato Kasika na Sharon Sauwa, Jijini
Licha ya taarifa njema zilizoripotiwa leo asubuhi kuwa baadhi ya mahujaji waliokwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini wamepaa jana kwenda Makka, ukweli ni kwamba hakuna hujaji hata mmoja aliyesafiri.
Badala yake, imefahamika kuwa mahujaji hao wameendelea kusota tena usiku wa jana na kupewa matumaini mengine kuwa huenda wangeanza kuondoka leo.
Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, mmoja wa viongozi wa msafara huo wenye mahujaji zaidi ya 1,000, Sheikh Saleh Issa wa wakala wa Hajji Trust, amesema yeye na mahujaji wengine zaidi ya 300 walipanda ndege mishale ya saa 4:00 usiku jana na kukaa kwenye siti zao.
Akieleza zaidi, Sheikh Issa akasema badala ya safari kuanza, wakastukia wakishushwa ndani ya ndege hiyo kutokana na maelezo kuwa kuna taratibu fulani za ndege hiyo kutua Jijini Jeddah kule Saudi Arabia hazikuwa zimetimizwa.
``Tulielezwa kuwa hakukuwa na kibali cha kuingilia Jeddah? pia tukaelezwa mambo mengine kadhaa yaliyowalazimu wahusika kutushusha na kuahirisha safari,`` akasema Sheikh Issa.
Hata hivyo, Sheikh Issa akasema waliambiwa kuwa masuala yote tata kuhusiana na safari ya ndege hiyo yangekamilishwa mapema, hivyo leo wangeweza kusafiri huku mahujaji wengine wakiendelea kusubiri.
Kiongozi mwingine wa msafara huo ambao pia una baadhi ya mahujaji toka nchi jirani ikiwemo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC), Sheikh Ali Mia, amesema kilichotokea hadi wakashushwa, ni kutokamilika kwa baadhi ya taratibu ikiwemo ya kibali na pia, kutekelezwa kwa kanuni za kimataifa kuhusiana na usafiri wa anga.
Akifafanua, akasema Sheikh Ali kuwa abiria walipanda kwenye ndege hiyo mishale ya saa 3:00 na ilipotimu saa 4:30 usiku wakaambiwa washuke kwani ni ukiukwaji wa kanuni, usiotaka abiria awe kwenye ndege zaidi ya saa moja bila kupaa.
``Hayo ni baadhi ya yale tuliyoyasikia? tunaendelea kuomba na bila shaka, kama Mungu amepanga kuwepo kwa safari hii, inshallah itakuwepo tu,`` akasema Sheikh Ali.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa mwisho wa kuingia ndege za mahujaji nchini Saudi Arabia ni kesho, na kwamba baada ya hapo hakuna itakayoruhusiwa kuingi nchini humo.
Sakata la kukwama kwa mahujaji hao limeanza tangu Desemba 3 mwaka huu ambapo badala ya kusafirishwa na ndege waliyolipia na kuingia nayo mkataba ya ATC, mahujaji hao wakaambiwa wasubiri kwani ndege iliyotazamiwa ni mbovu.
Kuanzia hapo, wakawa wakipigwa danadana kila kukicha hadi Serikali ilipoingilia suala hilo na kutaka wasafirishwe kwa ndege nyingine zilizokodiwa nchi za Ureno na Hispania.
Katika hatua nyingine, viongozi kadhaa wa kitaifa waliendelea kufika katika uwanja huo ili kuwapa pole mahujaji hao akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Kandoro.
SOURCE: Alasiri