Usije shangaa hili likaipatia umaarufu Chadema. Naanza kuiona kama ni movie iliyopangwa kila upande ukitaka kumwingiza mwingine matatani. Wasipocheza vizuri CCM watajikuta wamenasa kwenye mtego wa Chadema. Nani alijua Lema angerudishiwa ubunge baada ya kuvuliwa na mahakama? Katika mazingira haya kuna uwezekano wa kila upande kuwa na 'mapandikizi' Serikali inaangushwa na wataalamu wake ambao wamelewa madaraka kiasi cha kutoonyesha umakini katika utendaji wake loophole ambayo wataalamu wa Chadema wanaweza kuitumia kukuza majina yao na kukiongezea chama umaarufu. Ni mapema kujua nani atatoka na kicheko hapa. Tuvute subira ni mchezo usiotabirika!
Mkuu, hivi una matatizo gani. Maji yako shingoni kwa nani?.Wewe si ndio nimekuambia maji yako shingoni ukajifanya hujui?.
Acha kusingizia uwezo wa wanasheria wa serikali, Kutetea uwongo huwa ni ngumu hata uwe mwanasheria vipi.
Acha ifahamike tu.
Mnateteaje waovu? Haingiu akilini wote humu mnatetea magaidi
Mie kwa mtazamo wangu nafikiri serikali ya CCM kupeleka hii kesi mahakamani kwa kutumia cheap video watakuwa wamejichoma kijiti cha muhogo masaburini. Kwa uelewa wangu: Unapotumia digital file(s) as evidence before the court(s), hapa una- involve computer forensic.
Kwa faida ya JF mambers and non-members: Wale mliosoma Cyber-crime or Cyber-security, Once you decide to present digital evidence before the court, you are mandated by law (sijui sheria ya kwetu) to show/prove that you're disciplined in associating elements of law and computer science to gather, secure, examine, and analyze data from computer systems, networks, wireless communications, and storage devices in a way that is admissible as evidence in a court of law. Kwa serikali yetu sina hakika if that happened.
1. The Magamba's gov needs to prove that whatever they gathered during their raid(s) wasn't contaminated.
2. The Magamba's gov needs to show how they examined the data collected (Ni computer lab gani waliweza ku-examine digital file from public domain in less than 17 hrs) iwapo mpaka dakika hii wameshindwa kukamata wale wezi wa TRA waliotumia mtandao 2 yrs ago (Kitillya knows what I'm talking about).
3. The Magamba's gov needs to prove they analyzed the collected data thoroughly and none of information byte(s) omitted/added.
4. The gov also needs to prove before the court that people who collected, secured, examined, and analyzed the data from Youtube domain are ethical and the whole process wasn't interfered by external pressure.
Inasemekana hiyo video ilikuwa edited, na sehemu nyingine ikiwa imeondolewa. Kwa mtazamo wangu, Information gathered wasn't secured before presented kwa mahakama ya Umma (video haijaonyeshwa mahakamani). Serikali inatakiwa ionyeshe hatua kwa hatua jinsi walivyoweza ku-secure hiyo process nzima hadi kumpeleka Lwakatare before the court.
Waeleze kama walikuwa na hiyo video kabla haijawekwa kwenye public domain (Youtube). Kama walikuwa hawana, waeleze hiyo process ya ku-gather and analyze digital file ilivyochukuwa muda mfupi bila ya kuwa na original storage media. Na kama walikuwa na original storage device(s), kwa nini sehemu ya video imekatwa?
Huu ni mtazamo wangu tu ingawa mimi si mwanasheria lakini nina background ya Digital Forensic Investigations.
Mkuu, mimi nina matatizo na watu kama wewe wanaotetea maovu kwa kujifichaficha.Mkuu, hivi una matatizo gani. Maji yako shingoni kwa nani?.
I'm not a blind follower kama unavyojitandaza kwenye mabandiko yako. Uongo upi unaousema?.
Ninapenda open discussion na ndiyo hiyo tulikuwa tunajadili na Lukolo.
Wewe unataka kwa nguvu zote na kwa njia yoyote mawazo yako yawe ndiyo kweli daima wakati hata hufahamu matokeo ya kesi yenyewe.
Tafuta mtu mwingine mwenye mawazo kama yako ndiyo mtaelewana.
Mitanzania mingine bana. Khaa
Mbona wanasheria hawasemi ile video ni fake?
Kama ule mkanda nk genuine basi huo ni ugaidi.
