Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Jamani sisi tulioko huku mikoani tunaomba Live Press Conference mtuwekee tujue kinachoendelea tafadhali!

alieko dar,alie mkoani alie ulaya hata mashariki ya mbali upataji habari kupitia jf ni uleule tu...zaidi ni yule mtao habari.
 
Tundu Lissu amefanya Press muda mfupi uliopita. Anasema
1. Anafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.

2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.

Lissu anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.
-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa
-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.
-Ludovick baada ya kukutana na Rwakatale tarehe 28Dec saa 5 muda mfupi baadae yaani saa 5:59 alimpigia simu Mwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.
-Siku iliyofuata tarehe 29Dec akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.
-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.
Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA. Press nzima itakuwa www.chadema.tv muda mfupi ujao

Naona kidogokidogo chadema wanaanza kumtema Ludovick.

Vilevile kidogokidogo wananza kukubali kuwa video ya Lwakatare sio fake.

Dr. Slaa amejidhalilisha sana kumtetea Lwakatare kabla hajajua nini kinaendelea.
Pasco aliwapa ushauri wa thamani kubwa sana wa kumkana Lwakatare mkaukataa, sasa muda wa kufanya hivyo umeshapita. La Lwakatare ni la chadema, hamuwezi kujitenga nae...

Stay tuned...
 
Last edited by a moderator:
Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.
Mawani yangu yameposuka, hebu mtu asome hapo kwenye bold!
hapo vipi, unaweza kuona bila miwani!?
Wataumbuka wengi hapa

 
  • Thanks
Reactions: FJM
Naapa chini ya Mbingu na Ardhi kamwe Shetani hatamshinda Mungu.

Kama Daudi alimuua Goliathi kwa jiwe katu Mashetani hawa wanaotaka kuichafua Chadema hawatafanikiwa na wataangamia.

Naapa kwa Mungu aliye hai yeyote aliyeshiriki kutunga mpango huu mchafu hatabaki salama.

Naapa kwa Mungu Mkuu muumba kila kitu kwamba kila aliyeshiriki kutunga uchafu huu lazima ataumbuka siku si nyingi na ataomba radhi hadharani.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Anania akapasuka matumbo mbele ya madhabahu kwamba wahalifu hawa watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Herode akadondoka juu ya kiti cha kifalme na mwili wake kuliwa na siafu kwamba waovu waliotunga mbinu hii watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu wa Abraham,Isaka na Yakobo kwamba watu hawa hawataweza kuendelea kuharibu Taifa letu kwa uchochezi wao bali watakipata sawasawa kile kiwapatacho watu wasiomjua Mungu.

Naapa kwa Mungu ambaye jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO kwamba Shetani kamwe hatajitwalia utukufu.

Wao wana Baali na Chadema wana Mungu kamwe Baali hawezi kumshinda Mungu.
 
How? alisema nini? na unahisi umati ulicheka kwasababu gani? umati ulimcheka Lisu au ulichekeshwa kwa jambo lingine? ZeMarcopolo ni miongoni mwa watu wachache sana nisiowaelewa kabisa hapa Jamvini!!!!

Njaa haina Adabu kaka , siyo kwamba haioni hali halisi , la hasha ! Ila atafanyaje ? Wapo kama watano humu jf , utawajua bila shida yoyote .
 
Last edited by a moderator:
wewe hata kiswahili huelewi? Lwakatare amesema kuwa kwenye ile video, picha ni ya kwake, halafu hiyo siku yeye hakuwepo huko eneo inakoonekana ilichukuliwa lakini Ludovick alifika nyumbani kwake siku hiyo video ilipochukuliwa. Baadhi ya maneno ni yake lakini mengine siyo yake.

Kwa haraka, hii ina maana gani? Ludovick ndiye aliyemrekodi Lwakatare alipoenda nyumbani kwake. Baada ya kurekodi, nahisi kwa kutumia simu, alikwenda ku-edit video hiyo ili ionekana kama inavyoonekana. Lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa video hiyo imekuwa edited zaidi ya mara moja, ndiyo maana ile iliyopo kwenye Youtube inatofautiana na ile waliyo nayo polisi.

Mbona wanasheria hawasemi ile video ni fake?

Kama ule mkanda nk genuine basi huo ni ugaidi.
 
Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .

Kwa wale waliokuwa wanasema hiyo video siyo ya Lwakatare nafikiri jibu limepatikana vizuri ila point wanayoshikilia wanasheria ni kuhusu sound editing kama wanavyosema hapa chini.

Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.


 
hakika CCM ni chama cha kipuuzi! CCM wanadhani wataiua Chadema kwa kuwabambikizia kesi na kufanya propaganda.
CCM wanadhani kutokukubalika kwao mbele ya wananchi wachawi ni Chadema wakati wachawi ni wenyewe CCM.
2015 CCM mtapata aibu.
 
ninahamu ya kusikia Ludovick na Mwigulu waliongea nini kwenye simu.....muda utaongea.
 
