AdvocateFi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 11,492
- 5,040
Freedom is coming tomorrow.
Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.
Aidha , ameongeza kuwa tarehe 27.12.2012 Denis Msacky alimpigia simu Lwakatare wakati akiwa njiani kurejea akitokea Kagera , akiwa Morogoro na kumuuliza kama yupo DSM , akamjibu yuko njiani.
.
Clouds wanalazimisha kujitumikisha...siyo tatizo. Lakini wajitahidi kuwa smart!Clouds redio waliorusha ya kwenye you tube watakuwa matatani mara baada ya hii ya polisi kuwekwa hadharani , wajiandae kumlipa Lwakatare fidia kutokana na kumdhalilisha mbele ya umma .
Only Almighty God can take him there. Ndiyo maana hata kina Ulimboka waliotaka kufikishwa huko bado wanadunda.Tumpeleke alikoenda Mr KIVUITU
Bunge la MAKINDA ndo lina issue ila zama za SITTA huwezi leta hoja zako za kipuuzi puuzi ndo maana wakampiga chini ata PM wa kale EL.Hivi unaamini kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea? Wote bunge na mahakama wanaendeshwa remotely toka magogoni.
Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.
Anaeleza kuwa kama ameshitakiwa kwa ugaidi lazima makosa hayo yawe ni ya kigaidi, ila makosa ya
Kidnapping na abduction ni makosa ya kawaida ya jinai , na kama ili yawe ya kigaidi ni lazima hayo makosa yawe yamefanyika kwa malengo ya kigaidi , na hata hati ya mashitaka haina maelezo ya makosa ya ugaidi .
Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.
Aidha , ameongeza kuwa tarehe 27.12.2012 Denis Msacky alimpigia simu Lwakatare wakati akiwa njiani kurejea akitokea Kagera , akiwa Morogoro na kumuuliza kama yupo DSM , akamjibu yuko njiani.
Tatu, tarehe 29.12.2012 Mwigulu Nchemba , akiwa na Zitto na Mtatiro Star Tv , kipindi cha tuongee asubuhi ndipo alisema kuwa ana mkanda wa viongoz i wa chadema wakipanga mauaji ......sasa haya yote yatajulikana mahakamani.
Ziada .
Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .
Sasa polisi nao waliulizwa ni kwanini hawajamkamata aliyeweka hiyo you tube kwenye mitandao walitoa majibu yao na mawakili wanaendelea na uchunguzi wao.
hii serekali imekaa kijoti joti,ukiangalia na ile kesi ya Lema ya ubunge utugundua dhuluma ni nyingi sana!
Tundu Lissu siku ile alijidhalilisha sana pale mahakamani mpaka akachekwa na umati wa watu!!!
mtawawaibisha mapolice na mahakimu bure!! kama mlivyofanya ile kesi ya Lema, yule hakimu anaelewa sheria ila anapidisha ili afuate maagizo ya Mary Chitanda -- ha ha haCHADEMA kupitia mgongo wa wanasheria wanaomba huruma ya wananchi, tambueni sheria ni msumeno; Lwakatare karikoroga ni wajibu wake kulinywa
Nasikia sauti ya jamaa mmoja wa chadema anaitwa ludovik akiitikia na kutoa maelezo kwa boss wake mratibu na mtendaji bwana rwakataremmh kweli hii ngoma nzito kwa chadema sijui watatokea wapi
hii ngoma nzito sana kwa chadema sasa sijui nayo wataandamana na huyo jamaa anaeitikia hapo na kujibu maswali ya mchora mchoro wa utekaji nyara lwakatare ni jamaa mmoja hivi wa chadema anafahamika na hizo ndizo kazi zake jamaa huyo bwana L kama herufi yake ya mwanzo ya jina lake ilivyo aliwahi somea upadre ila ukamshinda akaacha naye hana pakukwepea katika hili maana kwa wanaomjua vizuri kama mimi hawatosita kumtambua kwamba ni YEYE{KIJANA L]
Weka zote mkuu hali ya kiusalama ya nchi ni tete lasivyo watatumaliza hawa jamaa
Hili tunasema kwa kiinglish kuwa ni CCM sysmatic calculated mission na haitaishia kwa Lwakatale tu ni vema Chadema wakajiandaa kwa mengi zaidi.Ukweli daima utasimama mwisho wa siku, kama serikali kwa makusudi kabisa wanaamua kutumia pesa za walipa kodi masikini wa Tanzania kwa kufungua kesi za kutunga kwa malengo ya kuiondoa Chadema kwenye ramani ya kisiasa, hakika watafutika wao, maana malipo ya dhambi wanayoitenda sasa ni makubwa sana na hawatakaa waisahau milele.
Tusubiri tuone, kwanza wameonesha ambavyo wasivyo makini kupitia wanasheria wao, hivyo mwisho wa siku huku kudharisha wanakofanikisha kwa Lwakatare as individual person na Chadema kwa kiwango fulani kwao itakuwa disearter very soon, tusubiri yetu macho, acha wanasheria watifuane na tuombe mahakama isimamie haki.