Wana JF!
Nimebahatika kuongea na moja ya mawakili wanaomtetea Lwakatare, akaniambia moja ya mashahidi wanaompango wa kuwatumia ni Mwigulu Nchemba ambapo watamtaka aelezee hiyo video yake aliyosema tar. 29/12/2012, ndiop hiyo iliyoko polisi au la! Vilevile mawasiliano yao ya karibu na Ludovick Joseph kuanzia Facebook (kumbuka hawa nimarafiki ktk FB) hadi simu walizokuwa wakipigiana vitawekwa hadharani kwa ajili ya cross qns.
Vilevile wanaangalia uwezekano wa kuomba kuundwa kwa mahakama ya Coroner kuchunguza vifo vyote na utekaji wenye utata uliotokea siku za karibuni hapa TZ .
My take!
Mwisho wa hili sakata kuna watu wanaweza umbuka kuliko ilivyokuwa imedhaniwa.
Neno la leo;
It is what we think we know already often prevents us from learning.
By Mpigania Uhuru.
It is what
Mkuu,nilikuwa ninashangaa anavyokiri kila kitu na kukataa sauti katika statement ya police.Chafya inaweza kuwa ugaidi hivi leo kama unamafua ya ndege na kwa makusudi ukaama kuyaeneza sio jinai?Kwani chafya ni ugaidi?
Na wewe nawe ni mwanasheria toka wapi? Hebu kuwa mwangalifu na maandishi yako kwanza. In tandem na sio intandem!
Hapo mkuu kuna mtu aliandaa kile kipindi i think hapo sio mtangazaji bali ni mtu mwingine undercover
Tundu Lissu siku ile alijidhalilisha sana pale mahakamani mpaka akachekwa na umati wa watu!!!
Ukisoma Post za Pasco kama wewe sio muelewa wa malengo yake hapa
unaweza kuingia mkenge ukawa kichaa
Kwan chama gan, au ni kat ya wale wanaochukua posho Lumumba?!
Tatizo lenu nyie vilaza mjajiona kama vile mko police au mahakamani mnamtetea gaidi Lwakatare.Swali lenye kiwango hilo.
elimu ya Madelu na mambo anayo yafanya havifanani kabisa!Ninawasiwasi kama hata Mwigulu mwenyewe kama anafahamu kitu alichocheza nacho kwamba kina maafa kiasi gani kwake mwenyewe,familia yake na Taifa kwa ujumla.Labda ni ile kujiona kujua sana kila kitu mwisho wa siku unaangukukiwa na nyumba mbovu.
Hio sheria unayoiongelea wengine tulihitimu zaidi ya miongo mitatu iliyopita. Tulia dogo, usilete kujua sana. Tutabanana humu humu na watoto kama nyie mnaojifanya kujua. Kudaadadeki!Wenzio wanadeal na substantive law wewe unahangaika na procedural laws, sio kosa lako ukanjanja tutakutana AGM ya TLS tufundishane zaidi bwana mdogo
Mkuu Mpaka Kieleweke,
Kwanza poleni kwa yote!.
Pili mnayo team nzuri sana ya wanasheria, lakini nashauri, mara moja moja, muwe mnasikiliza maoni ya ma layman kama sisi kupitia humu jf.
Nasikitika kuwaambia kitendo cha kufungua kesi kuhoji mamlaka ya DPP, its a wastage of time!. Mamlaka ya DPP haihojiwi na mamlaka yoyote hata rais wa nchi, hawezi kuyahoji, hivyo you are fighting a loosing battle!.
Ni kweli timu yenu ya sheria is a good team, nashauri please seek legal opinion ya best criminal lawyers around, kwa sababu baadhi ya wanasheria wenu ni politiciancs, wajiangalie wasije wakaipoliticise hii kesi kuonekana its a political case, bali muendelee kuipigania iwe abduction na sio terrorisim!.
Mwisho mtake msitake, lazima Chadema kama chama, kitoe statement kuwa whatever mashitaka yanayomkabili Rwakatare, ni yake mwenyewe kama Rwakatare, vingenevyo hali ikiachwa ilivyo, kuna hatari ya jamii kuaminishwa kuwa hayo yaliiyotendeka, yamendwa kwa maelekezo ya chama, hivyo kuja kuwaingiza hata wasiokuwemo!.
Huu ni ushauri wa bure tuu toka kwa layman.
Pasco.
Hio sheria unayoiongelea wengine tulihitimu zaidi ya miongo mitatu iliyopita. Tulia dogo, usilete kujua sana. Tutabanana humu humu na watoto kama nyie mnaojifanya kujua. Kudaadadeki!
Sawa, siku nyingine usirudie!Haya babu kanjanja ze paralegal talk to my avatar, tuache thread ya watu
Hakuna binadamu asiye mshamba hapa duniani kama unafahamu maana ya neno mshamba. Back to topic,Mkuu we ni mshamba sana, yaani una-quote maneno mwenyewe kwamba .......''video imewekewa baadhi ya maneno''......hapo hapo unafurahi eti wamekiri wenyewe kuwa sio fake.......ivi inapobadilishwa baadhi ya maneno inabaki kuwa origino.....we wa wapi aiseee
Katia timu Che Nkapa, atakuwa atakuwa huyu mwenye majina mengi..??sio rahisi Chemba kutinga mahakamani
Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.
Anaeleza kuwa kama ameshitakiwa kwa ugaidi lazima makosa hayo yawe ni ya kigaidi, ila makosa ya Kidnapping na abduction ni makosa ya kawaida ya jinai , na kama ili yawe ya kigaidi ni lazima hayo makosa yawe yamefanyika kwa malengo ya kigaidi , na hata hati ya mashitaka haina maelezo ya makosa ya ugaidi .
Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.
Aidha , ameongeza kuwa tarehe 27.12.2012 Denis Msacky alimpigia simu Lwakatare wakati akiwa njiani kurejea akitokea Kagera , akiwa Morogoro na kumuuliza kama yupo DSM , akamjibu yuko njiani.
Tatu, tarehe 29.12.2012 Mwigulu Nchemba , akiwa na Zitto na Mtatiro Star Tv , kipindi cha tuongee asubuhi ndipo alisema kuwa ana mkanda wa viongoz i wa chadema wakipanga mauaji ......sasa haya yote yatajulikana mahakamani.
Ziada .
Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .
Sasa polisi nao waliulizwa ni kwanini hawajamkamata aliyeweka hiyo you tube kwenye mitandao walitoa majibu yao na mawakili wanaendelea na uchunguzi wao.
Mkuu Bams,
Sasa naanza kupata mwanga. Kuna mdau mmoja majuzi alielezea sababu kadhaa za kwa nini ile video ya youtube iwe ni 'feki'. Mojawapo ya sababu alizoeleza ni kwamba, kuna mahali inasikika watu wanakoroga chai na kijiko kinawekwa mezani. Lakini watu hao hawaonekani na WL anaonekana anaongea tuuu, pasipo kuwa interfered na tukio la chai.
Hapa napata jibu moja; Ludo alipofika kwa WL, akikaribishwa chai na akawa anarekodi mazungumzo yao kwa simu au kwa njia yeyote na baada ya hapo akatumia hayo maneno baadhi kuingiza kwenye script lakini akasahau kufuta vijiko vikikoroga chai.
Twende mahakamani, tutayajua mambo mengi!
Cc Molemo
nobody can argue with you "bado mtoto":
join date : 13th march 2013