Lissu kabla hajayasema haya aliwasiliana na Katibu mkuu wake? Maana huyo babu alikwisha sema hii video ni ya kuchakachua hadharani. Kweli Lissu kesi imefikia patamu sana na kwa kazi ya kumlinda Slaa Ludo atakuwa na mengi mno ya kushare na dunia.
KUNA KITU KINGINE ??? MhhhhhSio njaa...Kuna kitu kingine
Lissu kabla hajayasema haya aliwasiliana na Katibu mkuu wake? Maana huyo babu alikwisha sema hii video ni ya kuchakachua hadharani. Kweli Lissu kesi imefikia patamu sana na kwa kazi ya kumlinda Slaa Ludo atakuwa na mengi mno ya kushare na dunia.
Mkuu, mimi nina matatizo na watu kama wewe wanaotetea maovu kwa kujifichaficha.
Maji ni ya shingo kwa watetezi wa filamu, ninaamini wewe ni mmoja wao, kitu unachojidanganya ni kudhani kuwa unaandika ki tactic sana na kwamba unaficha mrengo wako, sio kweli, unaeleweka vizuri mno wa kwetu.
Nahisi wewe ndio unaweza kuwa blind follower kwa sababu ukiunganisha matukio ni lazima uamini kuwa clip imepikwa, na ndio uongo ninaouzungumzia. soma tena post hapo juu vizuri.
OMISHA MHOLA NKOYI?
Kuna kitu ambacho Wanasheria wa CHADEMA wanashindwa kukisema badala yake wanaweka privacy law mbele na kusema imevunjwa kwa Lwakatare kurekodiwa bila idhini yake.
Swala la mtu kurekodiwa anafanya kosa haliwezi kufunikwa na privacy law. Lwakatare amerekodiwa anatenda kosa na kosa hilo haliwezi kuwa siyo kosa kwa sababu privacy law imevunjwa.
Kitu cha muhimu kabisa katika kesi hii, ufunguo wa kesi hii uko na Ludovick kama kweli alikuwa ndiye anarekodi. Ushahidi wake ndiyo utatoa picha mbadala ya nini kilikuwa kinafanyika CHADEMA.
Tusibiri tusikie upande wa pili katika kesi hii kwa sababu kwa sasa tunafanya judgement kwa maelezo ya upande mmoja.
Is the video authentic?That's a legitimate question ,the rest will flow.Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.
=========
Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, Wakili Tundu Lissu, akiwawakilisha wenzake, ameongea na vyombo vya Habari akiwa Makao Makuu ya CHADEMA na kuzungumzia masuala kadhaa kutokana na sakata hili.
Lengo kuu la mkutano huo na wanahabari lilikuwa ni kuutarifu umma wa Watanzania kupitia kwa wanahabari juu ya hatua ambayo mawakili hao wameamua kuchukua kwa kupeleka ombi Mahakama Kuu ya Tanzania, chini ya hati ya dharura ili Mahakama hiyo ya juu iitishe mafaili yote mawili yaliyofunguliwa kuhusu kesi ya Lwakatare, yaani faili la kesi iliyofutwa na faili lililofunguliwa baada ya kesi ya awali kufutwa, wakiiomba mahakama iangalie na kujiridhisha
Kuhusu video
Wanahabari walitaka kujua maoni yake kuhusu video na namna kesi hiyo ilivyo, hasa kutokana na alivyoielezea charge ilivyo defective, ambapo Wakili Lissu kwa maoni yake, alisema kuwa kuna masuala mengi yanatakiwa kuwekwa wazi kuhusu video yake, akihoji maswali kadhaa:
- Nani aliyemrekodi Lwakatare? Je, Lwakatare alijua kuwa anarekodiwa? Je, aliruhusu? Kama hakuruhusu, ilifanyika kihalali? Je, haivunji katiba ya nchi inayozungumzia privacy ya mtu? Je, baada ya kurekodiwa mkanda huo ulipelekwa wapi? Nani alikuwa nao? Je, umefanyiwa uhariri (editing) na nani? Je, aliyemrekodi alitumwa na nani?
Ushahidi mwingine
Ameongeza kuwa, video inaonekana imechukuliwa tarehe 28 Desemba, siku iliyofuata, Desemba 29, kwenye kipindi cha TV, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akaanza kusema kuwa anayo video ya viongozi wakuu wa CHADEMA wakipanga mipango ya mauaji ya dhidi ya Watanzania.
Amezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.
Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.
Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.
===========
Habari hii unaweza kuisoma kwa kirefu -> Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA wafunguka! | Fikra Pevu