Hivi km CCM wanataka kuidhoofisha CDM hawana njia nyngne ambayo inaleta sense kwa wananchi zaidi ya hii SERIES,maana season 1 ilisha pale mahakama ilipomwachia huru Lwakatare,wakaona hutujaridhka wakaamua kuendelea na season 2 kwa kumkamata tena Jamaa.
Only in TZ!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni dhahiri kuwa CCM walikuwa wakimtumia Ludovick kijasusi. Mawasiliano kati ya Mwigulu Mchemba na Ludovick siku ambayo video ilichukuliwa yanaondoa shaka kuwa aliyeichukua video ni Ludovick, na aliyeifanyia editing ni Mwigulu na Ludovick.

Hii ni aibu nyingine ya Kikwete, viongozi wa chama chake kwa kushirikiana na polisi wanahusika na mbinu chafu na za kipu.mbavu. Big shame to Mwigulu, big shame to Ludovick, big shame to the police and big shame to CCM.


Naona kidogokidogo chadema wanaanza kumtema Ludovick.

Vilevile kidogokidogo wananza kukubali kuwa video ya Lwakatare sio fake.

Dr. Slaa amejidhalilisha sana kumtetea Lwakatare kabla hajajua nini kinaendelea.
Pasco aliwapa ushauri wa thamani kubwa sana wa kumkana Lwakatare mkaukataa, sasa muda wa kufanya hivyo umeshapita. La Lwakatare ni la chadema, hamuwezi kujitenga nae...

Stay tuned...
 
sina imani kama kweli kwa hali ya Tz mahakamani ni sehemu ya kupatia haki kwa mwenendo wa mambo sasa yanavyokwenda kisiasa, yani kila kitu ni siasa

Ndugu yangu mpaka usiogope sana, muhimili wa sheria hapa nchini siyo mbaya sana,ni baadhi yao wachache sana ndiyo wanaojaribu kuvuruga huo muhimili,nataka nikuhakikishie kua kwa mahakamani hiyo kesi itatupiliwa mbali,tatizo ni kule kuchafuana na ndiyo lengo lao kuu,yaani wanacho kitaka hadi uchaguzi ujao ufike (watu)viongozi maarufu wa upinzani karibu wote wewe wameshafikishwa mahakamani ili wananchi wawaone kama hawafai kua viongozi wao,kumbuka kesi ya mheshimiwa Lema,kilichosaidia ni hao hao watumishi waliosafi wa mahakama zetu,usiogope wapo waadilifu na wanaoitakia mema nchi hii.
 
Kwamba maelezo ya tundu lisu ni kukubaliana n'a uhalisi wa ile video? Inawezekana ila pia tusiwe n'a haraka n'a mambo. mbona muda tunao n'a ukweli utajulikana.
 
huu muda wa kubabikiziana mi-kesi isiyo na manufaa kwa taifa tungeutumia kutengeneza mitaala ya elimu ambayo hatuna tangu uhuru - eti UGAIDI, hivi mnacheza na UGAIDI nyie? hiyo kidnapping mnaita ugaid? police wa tanzania wanaseza kupeleleza UGAIDI?

nafikiri Tanzania mnautaka UGAIDI mtaupata, kama mlivyouomba udini na ukabila.

Kongolo umenena kweli, ugaidi kama wanautaka waone kule Syria, Nigeria, Mali n.k.Uchochezi na utekaji nyara unaita ugaidi?, ni ujinga tu wa kutumia madaraka vibaya.Kama juzi tu serikali ilifukuza Polisi kwa kubambikia wananchi kesi za mauji huko Karagwe ,kumbe Mapolisi upewa amri na Serikali ya ccm kubambikiza wananchi kesi kubwa kama wanavyofanya kwa huyu Lwakwatare.
Nilisoma gazeti la Daily News la jana wanataka kumbambikiza dereva aliye gomga askari wa trafiki kesi ya Uhaini kwamba alihatarisha maisha ya Rais Kikwete kwa kuhatarisha msafara wake.Unaona kesi za kijinga zinazoibuliwa na kubambikwa wananchi?.Msafara wa rais ni magari zaidi ya 50 mtu akiwa nyuma na gari zinavutwa tuanaweza kufikri magari yanaitwa na trafiki na muda wao kupita maana mataa au trafiki light kwa dar hazitumiki kabisa.Yule dereva kosa lake ni kugonga na kuua na kukimbia bila kutoa msaada na siyo kubambikia wananchi kesi kubwa kukomoa tu.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya mabishano ya kisheria, juzi mahakamani , hakimu alisema angetoa hukumu juu ya kama mashitaka ni sahihi kwa mujibu wa sheria ama laa, ila jana asubuhi badala ya kusubiria hukumu ya awali juu ya uhalali wa mashitaka hayo hawakusubiri hukumu badala yake walipeleka hati ya kufuta kesi na baada ya dakika tano walimkamata na kumfungulia mashitaka yale yale , ila kilichobadilika. Ni namba ya file ya kesi tuu , ila mashitaka ni yaleyeale mpaka nukta ya mashitaka.

Lengo lilikuwa ni kuizuia mahakama isitoe uamuzi ndio maana waliamua kufuta kesi na kuifungua hiyo hiyo,
Nia ya hawa watu ni kutafuta wakubwa wa chama cha CHADEMA ili ionekane ndio waliomtuma Lwakatare apange njama za uharifu huo!!! Wamesahau kuwa CHADEMA kuna wanasheria wa kuchunguza na kutoa utetezi ulio halali badala ya viini macho!!! CCM imeishiwa sera wakalale kazi yao imekwisha!!!
 
Back
Top Bottom